Kitu gani haswa kilisababisha Mhadhiri Msaidizi wa UDSM Andrea Hange ajiue Sweden?

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Wadau wa JF nimebaki najiuliza sababu zilizomfanya Mhadhiri Msaidizi wa UDSM ajiue?
Mhadhiri huyu ambaye ameanzia kwenye ngazi ya ualimu wa shule ya msingi,Sekondari hadi kuwa Mhadhiri Msaidizi pale Mlimani alikutwa amejinyonga kwenye chumba chake huko Sweden alipokuwa anafanya PhD.yake... Najua kuna wadau waliopo Sweden au Wahadhiri wenzake wanaweza kutupa maelezo zaidi kwani kuna Mdogo wangu alimfundisha shule ya sekondari miaka ya nyuma MAREHEMU ALIKUWA ROLE MODEL WAKE!
Nawasilisha.
 
Hakuacha ujumbe wowote. Hivyo ni ngumu kujua sababu. Jamaa aliamua kutuachia maswali ambayo "marking scheme" yake aliondoka nayo. Poleni sana kwa wale wote tulioguswa na kifo chake.
 
Tutajua tu, wenzetu ktk forensic investigation hawana longolongo wala ubabaishaji.

Cha msingi ndugu zake wakomae kuwa ufanyike uchunguzi wa nini kilichosababisha/kiini cha kifo cha mzazi/ndugu/jamaa yao. Wasiisubiri Serikali, kwasababu kama serikali ya Tz ina mkono basi watatafuta namna ya kuziba ukweli usijulikani. Cha muhimu nafikiri ni kufanya mawasiliano na ubalozi wa Sweden nchini.
 
uh,kuna mtu kashajiua?hawa wanfunzi their friend of mine na sijawahi kusikia tatizo,kwanini yeye ajiue?
Aisee wabongo tuache kuwatwika mzigo raia wengine,this can bring us nowhere
fight strive for your life
 
Amehojiwa mhadhiri mmoja main campus akadai amekufa kifo cha kawaida kama binadamu wengine! zipo tetesi kuwa (believe or not) kuwa msongo wa mawazo ndo umemuondosha baada ya defence ya PHD yake kuwa ngumu. Hizi shule nazo zina mambo yake. Mtu anakuwa na expectation za juu kisha mwisho wa siku mambo yanagoma, Mungu na ailaze roho yake mahali pema peponi kwani yeye ametangulia na sisi tutafuata.
 
Hizi shule haishangazi kwani PhD ni mateso jamani mungu amsamehe na poleni wafiwa ila inasikitisha sana kama ni kweli ingelikuwa vizuri tukapata taarifa kamili ni nani na ametokea idara gani pale UDSM ili kama tuna chochote tuwapelekeee ndugu na jamaa
 
Ukisikia mtu ana PH.D ya ukweli ujue amepata mateso makubwa mpaka amefika hapo; sio hawa wenzetu wanapata udokta wa kulipana fadhila!! It is possible kuwa pengine alikuwa depressed baada ya kushindwa kudefend thesis yake na akaamua kusepa!!
 
Amehojiwa mhadhiri mmoja main campus akadai amekufa kifo cha kawaida kama binadamu wengine! zipo tetesi kuwa (believe or not) kuwa msongo wa mawazo ndo umemuondosha baada ya defence ya PHD yake kuwa ngumu. Hizi shule nazo zina mambo yake. Mtu anakuwa na expectation za juu kisha mwisho wa siku mambo yanagoma, Mungu na ailaze roho yake mahali pema peponi kwani yeye ametangulia na sisi tutafuata.

Kwa UDSM, SUA na MUHAS mhadhiri akifeli masomo ya kiwango chochote (Masters au PhD) kibarua kinaota nyasi!
 
Aisee kusoma PhD ukiwa mzee wa miaka 33 na kwenda mbele ni mateso kweli kweli. Katika kipindi hicho familia inakuwa na umuhimu mkubwa sana kwenye maisha yako, na huku kila leo spidi ya teknolojia inakwenda kwa kasi katika kila fani ya elimu.

Kwa akina mama challenge ndiyo inaongezeka zaidi. Pengine familia imebakia nyumbani na baba mwenye nyumba ni kicheche basi balaa tupu.

Namfahamu mdada mmoja baada ya miaka mitano alishindwa PhD, amerudi nyumbani nyumba ndogo imeshamiri, basi amechanganyikiwa kabisa.
 
Mzumbe wanaokoteza tuu wahadhiri hata wenye PHD za kwenye mtandao

Acha uongo wewe. problem iliyowakuta wahadhiri wa mzumbe ni kusoma chuo ambacho hakikorecognized by tcu, na wengi wao wamesharudia kusoma phd wanakaribia kumaliza na wengine wameshamaliza. ni tatizo ambalo linaweza kumkuta mtu yoyote yule, kwahiyo usigeneralize kuwa wahadhiri wote wa mzumbe wapepata phd za kwenye mtandao
 
Hizi shule haishangazi kwani PhD ni mateso jamani mungu amsamehe na poleni wafiwa ila inasikitisha sana kama ni kweli ingelikuwa vizuri tukapata taarifa kamili ni nani na ametokea idara gani pale UDSM ili kama tuna chochote tuwapelekeee ndugu na jamaa

Alikuwa Mhadhiri wa Physical Studies kama alivyokuwa Super Coach Mziray!
 
Back
Top Bottom