benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,035
Mkurugenzi Mkuu wa kituo Kituo Cha Kisasa Cha Biashara Afrika Mashariki Cathy Wang akizungumza kwenye maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam amesema kituo hicho kinatarajiwa kufunguliwa mwezi June mwakani
---
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Cathy Wang, kwenye maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu mkurugenzi huyo, ili kuwezesha na kuyaongeza uhai maonesho hayo mwakani, China itajitolea kuonesha uzoefu wake katika ukuzaji wa viwanda, maendeleo endelevu, kutanua wigo wa fursa na kutatua changamoto za kibiashara zinazohusiana na nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini, Chen Mingjian, amesema Idara ya Biashara ya Mkoa wa Shandong ilisaini hati za ushirikiano wa kimkakati na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ya Tanzania na TCCIA, ili kuimarisha mazungumzo na ushirikiano wa kina baina ya pande hizo mbili.