Kitila Mkumbo awashangaa Upinzani wanaotetea vihiyo

Pale issue ilikuwa ni kuwatoa hao anaosema wana 4 na zero na kuwaacha wenye sifa waendelee, mbona rahic tuu jamani!? Tawi bovu dawa sio kung'oa mti na mizizi yake
Hiyo ndio tafsiri halisi ya kukurupuka.
 
Kwanini asishangae magufuli kudai amekuta barabara hewa wakati ni yeye mwenyewe ndiye amezijenga miaka yote hiyo ya uwaziri was Ujenzi!!!

Kujipendekeza kwingine ni majanga.
 
Kitila ni mchumia tumbo, uchu wa madaraka. Watanzania msiwe wepesi wa kusahau! Huyu alitimuliwa CHADEMA kwa ajili ya kutaka kufanya "mapindizi" kutafuta madaraka kwenye chama. Maadamu amempata rais anayetaka watu wa kujikomba, atafanya "vituko" vingi!

wengine wakitaka madaraka ni uchu ile mwenyekiti wenu ni sawa tu,
 
Kuinyoosha elimu yetu lazima kuna watu watatimuliwa vyuoni na makazini pia hakuna namna .
Elimu yetu hii ni balaa kuna walimu wana sifa zina mashaka sana mpaka unashangaa alikuaje mwalimu
Sasa kama mtu ana D tu ya Biology na aliacha Physics na Chemistry form 2 atasomaje ualimu wa sayansi
 
Huyu kikumbo nae bogus kweli kuna MTU kawatetea ?watu wana mind the way ishu yako ya kutimuliwa ilivyokua handled basi
 
Ishu sio kutetea vihiyo..walichokuwa wanadai ni utaratibu wa kuwaondoa chuoni ambao ulikuwa umewadhalilisha utu wao..Naona watu wamehamisha magoli kutafuta siasa za maji taka
Hahaaa ngosha sio mchezo. Mnatoka kwenye mada kisha mnarudi wenyewe.
 
Tunaomjua Kitila Mkumbo, naye ni kilaza. Alimaliza PCB mwaka 1992 akefeli, akapitia njia za panya kuingia chuo na kusoma arts. Si genius kama anavyoji potray. Kwa hiyo kusona diploma na kutafuta njia ya kuingia chuo si kitu kigeni kwa Mkumbo, hata Magufuli pia. Alisoma diploma ya ualimu kabla ya kujiunga na chuo. Ni utoto kuwadhihaki watoto hao ati ni vilaza wakati mazingira ya shule yetu ni ovyo na Magufuli anajua hivyo. Mbona Jesca wake naye alipata dvs 4 mwaka 2102? Naye tumuite baba kilaza?

Rais ni baba wa watz wote, kumdhalilisha mwano hadharani kama baba si busara.

Comrade, watu mbona mnasema sana???!!!! Profesa Kitila Mkumbo tangu lini 'ameji-potray' kuwa yeye ni 'genius'? Tuwe fair jamani wakati mwingine...kupita nia za panya maana yake nini? Kama alifeli PCB na akabadilisha masomo na kuchukua ya arts na kupitia diploma kuna ubaya gani?! Kumwita mtu kilaza aliyefeli sioni ubaya wake...ni msemo uliozoeleka vyuoni..Lakini kumwita motto kilaza haina maana na ukoo wake au baba yake kilaza au vilaza..Kama huyo Jesca alipata division 4 naye pia ni kilaza...lakini mtu unaweza ukajibidisha na ukaondoka na ukilaza...
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Kitila ni mwenyekiti tangu lini? Ila naungana nae kwenye hoja
 
UNAFIKI UNATUSUMBUA SANA TANZANIA,NA KWA UNAFIKI HUU WA KITLYA SIJUI ATAIFIKISHA WAPI ACT.Unafiki mkubwa kuwabwatukia Wapinzani na kuwaacha waliowadahili watoto hao,ni unafiki kusema wale ni watoto wa vigogo,waacheni watu watetee haki za wanyonge jamani.
Acheni umbumbu nyie Mkumbo kaongea kama mtaalamu, amewakosoa pia kitendo cha kuchukua wanafunzi wengi inje ya uwezo wa chuo, yaani nyie mmekuwa mbulula kila mnadhani watz wore ni vichwa maji kama boss wenu!
 
Kitila Mkumbo naye kumbe IQ yake ipo down tatizo la kutaka huku na huku siasa mbaya sana... Kazi unataka kujikomba unataka MAdaraka unataka kazi hutaki kuacha Chagua Moja wewe... Issue sio Vilaza namna ya walivyoondolewa pale Chuoni ndio issue... so kupewa Airtime basi ndio unajishusha hadhi na kupotosha UMA ni zaidi ya Upumbavu.

How come umuite Mwenzio Kilaza tena hadharani? na wao wakikujibu kwa jina watakalo amua wao wakujibie utafurahi? au ndio mtawapeleka Mahakamani maana Sheria kwa wenzenu na sio kwenu... tunapoelekea ni kubaya sana viongozi wapo Wana act like God
 
Wapinzani na wale wa Chama Tawala walitetea logistics za kuwaondoa pale chuoni,especially wale wanafunzi walikua under 18years. Kwa kweli mimi naona hii issue inakuwa twisted kila sisiku na sababu zinazotolewa zinabadilika.Tuzidi kuliombea hili taifa letu,tukiendelea kuwalaumu wapinzani wakati haya yote yamefanyika chini ya Chama Tawala,hatuta fika.Cha muhimu ni kujisahihisha pale palipo kosewa na kwenda mbele.Sio wakati wa kutafuta mchawi.
Taarifa ya kutolewa ilitoka jioni ikiwapa saa 24 wawe wameondoka inamaana walitakiwa kulala chuoni na kuamka kwa ajili ya safari. Pale Dodoma kuna usafiri wa kuelekea eneo lolote katika nchi hii. Hivyo kulikuwa hakuna sababu ya wale vijana kukaa mpaka saa 24 ziishe. Wao walikubali kubebwa na baadhi ya wabunge ili wawatumie kupataa ujiko wakidai waliwaokota usiku wakiwa hawana pa kwenda. Ukiangalia wanafunzi waliookotwa hawafiki hamsini kati ya wanafunzi 7000. Iweje wanafunzi 6500 wawe na nauli nakuondoka wabaki hawa hamsini tu? Jibu ni kwasababu wabunge hawakuwa na uwezo wa kukaa na idadi kubwa ya wanafunzi wa kuwapatia ujiko.
Tumia akili yako kutafakari hii kadhia. Siajabu huu ujinga wa wabunge kuwatumia hawa wanafunzi kufanya siasa ndio maana serikali imechukia zoezi zima. Wahadhiri kugoma kunatetesi chadema wamo ndani ndio maana walaka wa wahadhiri uliletwa na Yercko ukitoka kwa mtu wao ndani ya wahadhiri. Ushahidi mwingine ni king'ang'anizi cha wabunge wa chadema kwa swala hili. Hata pamoja na Mh Mkamia kuwa ameomba muongozo kwa swala hili na kujibiwa bado Nasari aliongelea kitu kile kile na baada ya kukataliwa chama kizima kikasimama. Baada ya ufafanuzi ccm walikubali chadema wamekataa kwasababu hii hoja walihisi itakuwa turufu ya kuwaludisha mchezoni kwani sasahizi kisiasa wamechemsha.
 
Prof Mkumbo anatumika sana na watawal ndio maana anathubutu kuwa wazi kwenye vyama vya siasa akiwa mtumishi wa serikali! Na hakuna wa kumgusa! ZZK na Prof Wanajulikana ni vibaraka!
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO Tanzania Prof. Kitilya Mkumbo amewashangaa Wapinzani wanaowatetea wanafunzi "vihiyo" waliotimuliwa.

Aidha amesema kuwa alishawahi kuandika makala ya namna ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ila hayakufanyiwa kazi.
Hebu Lumumba lete source hapa, au ni ile kauli ya Magu jana an si unachanganya kweli habari??

Kwani umesha sign buku 7, ukanywe chai kwanza, then uridi?
 
Nyinyi ndo wale mnaofukuza ma-housegirl usiku wasijue pa kwenda.
 
Back
Top Bottom