Kitabu cha "One by One"

Bazobonankira

Senior Member
Jan 18, 2007
120
61
Wazww wa kazi,

Kuna kitabu nilipata kukisoma miaka tele hapo nyuma, kikiandikwa na Mkenya mmoja mtundu sana ambaye kwa bahati mbaya siwezi kukumbuka jina.

Kitabu hicho kinaitwa One By One, basically kinazungumzia binti ambaye alilaanika kwa vitendo vya ngono na hata kuogopwa katika jamii aliyokuwapo. Ilifika hata wakati akawa anaogopwa na watu kwa kuamini kuwa kukutana naye ni mkosi.

Mtindo wa uandishi ulikuwa wa kishairi zaidi.

Tafadhali sana kama kuna mwenye kumbukumbu na taarifa muhimu juu ya mwandishi na kitabu hicho kwa ujumla tusaidiane. Pia ikiwa kuna anyeweza kuweka nakala humu, abarikiwe sana.

Wasalaam!!

Bazooo
 
Sitaki kuamini hata kidogo kuwa hakuna aliyewahi kusoma au kusikia juu ya kitabu hiki.

Msaada jamani!! Lol..
 
Sitaki kuamini hata kidogo kuwa hakuna aliyewahi kusoma au kusikia juu ya kitabu hiki.

Msaada jamani!! Lol..

Tupo. Huyo ni David Maillu ambaye pia alitunga 'After 4.30', 'Unfit for Human Consuption', 'My Dear Bottle' 'One by One' na vingine vingi ambavyo nimevisahau kidogo. Hivyo nilivyotaja hapo vilipigwa marufuku na serikali ya Tanzania kwenye miaka ya 70 kutokana na sexual content zake! Kuhusu namna ya kukipata natumaini wengine watajazia.
 
Yes, ni David Maillu, Hata mimi navitafuta sana hivyo vitabu, naungana na Mkuu Bazobonankira, mwenye kujua jinsi ya kuvipata atoe msaada pls!
 
Babadeci, nimekukubali mkuu. Wallah sikuweza kumbuka kabisa jina la mwandishi wa kitabu hiki. Thanks a lot babake.

Pia by now nimeweza kupata site yake David Gian Maillu - Home .

Sote sasa tunaweza pitia na kufahamu mengi zaidi juu yake na kazi zake.

Sasa naingia porini kusaka nyoka, I hope in few days nitaweza kupata nakala ya kitabu hiki kutoka kwa wadau fulani fulani hapa town.

Punde ntakapokipata, ntajaribu kushea na wadau wote baadhi ya interesting pages from the book.

Wasalaam!!
 
babadeci, nimekukubali mkuu. Wallah sikuweza kumbuka kabisa jina la mwandishi wa kitabu hiki. Thanks a lot babake.

Pia by now nimeweza kupata site yake david gian maillu - home .

Sote sasa tunaweza pitia na kufahamu mengi zaidi juu yake na kazi zake.

Sasa naingia porini kusaka nyoka, i hope in few days nitaweza kupata nakala ya kitabu hiki kutoka kwa wadau fulani fulani hapa town.

Punde ntakapokipata, ntajaribu kushea na wadau wote baadhi ya interesting pages from the book.

Wasalaam!!

i salute you for this. I read maillu's books while at ilboru high school, fom six
 
Tupo. Huyo ni David Maillu ambaye pia alitunga 'After 4.30', 'Unfit for Human Consuption', 'My Dear Bottle' 'One by One' na vingine vingi ambavyo nimevisahau kidogo. Hivyo nilivyotaja hapo vilipigwa marufuku na serikali ya Tanzania kwenye miaka ya 70 kutokana na sexual content zake! Kuhusu namna ya kukipata natumaini wengine watajazia.
Vitabu hivyo vilikuwa moto kweli,nakumbuka "son of women" sikumbuki vizuri kama nacho aliandika pia nakumbuka Kiunyu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom