Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

Pitio la Kitabu

Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha “uongo” wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo “penye ukweli uongo hujitenga.” Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, “The Nationalist” chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na “Uhuru” yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa “The Tanganyika Standard” na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika “Sunday News” akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. “The Standard” na “Sunday News” wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake “Conflict and Harmony in Zanzibar” na kitabu cha Mohamed Said “The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.” Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
Nakiri sijakisoma kitabu hiki ila nitajitahidi nikipate.
Nimepitia michango mingi iliyotolewa na tayari upotoshaji unaonekana.
Naamini kinachopiganiwa ni historia kutokupotoshwa.
Tumeona katika mapinduzi ya Zanzibar John Okello akiwa amekaa kwenye kiti wakati kina Sei Bakari wakiwa wamesimama ikionyesha ya kuwa alikuwa ni mtu muhimu lakini waandika historia wameamua kumfukia kabisa asionekane kwenye historia ya Zanzibar,naamini lengo la mwandishi ni kuziba pengo lahistoria.
Pia tujitahidi kuwashukuru watu ambao wameamua kuchimbua na kutumia muda wao kutuandikia historia.
 
books


No doubt...
 
mi sioni sababu ya malumbano as kila dini ikisema ile historia yake na jinsi ilivyo changia uhuru itakuwa ni tatizo nyerere alitokea kuwa mfuasi wa dini ya kikristo ila si raisi wa wakiristo na wala akupigania uhuru wa wakristo bali tanzania sasa hapa tatizo kubwa ni nini...... Kuna wa2 kama Field Marshall John Okello je mchango wake inakuwaje? mi naona 2gange ya jayo 2 kutoka Magamba State into Tanzania
 
mi sioni sababu ya malumbano as kila dini ikisema ile historia yake na jinsi ilivyo changia uhuru itakuwa ni tatizo nyerere alitokea kuwa mfuasi wa dini ya kikristo ila si raisi wa wakiristo na wala akupigania uhuru wa wakristo bali tanzania sasa hapa tatizo kubwa ni nini...... Kuna wa2 kama Field Marshall John Okello je mchango wake inakuwaje? mi naona 2gange ya jayo 2 kutoka Magamba State into Tanzania

Ijuwe Historia ya ulikotoka ili ujuwe uko wapi na uweze kupanga unaelekea wapi.
 
Nchi hii na watu wengine bwana...wamechanganyikiwa jumla jumla...kila kukicha ni kuongea hadithi za kufikirika
 
Siku kama ya leo tarehe 13 october 1967, kijana mmoja shupavu na shujaa katika historia ya nchi ya Tanzania alzikwa katika makaburi ya kisutu.
Alikuwa ni abdulwahid sykes aliyewapokea nyerere na mkewe walipokuja kwa mara ya kwanza jijini dar-es-salaam.
Gerezani yote ambako abdulwahid sykes aliishi katika utoto wake na mahali ambapo alianza harakati zake dhidi ya uingereza ilikuwa kama vile imesimama, hakuna kilichoendelea siku hiyo zaidi ya maziko ya abdulwahid, siku hiyo gerezani ilikuja kumzika shujaa wao.
Nyerere alihudhuria mazishi hayo ya aliyekuwa rafiki yake wa zamani na huzuni tele zilimjaa..ilikuwa ni mwaka 1952 abdulwahid alipofahamiana na nyerere na yeye abdulwahid akamjulisha kwa watu mashuhuri wa dsm.
Pumzika pema peponi abdulwahid sykes, huku kesho nyerere nae anatimiza siku ya kufa kwake kwa sikukuu, wewe umesahaulika..lakini upo kwenye mioyo yetu kwa wema wako..dua zetu zipo na wewe.
 
Nina kitabu kingine njiani chaja Insha Allah "Broken Dreams" mambo kati ya 1940 hadi leo. Utawaona wazee wetu walivyoteswa na ukoloni.

Vuta subra.

Nasikitika nimeandika Kiingereza na hili litaathir usomaji hadi ipatikane tafasiri yake.

Vipi, kimeshatoka au tuvute subra?
 
Acheni ujinga...BROKEN DREAMS ...?mliota nini hamjapata..km mliota uhuru Nyerere aliuleta..km mliota kuwekeza ktk siasa ili uhuru ukipatikana basi mle miguu ikiwa juu bora mngenunua hisa....mwambie JK amkuze,mwinyi si alipita?Mbona mlimkuza MKWAWA,KINJE NA ABUSHIR pamoja na kuuza watumwa mkaficha majina ya dini zao ili waonekane walipigania uafrica...kwani hamkuweza kwa huyu jamaa...mohamed said ni laana nyingine ktk hii nchi.
 
Siku kama ya leo tarehe 13 october 1967, kijana mmoja shupavu na shujaa katika historia ya nchi ya Tanzania alzikwa katika makaburi ya kisutu. Alikuwa ni abdulwahid sykes aliyewapokea nyerere na mkewe walipokuja kwa mara ya kwanza jijini dar-es-salaam. Gerezani yote ambako abdulwahid sykes aliishi katika utoto wake na mahali ambapo alianza harakati zake dhidi ya uingereza ilikuwa kama vile imesimama, hakuna kilichoendelea siku hiyo zaidi ya maziko ya abdulwahid, siku hiyo gerezani ilikuja kumzika shujaa wao. Nyerere alihudhuria mazishi hayo ya aliyekuwa rafiki yake wa zamani na huzuni tele zilimjaa..ilikuwa ni mwaka 1952 abdulwahid alipofahamiana na nyerere na yeye abdulwahid akamjulisha kwa watu mashuhuri wa dsm. Pumzika pema peponi abdulwahid sykes, huku kesho nyerere nae anatimiza siku ya kufa kwake kwa sikukuu, wewe umesahaulika..lakini upo kwenye mioyo yetu kwa wema wako..dua zetu zipo na wewe.
sijui ulitaka akumbukwe vipi?...au alishakuwa teja nini.....mbona sioni nini mlitaka apewe au nani ndiye alistahili mkumbuka ili mridhike..?mwinyi,JK, mkapa,Nyerere au ..?
 
Naam kumekucha.

Sheikh Suleiman Takadir (Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Makao Makuu, New Street Dar es Salaam) alikuwa akipanda jukwaani pale Mnazi Mmoja siku za mwanzo za TANU alikuwa anaanza na kibwagizo hiki: "Kwaaaacha!" (yaani kumekucha) na wananchi wana TANU wakijibu kwa pamoja: "Kweupeeee." Kisha anasoma dua halafu anamkaribisha Mwalimu Nyerere kuhutubia.

Yote haya utayapata katika kitabu hicho.

Hakika kumekucha.
Ngoja nitoe dukuduku langu kwa mzee wangu @ Mohamed Said hebu nikuulize,
  1. je kitabu chako umemlenga nani asome yaliyomo, kama ni vijana je vijana wako dar peke yake, kama ni waislamu je wako dar peke yake??? kimsingi unatunyima watu wa mikoani haki ya kujua historia ya nchi yetu.
  2. nadhani huna sababu ya kujitetea kwa nini vitabu vyako havipo mikoani, kama una sababu niambie kwa nin CD's zako zinatufikia. akhsante. kimsingi nakihitaji sana hiko kitabu
 
Bill Shankly,

Liverpool Manager wa 1970s.

Hajapatapo kuona manager kama yeye.

Usitishike na hicho unachoita "udini." Mimi naandika historia kama ninavyoijua.
Ikiwa wahusika wa jamvi hili wataona labda sielimishi na wakanipiga marufuku
hiyo itakuwa bahati mbaya.

Situkani wala sikejeli mtu.

Napenda majadiliano tuondoe nakama inayokabili nchi yetu.
Nimekisoma mara mbili na bado kila nikisafiri huwa nakisoma baadhi ya maeneo.
Mambo mawili makubwa nimeyaona,
La kwanza ni kuwa Nyerere aliliona suala la upungufu wa elimu kwa Waislamu hata kabla ya Uhuru.
La pili ni kuwa kuna upotoshaji mkubwa kuhusu historia ya nchi hii na mwandishi ameandika kitabu baada ya kufanya uchunguzi,kusoma nyaraka nyingi na kuhojiana na watu tofauti hivyo si vizuri kupuuzwa.Tumeona Okello anavyofutwa katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom