Kiti cha umeme

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,604
Mwanamke mmoja alikuwa wa ki-leo sana kiasi kwamba sehemu kubwa ya pato lake na mume wake liliishia katika kubadilisha samani na vyombo vya matumizi ya nyumbani na kuweka vya umeme: jiko, sufuria, jokofu, radio, fagio...vyote vya umeme. Mume akawa anajitahidi kukidhi matakwa ya mke wake mpaka wakamaliza mahitaj yote. Mume akafikiri "sasa nitapumua", lakini wapi. Siku moja mke akadai:
"Mume wangu, leo nikirejea kazini nitapita madukani ninunue kiti cha umeme"
Mume wala hakujibu, alipotoka kuenda kazini hakurejea nyumbani hadi leo.
 
Back
Top Bottom