StricklyBiz
New Member
- Jan 4, 2015
- 4
- 0
Binafsi sijafurahishwa na sijui kitu gani kingine cha kufanya katika nafasi niliyonayo kama mwanafunzi kuzuia jambo hili kutokea tena zaidi ya kuandika hapa. Leo nimeshuhudia Lecturer wa hapa chuoni akimshushia kichapo kikali ikiwemo ngumi na vibao mwanafunzi mwenzangu hapa chuoni (DIT).
Chanzo kikubwa ni kuwa, Lecturer huyo alikua akifundisha lecture room jirani, wakati ambapo kulikuwa na discussion ya darasa zima ikiendelea katika lecture room tuliyokuwemo. Alituomba kuondoka maana discussion yetu ilionekana kuleta kelele na kumsumbua wakati akiendelea na kipindi chake. Tulitii na wakati watu wakiendelea kutoka nje kuna baadhi waliendelea kufungasha vitu vyao ikiwemo laptops na vitu vingine kama madaftari, mmoja wao akiwa muhusika ninaye mzungumzia katika thread hii. Mwalimu kuona kuna watu bado wanafungasha vitu sijui alikua ana mawwazo gani siku ya leo, maana moja kwa moja alianza kumrushia maneno ya fedheha. Baada ya hapo kilichofata zilikua ni ngumi na vibao akimsukuma kuelekea nje, Lecturer alionekana mwenye hasira na sababu pekee niliyofikiri kwa muda huo ilikuwa ni kuchelewa kwa wanafunzi kutoka nje ya hiyo lecture room. sijapenda kuona mwanafunzi akidharirishwa namna hiyo bila kufanya kosa lolote la msingi, na hata kama angekuwa na kosa sidhani kama lecturer ama mtu yoyote ana mamlaka kisheria ya kumpiga mtu mwingine namna hiyo. Leo imetokea kwa rafiki yangu, na ameamua kutochukua hatua zozote ukizingatia lecturer huyo huyo anatufundisha semister hii, kesho inaweza kutokea kwangu ama kwako.
kama titile inavyojieleza karibu.