KISUTU: Ndama Shabani Hussein (Pedeshee Ndama) jela miaka 5 au faini 200 milioni

Kwa hilo itakuwa furaha kwa Ndama kwa kuachiwa bila shida, wanasheria wake walikaa vizuri kujua mapengo yapo wapi.. safi sana kwao

Kivingine, inamaanisha kwamba mchezo huu kumbe mtu anaweza kutoka kiurahisi hivi...

Naona watakamata na watakubali kosa, na mchezo utaendelea kama kawaida.

Huyo jaji duh!!!! au sijui ni sheria yetu kumbe bado bomu kabisaaaa

Serikali bado mna kazi kubwa sana kwenye mengi, mkitaka yasitendeke na ifunze wengine.
 
Asante mkuu so kwa maana nyingine walifatilia vyanzo vya hela z ndama na kukosa jibu kazipataje so akashtakiwab,,sasa hapa ndo nimeelewa mana nilidhan ndo kapiga dil tu kumbe za kitambo

Yap wamefuatilia vyanzo vya mapato wakakosa majibu , so ndo maana kashitakiwa na kesi ya utakatishaji wa Pesa.
 
Unauza madawa au unafanya dili haramu kama kuuza nyara za serikali au utapeli sasa ile hela utakayoipata ambayo imetokana na hizo deals unaenda kuweka bank au kuwekeza kwenye biashara huo ndo utakatishaji wa pesa
Shukran kwa kunijuza
 
Nchii hii maskini tu ndo atasota jela! very soon tutamuona kitaani papaa..
 
Ndio maana nikasema 'muungwana', kwamba kuanzia sasa hata mtaani atatambulika kama mtakatisha pesa. Isije ikawa kama yule jamaa aliyewahi kuiba pesa za umma na kufungwa jela alafu alivyomaliza kifungo akakata rufaa na kufutiwa maskosa then akatumia hiyo gear kugombea ubunge na akaupata aisee!
Rage
 
Baada ya ndama kukiri kosa la kutakatisha pesa , leo mahakama imemhukumu kwenda jela miaka 5 au kulipa faini 200 milioni.

Awali mfanyabaishara Ndama Hussein maarufu kama mtoto wa Ng’ombe alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka sita ikiwamo kughushi na kutakatisha Dola za Kimarekani 540,390 (sawa na Sh, bilioni 1.181).

1.181.000.000-200.000.000= ????????????????? Tatizo liko wapi?. Unaishi kama mfalme.
 
Asante mkuu so kwa maana nyingine walifatilia vyanzo vya hela z ndama na kukosa jibu kazipataje so akashtakiwab,,sasa hapa ndo nimeelewa mana nilidhan ndo kapiga dil tu kumbe za kitambo
Inavyosemekana ni kuwa walimwingiza mzungu wa Australia mgenge kwenye deal la dhahabu.. Akatanguliziwa hizo $lk 5.. Wanamtumia mzungu vivyuma! Faster Ndama akazichomoa dolari na kuziingiza kwenye mzunguko wa biashara zake! Mzungu mzigo ulipofika akajua tayari kalizwa. Akafuatilia na kufungua mashtaka! Kama jamaa anavyosema Kuna mashtaka zaidi ya matano hilo ndo lilikuwa halina dhamana.. Kama akilipa ashalipangua.. Hayo mengine atakuwa uraiani.. Wakati wa mjini hao mkuu!
 
Back
Top Bottom