KISUTU: Ndama Shabani Hussein (Pedeshee Ndama) jela miaka 5 au faini 200 milioni

Sheria za tanzania bana mtu kaiba mabilioni faini mil200?? Hii sheria inayosema hivi ina akili gani?? ndio maana ufisadi hauwezi isha nchi hii
 
Mkuu hiyo ilikua ni mbinu tu ili apate hii hukumu yenye option ya faini au kifungo , nina uhakika anakusudia kulipa hiyo faini watachangishana wapigaji wote watamtoa magereza atarudi barabarani kuendelea kuwapiga wazungu.
Naifahamu hii shuhuli yao vema.
Kwa kosa kama la kwake sheria ya Tanzania namba 12 ya mwaka 2006 ya anti money laundering sehemu ya 3 kifungu cha 12&13 adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 10 na kutopungua miaka 5 jela au faini isiyozidi million 500 au kupungua million 100 za kitanzania.
 
Aina mpya ya wahalifu waungwana, hawaisumbui Mhakama kwa kukataa makosa waliyotenda bali wanakiri. I wish na wezi wa serikalini walioingia mikataba ya madini na IPTL wangeiga mfano huu!
Ndama anajua hana namna...anakutaka huku nje vibaya. Anawakosa Yanga wakicheza
 
Hizi sheria zetu bwana, mtu katakatisha dola 540,000 lakini faini anapigwa milioni 200. Ngoja tuone kwenye mashitaka yaliyobaki itakuwaje
 
Umetakatisha 1.181b na faini 200m mbona wanapromote kutakatisha fedha za kigeni!
 
Nilivyokuwa nasikia "kosa la kutakatisha pesa" likitisha nikajua kwamba lazima aliyebambika apigwe mvua za maisha, kumbe dah......!!!
 
mtu katakatisha mabilion...ila faini milion 200 tu.. hata mwehu gani hapo analipa faini tu
Mkuu kutakatisha sio wizi , si afadhali yy hiyo , mbona wanasiasa wanaingiza hasara mamilioni wanapewa adhabu kidogo au hawahukumiwi kabisa , kama unabisha ngoja tuone wanasiasa waliotuingiza king kwenye madini
 
Adhabu faini 200m kwa kutakatisha 1.8bn. Ndio maana alikiri alishajua kitakachofuata.
Kufanya pesa ilitoka kwenye source A ionekane imetoka source B, yaani ilitokane shughuli isiyo halali unaifanya ionekane imetokana na shughuli halali , mf umeuza madawa ya kulevya then hiyo ukajenga guest na kupangisha ukapata pango , money laundering involves three stages placement , layering and integrations.kwa Leo naishia hapa nitafute siku nyingine tutaendelea
 
Kwa kosa kama la kwake sheria ya Tanzania namba 12 ya mwaka 2006 ya anti money loundering sehemu ya 3 kifungu cha 12&13 adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 10 na kutopungua miaka 5 jela au faini isiyozidi million 500 au kupungua million 100 za kitanzania.
Kama maximum penalty ni 500M na minimum ni 100M, hakimu kapiga 200M ili asionekane kavuta hela lakini hapo ana 200M yake imetulia huku ndama akisave 100M.

Ndama ametakatisha 1.2B, akitoa 300M kwa ajili ya kesi anabakia na 900M za kula, kwa nini kesho asirudie?
 
Hizo faini ni mapato ya sirikali (serikali).
Ukiongeza zile za trafiki tutafika tu.
 
Ingawa 200M ni ndogo kwake but its a right move, alitakiwa aongezewe kipengele cha kufungwa 10yrs akikutwa na kosa jingine within hiyo 5yrs atakayokaa nje.

Hapo itamlazimisha awe mwanachi mzuri (for atleast 5yrs)
 
Back
Top Bottom