Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,220
Kisiwa cha Patmo kipo nchi ya Ugiriki kwa sasa…Kisiwa hicho kipo mashariki mwa Taifa la Ugiriki na magharibi mwa nchi ya Uturuki, kama vile Zanzibar ilivyo mshahariki mwa nchi ya Tanzania ndivyo kilivyo hichi kisiwa cha Patmo kwa Ugiriki.

Kisiwa hicho ndicho Mtume Yohana, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Bwana Yesu, alifungwa.

Warumi walimkamata Yohana na kumtupa katika kisiwa hicho, kwa lengo la kumtesa kwa kosa la kumhubiri Yesu. (Kwa maelezo kwa njia ya sauti, fungua hapa chini)

[embedyt]
View: https://www.youtube.com/watch?v=EhBLp-8-vPw%5B/embedyt%5D

Lengo la kumtupa Yohana katika kisiwa hicho cha Patmo, sio tu afe, bali afe kwa mateso. Kwani kisiwa hicho hakikukaliwa na mtu yeyote wakati huo, kwasababu kilikuwa ni kisiwa ambacho hakistawi nafaka, wala miti na zaidi sana, kilisifika kuwa na nyoka wengi.

Kwahiyo yoyote aliyetupwa katika kisiwa hicho, ilikuwa ni lazima afe kama hatakuja kuokolewa huko.

Lakini tunasoma, Yohana alipelekwa kule, kwaajili ya ushuhuda wa Neno la Mungu, wakati Jeshi la Warumi linaona limempeleka kwaajili ya mateso, yeye Yohana alijiona amepelekwa kwaajili ya ushuhuda…Kwamba akashuhudie mambo atakayokwenda kufunuliwa au kuambiwa na Mungu huko.

Ufunuo 1:9 “Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu”
Hii ikifunua kuwa sio kila jaribu baya, lengo lake ni baya!. Yohana asingepelekwa Patmo, tusingekuwa na kitabu cha ufunuo, hali kadhalika Bwana Yesu asingepelekwa msalabani, tusingepata wokovu.

Kisiwa cha Patmo, sasahivi kinakaliwa na watu, kutokana na kuongeza kwa idada kubwa ya watu ulimwengu na yenye kuhitaji makazi..vile vile, kuongezeka kwa teknolojia ya mawasiliano, na usafiriwa wa haraka, umekifanya kisiwa hicho kiweze kukalika na watu leo.

Kisiwa cha Patmo, jina lake mpaka leo halijabadilika, kinaitwa hivyo hivyo Patmo, kama vile Yerusalemu jina lake lisivyobadilika siku zote.

Wakazi wa kisiwa cha Patmo kwasasa hawazidi 4,000 kulingana na sensa za Ugiriki.

Na kisiwa hicho, hakina miujiza yoyote ya kiroho, kwamba yeyote afikaye kule basi atapata ufunuo kama aliopata Yohana.
 
Nimefurahia andiko.
Mungu akubariki
Amina.
Pia usiache kusoma Isaya 50:11 utajua kwanini Tanzania chini ya CCM kamwe haitokuja kuendelea. Itaishia kulala kwa huzuni.

Tayari SGR imekufa na Magufuli wake. NENO LA MUNGU ALIYE HAI HALIDANGANYI
 
Amina.
Pia usiache kusoma Isaya 50:11 utajua kwanini Tanzania chini ya CCM kamwe haitokuja kuendelea. Itaishia kulala kwa huzuni.

Tayari SGR imekufa na Magufuli wake. NENO LA MUNGU ALIYE HAI HALIDANGANYI
11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Isaya 50:11
 
Back
Top Bottom