Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,303
- 12,852
Sias zina unafiki sana. Siku zote wanasiasa wanatanguliza maslahi yao, wasikudanganye vinginevyo. Suala la kuruhusu mgombea binafsi liliamuliwa na mahakama kuwa ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi. Bahati mbaya CCM wakalipindisha. CHADEMA nao katika kupigania kote tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi hawajawahi kugusia suala a mgombea binafsi.
Ukweli ni kuwa mgombea binafsi ni mwiba mkali sana kwa vyama vyote vya siasa. Mgombea binafsi itavipunguzia nguvu vyama hivi, matokeo yake wameona ni bora wakalie kimya ukiukwaji wa haki ya kikatiba. Mahakama inabidi ikazie utekelezwaji wa haki hii ya kiraia.