Kiteto: Ampa mimba mwanaye kwa kuwa alikuwa hataki aolewe na Wakamba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Jela miaka 30 kwa kumpa mimba mwanae

1662616583710.png

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kiteto, imemhukumu kifungo cha miaka 30, Yerenia Chidaka, mkazi wa Kijiji cha Dongo wilayani humo, baada ya kumtia mimba mtoto wake wa miaka 16.

Mtuhumiwa amekiri kosa hilo hii Septemba 7, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mosi Sasy, na kusema hataki kuisumbua Mahakama kwa kuwa aliamua kutembea na mtoto wake huyo hakutaka aolewe na kabila la Wakamba.

Aidha Baba huyo imeelezwa kuwa alipomuuliza mke wake juu ya suala la kutotaka mtoto wao aolewe na Wakamba, mkewe alimjibu kwa dhihaka kwamba kama hataki aolewe basi amuoe yeye na ndipo alipoamua kumpa ujauzito.

Alipotakiwa kujitetea, mtuhumiwa aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa shetani alimpitia kutenda kosa hilo,huku Mwendesha Mashtaka wa Polisi Mahakamani hapo Inspekta Wilfred Mollel, akisema Jeshi la Polisi halina taarifa kama mtuhumiwa aliwahi kufanya kosa zaidi ya hilo na kumwomba Hakimu kumpa adhabu inayostahiki.

EATV
 
Siku hizi kila siku balaa. Mara mauaji, mara ulawiti, mara mzazi kumlala mwanae. Wenzetu wa Pwani nadra sana haya matukio. Sie wa bara kila uchwao mabalaa.
 
Kwa hiyo alimpa mimba ili asiolewe au alikuwa hataki aolewe ili aendelee kumgeuza mke? Mi nadhani mimba imekuja bahati mbaya tu, ila mzee baba alikuwa anataka aendelee kula mayai yake bila bugudha.
 
Ustawi wa Jamii, binti anahitaji ushauri nasaha kupona kidonda chake.

Baba kawa baba mtoto wake.

kawa babu wa mtoto wake
 
Back
Top Bottom