BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Kuna mazoezi ya kulala chali huku umenyooka mwili wote hata kwenye carpet. Wakati umelala chali mikono umeinyoosha kuelekea miguuni, unainyanyua juu miguu yote miwili kwa wakati mmoja huku ikiwa imenyooka halafu mkao wako unakuwa kama herufi ya L, halafu huku umelibana tumbo unairudisha miguu chini taratibu hadi kwenye carpet. Halafu unarudia tena hivyo hata mara 10 au zaidi kutokana na pumzi yako. Ukiweza kufanya hivi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni utaona tumbo linaanza kupotea taratibu. Siku utakayoanza kesho yake utaisikia misuli ya tumbo inauma, usipumzike ingia mtamboni tu. Baada ya mwezi utasuuzika roho yako na matokeo lakini pia inabidi ubadilishe life style hasa kwenye makulaji na mvinyo kama unakamata. Kila la heri