Wadau, ningependa mnifahamishe usahihi wa maneno ONYESHA n ONESHA...
Kwa mfano sentensi ipi ni sahihi kati ya hizi?
> CHADEMA YAONYESHA DEMOKRASIA
> CHADEMA YAONESHA DEMOKRASIA.
Aksanteni sana.
Yote yapo sahihi na yanatumika, ingawa kimantiki onesha ni sahihi zaidi (linatokana na mzizi -ona).
Lakini kinachosisitizwa ni kwamba, kama mwandishi ametumia 'onyesha' basi iwe hivyo hivyo bila kuchanganya-changanya na 'onesha'.