Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,509
- 9,296
Kivuko cha MV. Temesa, kinachotoa huduma ya usafiri wa abiria kati ya Luchelele Jijini Mwanza na Kijiji cha Ilunda, kata ya Ngoma'B' Wilayani Sengerema kilichojengwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 3 kinadaiwa kujiendesha kwa hasara kutokana na kukosa abiria.
Hatua ya kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 75, kwa siku, mapato yake hayazidi Shilingi laki 2 wakati gharama za uendeshaji zikidaiwa kufikia Shilingi laki 5, kitendo ambacho kinatajwa kuisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 10 kila mwezi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe.Mwita Waitara akizungumza baada ya kusikiliza kero za wananchi na matatizo ya miundombinu maeneo ya vivuko na bandari, amemwagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Japhet Maselle kuyafanyiakazi malalamiko yaliyoelezewa.
ITV