Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,024
- 1,616
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Rashid Mustapha Makocha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 10,000 (Elfu Kumi)
Akisoma hukumu katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isaac Mlowe amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea #Rushwa na kosa la kumshawishi Mkulima ili aweze kumsajili kwenye Daftari la Wakulima ili awe mnufaika wa Mbolea ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali
Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini.
Chanzo: TAKUKURU