Kisutu, Dar: Robert Kisena apandishwa Kizimbani kwa Utakatishaji fedha, asomewa mashitaka 33

Zakaria gani huyo?
I hope he is not Hans Pope Zakaria....
The dead don't tell the tales.

Zaccheus is dead!
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (UDART) Robert Kisena na wenzake watatu wamesomewa mashtaka 33 katika kesi mbili tofauti kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo Utakatishaji wa fedha na kuongoza genge la uhalifu.

Kwenye kesi namba 21 ya mwaka 2022 inawahusu Kisena na wenzake wawili ambapo ni Charles Newe na Tumaini Kulwa wanadaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu kaisi cha cha Shilingi 4.5 Bilioni huku wakituhumiwa kutakatisha na kusababisha hasara serikali kiasi hicho hicho.

Katika kesi namba 20 ya mwaka 2022 Kisena na washtakiwa wanne akiwemo Newe, Kulwa na Jonhn Samangu wanadaiwa kutakatisha kiasi cha Shilingi Milioni 750 ambazo zinadaiwa kuwa ni zao la kughushi na kulaghai.

Washtakiwa hawakuwa na haki ya kujibu chochote kwa Mahakama hiyo kwani haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo kisheria.

Watuhumiwa wamerejeshwa mahabusu ya magereza mpaka tarehe 23 Mei 2022 shauri hilo litakapotajwa.

Wote Wamekosa dhamana.

=====

UPDATES;

======

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo haraka, maarufu mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 33 yakiwemo ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia hasara Serikali ya Sh 5.2 bilioni.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Mei 9, 2022 na kusomewa kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi mbele ya mahakimu wawili tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili watano wandaamizi wa Serikali wakiongozwa na Pius Hilla akisaidiana na Jackline Nyatori, Ester Martin, Iman Mitumemingi na Upendo Temu.

Mbali na Kisena, washtakiwa wengine ni Charles Newe (48) Mkurugenzi wa Udart, mfanyabiashara John Samangu (66) na Mtunza fedha Tumaini Kulwa (44).

Septemba 13, 2019 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) aliwafutia mashtaka manne ya utakatishaji fedha washtakiwa hao na hivyo kubaki mashtaka 15 kati 19.

Kati ya mashtaka hayo 15 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa hao, yapo mashtaka manne ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo; manne ya wizi; moja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja ni kusababisha hasara UDART.

Mengine ni kuongoza genge la uhalifu, kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka Ewura na kuiba.

Chanzo: Mwananchi

Haya makesi makubwa hayanaga part two, rejea Masamaki, Gugai nk
 
Haya mambo inaonekana nyuma yake kuna mkono mrefu usioonekana.

Huyu jamaa kawekwa kati na makundi mawili ya wapigaji, moja kiongozi wao alishatwaliwa, na jingine kiongozi wake bado yupo, ndilo limeshika hatamu kwa sasa, hakika ana mtihani.
Huyo kisena si ilidaiwa ni mtoto wa jakaya!!
 
Mwaka hauishi tutakuwa nao mtaani Hawa jamaa,

Jamhuri Haina Nia ya kuendelea na kesi au kubadilishiwa mashitaka.
 
Milion 750 nadhani alimtapeli ndegesela.

Robert ni mjanja mjanja sana na binam yake kulwa na dogo lakd willi.
Uda nzima ilijaa watu wa malampaka.

Kama kwenye uzi huu atasoma ricardo nichek inbox

Kweli unaielewa hiyo familia.

Baba yake kulwa alimlea sana huyo r. kisena mwishowe huyo mzee akafariki.

Katika kulipa fadhilia na kuitunza familia, nadhani kisena akamuajiri kulwa. Yaani hadi sasa sielewi vipi kulwa yupo ndani.

Ngoja tusubiri tuone
 
Wakati watu wanafanya maufisadi yote haya, wale jamaa wa intelijensia huwa wapo wapi?

Maana pesa yote hiyo huwa haipotei kwa siku moja...
 
Unataka kuonesha nini?

Hawa kwanza watakuwa wamezitia hasara hata baadhi ya benk kwa kuchukua mikopo na kushindwa kulipa.

Wamefanya hata mradi uwe na ujanja ujanja mwingi huku ukiwapa kero wananchi.

Duh...!. Kumbe haya mambo bado yanaendelea?!.
P
 
Wakati watu wanafanya maufisadi yote haya, wale jamaa wa intelijensia huwa wapo wapi?

Maana pesa yote hiyo huwa haipotei kwa siku moja...
Inteligensia wao ni wanyetishaji tu. Hasa ya Tanzania. They do not execute. Wanaotakiwa kufanya execution ndio hao unaona wamewafikisha mahakamani.
Execution ya Intelligence is silent kama ilivyo intelligence yenyewe.
Sasa ipi bora? Kumnyamazisha mtu kabisa milele au kunshtaki mahakamani?
 
Back
Top Bottom