muhosni
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 1,108
- 152
Naomba kuweka masikitiko yangu kuhusu kitengo cha mawasiliano ya umma cha Chadema hapa janvini. Watu mbali mbali wamekuwa wakilalamika na kutoa ushauri kwa muda sasa, lakini nasikitika kwamba sijaona jitihada za kuboresha kitengo hiki.
Masikitiko yangu yamejikita zaidi kwenye maandamano na matukio makuu ya Chadema hasa yale yaliyotokea kuanzia Desemba 2010 hadi leo.
Tunaambiwa kwamba kikao cha uchaguzi wa Meya Arusha mjini kilikuwa na vurugu. Hatukupata picha hata moja hadi leo. Tukaambiwa kwamba katika kikao hicho Godbless Lema alipigwa na polisi. Picha pekee tuliyopata ni ile ya Godbless Lema akiwa amelazwa hospitalini
Kukawa na maandamano tarehe 5 Januari, picha tulizopata ni zile za kuokoteza kutoka kwa washabiki tu. Polisi walichakachua picha zoa wakatuonesha lakini Chadema hawajawahi kutuonesha chochote. Kuna watakaodai kwamba TV za Tz hazikubali kurusha vipindi vya Chadema. Mimi nitasema kwamba teknolojia imekua, kuna YouTube, na pia blogs kama JF. Zisambazwe kwa CD.
Tarehe 12 Januari kukawa na mazishi ya waliouawa na polisi. Hadi leo hatujapata picha rasmi kutoka chadema.
Kumekuwa na maandamano yaliyoanzia Mwanza na jana yalikuwa Mara. Hali ni ileile.
Wakati wa tukio, tunapewa taarifa na members pengine na viongozi kama Regia kwamba ni nini kinachoendelea. Lakini hatupati picha za kuanzia mwanzo wa tukio hadi mwisho. Na hatuoni jukumu la kitengo cha mawasiliano ya umma katika hili.
Sipingi wakereketwa na wapenzi kuturushia picha moja au mbili (baada ya kuchelewa na kuomba sana). Sipingi wakereketwa na wapenzi wa Chadema kutupa updates za kinachoendelea kwenye tukio fulani. Tungeweza kupata zaidi kama kuna kitengo rasmi kilichopewa vifaa na kina watendaji waliofuzu kutumia teknolojia ya kisasa.
Kama tungekuwa tunapata picha na taarifa za tukio kadri linavyotokea, polisi na ccm wasingeweza kudanganya wananchi kirahisi. Lakini sasa hivi jambo kubwa linatokea halafu kinachofuata ni malumbano ya maneno kati ya serikali/ccm/polisi na Chadema. Kama vile bado tunaishi katika karne ya 17.
Kuna swala la kutunza kumbukumbu pia, sijui matukio haya makuu yenye historia ya nchi yetu yatakuwa yamehifadhiwa vipi.