DOKEZO Vyoo vya Madereva Kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga ni hatari kwa afya kutokana na uchafu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni dereva wa malori yanayobeba simenti katika Kiwanda cha Simenti cha Rhino (kwa Mchina) kipo Kange Mkoani Tanga.

Vyoo ni vibovu havina miundombinu ya maji wala taa, hivyo kusababisha watu kujisaidia bila kumwaga maji na hivyo kuwa hatarishi kiafya kwa watumiaji.

Kwa ufupi vyoo hivi ni vichafu na hatari kwa watumiaji lakini wamiliki na uongozi wa Kampuni hujali kuhusu hilo kwa kuwa wao hawavitumii.

Sijapata nafasi ya kupiga picha kwa kuwa ni zaidi ya kinyaa kwa jinsi mazingira yalivyo, sisi wenyewe watumiaji ukijikuta una mzigo mkubwa wa kusubiri maeneo hayo tunaona kama tupo jela kutokana na uchafu uliopo hapo.


=================

Mwaka 2016 kiwanda hicho kilifungiwa kwa kuharibu mazingira

Sehemu ya habari ya kufungiwa kiwanda hicho ilikuwa hivi (Machi 2016)….

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (MB) amekifungia kiwanda cha kuzalisha cement na chokaa kilichopo jijini Tanga cha Rhino Cement, kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni uharibu na uchafuzi wa mazingira na kuvunja sheria ya usimamizi wa mazingira ya Mwaka 2004 na kanuni zake.

Mpina amechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya maweni kupitia diwani wa kata hiyo Joseph Colvas na kujionea mwenyewe namna ambavyo kiwanda hicho kinavyo achilia moshi mzito kwenda angani, pamoja na vumbi lisilovumilika kusambaa katika maeneo ya makazi ya wanachi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaa katika maeneo ya Shule ya Sekondari ya Don Bosco.
 
Back
Top Bottom