Kisiwa cha Changuu, Zanzibar: Sehemu nzuri ya kutalii na kubarizi

Kalaga baho

JF-Expert Member
Sep 27, 2020
5,465
11,234
Habari ya muda huu wakuu..

Leo nitatoa dodoso dogo linalozungumzia histori,na maelezo ya vivutio mbalimbali vinavyopatikana kisiwa kidogo kilivhopo maili 4 kutoka unguja. Kisiwa hiki kinaitwa Changuu au Prisona au kisiwa Cha Kobe.

Kisiwa Cha prisona kilianza kujulikana hivyo, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 1890. Kisiwa ambacho kilijengwa majengo na koloni la muingereza kitumike kama gereza lakini hakikuwa gereza na hatimae majengo yake yalitumika kama hospitali kati ya 1899 mpaka 1930s.

HISTORIA
Mfalme wa kwanza wa Zanzibar alikitwaa kisiwa hiki na alikitoa kama zawadi kwa wafanya biashara wakubwa wa biashara ya watumwa ambapo kisiwa kilitumika kama reserve ya watumwa. Watumwa walifika hapa na kupunzishwa wakisubir kwenda kuuzwa huko stone town.

Kufuatia kufungua kwa biashara ya utuwa 1870s kisiwa huku kikabaki kuwa tupu. Mwaka 1885 koloni la uingereza lilifanikiwa kutwaa afrika mashariki na kufanya kuwa chini ya utwala wake hivyo Zanzibar yote ikawa chini ya uingereza. Muingereza katika utwala wake alijenga magereza machache sana katika upwa wa pwani ya unguja, HISTORIA inaonesha magereza yaliongezwa Kati ya miaka ya 1920s hasa, gereza kubwa la Kilimani.

Uchache wa magereza haya miaka hii ya 1885-1892, ulipekea wafungwa kusongamana sana na mwaka 1895 uongozi wa kisiwa hiki ulipokea ugeni wa Lloyd Mathew ambayr alikuwa ni waziri wa kwanza wa utawala wa Uingereza kwa Zanzibar. Yeye aliona hali mbaya kwa wafungwa, msongamano ukitishia afya na kuondoa utu. Akapendekeza kujengwe gereza lingine, kisiwa Cha CHANGUU kikapendekezwa na ujenzi ukaanza.

**********************
Kutokana na mvuto wa hali ya hewan na utulivu wa hiki kisiwa. Ujenzi huu ulikumbwa na sitofahamu kubwa ya muingiliano mkubwa wa wakaguzi na wazungu wengine walifika hapa. Wakaanza kuyatumia majengo yaliyopo kama lodge au makazi ya kujichimbia. Hivyo, ujenzi ukiwa unaendelea, bangalow zikaanza kutumika. Kufikia mwaka 1896-7 kisiwa kikawa kina muingiliano mkubwa wa watu wanaokitrmbela kila wiki.

IMG_20240118_082447_361.jpg

Screenshot_20240118-100335.png
download (1).jpeg
 

Attachments

  • Screenshot_20240118-105612.png
    Screenshot_20240118-105612.png
    17.5 KB · Views: 5
  • IMG_20240118_104330_712.jpg
    IMG_20240118_104330_712.jpg
    669.2 KB · Views: 7
  • IMG_20240118_101534_144.jpg
    IMG_20240118_101534_144.jpg
    743.7 KB · Views: 5
Katika kipindi hiki pia, kama nilipokwishasema hapo juu kwamba, Muingereza alijitwalia Afrika Mashariki yote hii. Kunako mwaka 1889-1890s Muingereza alitamani sana kuijenga Afrika mashariki kuwa rafiki katika uzalishaji wake, aliona haja ya kuunganisha nchi hizi kwa miundombinu. Miaka hii, alikuwa katika jitihada za kujenga reli kutoka Ziwa Viktoria kwenda Uganda.

Reli ile ilihitaji nguvu kazi kubwa sana. Takribani wafnyakaz 230,000 walihitajika. Watu walitoka SEHEMU mbalimbali mwa Afrika Mashariki. Wengine Tanga, Morogoro nk. Muingiliano wa watu ukawa mkubwa. Na HISTORIA inaonesha pia, ni katika kipindi hiki Cha 1880s maginhwa makubwa yalishamnulia Dunia (epidemics) ambayo ni Small pox, bubonic plague (black death) na Cholera. Haya magonjwa yalikuwa yanaenea pia kwa Kasi kufatauingiliano huu.

Waingereza wakaona haja ya kutuliza au kupunguza Kasi ya ueneaji. Wakapendekeza kuwepo na SEHEMU maalumu ya karantini. Watu wote wanaoonesha dalili au kuwa na maambukizi wawekwe pale kupata matibabu. Kisiwa Cha CHANGUU kikapendekezwa kutumika kwa minajili hiyo. Na mnamo mwaka 1899 kisiwa Cha CHANGUU kikaanza kuwa kisiwa Cha karantini kwa watu wa Afrika Mashariki na kituo Cha kupima afya wageni kabla ya kuingia Zanzibar ili kuzuia ueneaji wa magonjwa haya yaliyolipuka
 

Attachments

  • VID_20240118_090637.mp4
    30.6 MB
Ikumbukwa kisiwa kilishajengwa kwa ajili ya kuwa gereza, mahitaji ya eneo la karantini yakakibadilisha matumizi. Ikawa hospitali, baadhi ya majengo yakafanywa kuwa makazi ya wahudumh wa kisiwa hiki. Kisiwa kikapokea wagonjwa na kutibia mpaka mnano miakaya 1930s.

Kisiwa Cha changuu kilipata jina la prisona kwa sababu hii, lakini pia hakikuwahi kuwa gereza kama ilivyodhamiriwa. Hii inazalisha msemo wa "The prison, that never was"...

UTALII.
Kisiwa kwa sasa kinatumika kwa ajili ya utalii. Kuna vivutio vingi, pia na HISTORIA hii inavutia kwatu kuja kutembelea. Kisiwa kina uoto asilia, majengo kale na wannyama. Kwa sasa wannyama wanaovuma au wenye mvuto mkubwa kisiwani hapa ni Kobe aina ya giant adalbra, pia Kuna Minokela au digidigi na tausi. Kisiwa kinapolea watalii wengi sana kwa siku, hasa kwa kipindi Cha miezi ya Juni mpaka Septemba. Kwa miezi hii kisiwa hakuna watu wengi.. watalii wanaofika hapa ni takribani 100 mpaka 300 kwa siku. Wengi wanatoka nchi zinazoongea latin. Wachache Toka urusi, Wengine ufaransa na familia zao...

1. Giant tortoise / Adalbra /Geochelone gegantia
Ni Kobe wakubwa wenye aslia ya visiwan vya Shelisheli (Seychelles). Hawa Kobe huko wanaisihi porini Kwan hawaishi maenei yenye watu wengi. Kobe wa aina hii Wana fika kilo 300 na wanaofikisha umri wa miaka 100 mpaka 220. Pia dume huwa na maumbo makubwa wakati wa kike Wana umbo dogo....

Hawa Kobe visiwan Shelisheli wanapatikana sana maeneo ya Malabar na Picardo. Hawana asilia ya Zanzibar, walifika Zanzibar kwa njia ya usafirishaji wa kibinadamu. Ambapo, mwaka 1919 uongozi wa visiwan vya Shelisheli ulitoa kwa uongozi wa Zanzibar kama zawadi. Mpaka sasa, Kuna Kobe mmoja AmBae alitolewa kipindi hiko anaishi hapa.

Kobe Hawa wana sifa ya kuishia muda mrefu sana. Kadirio lao la kuishia ni miaka 60+ na huanza kupevuka wakiwa na miaka 25-30. Hawa Kobe hawana ukomo wa kukua, hata yule mkubwa kuliko wote huwa anakua walau 2 cm kila mwaka.
Wana uzito wa kati ya kilogram 50 Hadi 200.

Kobe Hawa huishi mazingira yenye maji au matope, pia huvutiwa zaidi kuishia maeneo yenye kivuli. Hii huwasaidia kujikinga na jua na sababu ya lishe. Wanaweza kushinda bila kula zaidi ya siku 10 kwani miwili Yao mikubwa huwasaidia kutunza chakula.

Wana uwezo wa kutembea mita 800 Hadi mita 1500 tu kwa muda wa mwaka mzima. Kobe Hawa zamani walikuwa wanaliwa na watu.

Kobe hawa wakifa, huchukua siku 200 kusmabaratika kwa mifupa Yao (wadogo) na siku 300+ (wakubwa) endapo kiunzi hicho hakitakutana na kashkash zozote za kuhamishwa au miwili uliokufa kuliwa na wadudu au wanyama

Updates...
Kobe wa adabra Wana majina mengine yakiwemo geochelone gigantia au dusumieri dipsoshelis ambao huishi zaidi ya miaka 200. Katika kisiwa hiki Kobe mmoja kati ya wale wanne waliotolewa 1919 bado anaishi hapa na kwa kawaida, katika malezi yake huanza kukutana kimwili akiwa na unmri wa miaka 25.
Baada ya kupata mimba hukaa muda wa miezi (kadhaa) ili kutaga mayai. Mayai haya huchimbiwa chini au kwenye shimo, na tai lenye joto Kali huashiria kuzaliwa kwa Kobe wa jinsia Ke, joto la kawaida jinsia Me na tai ambalo hakina joto Lina ishara ya kukosa uhai, so hakuna kitakachotoka.


2. Tausi
Kisiwa kina Tausi takribani 2000.
(Updates)
Tausi dume huwa na mvuto kuliko ke. Tausi Hawa hulala juu ya miti huku vifarabga vyao kuviacha chini
 

Attachments

  • VID_20240118_090654.mp4
    10.9 MB
  • IMG_20240119_064945_066.jpg
    IMG_20240119_064945_066.jpg
    644.8 KB · Views: 6
  • IMG_20240119_064913_159.jpg
    IMG_20240119_064913_159.jpg
    528.7 KB · Views: 7
Umesahau kuongelea gharama za kutalii hapo😎
Huu Uzi wakuu ni wa changuu tu. Nitaweka hapa na Miata update kila kitu, mana sijaweka mtiririko mzuri sana mana nimejikuta tu nnashea na wadau hapa ndo mna video nachukua hapahapa naziweka.

Kutoka unguja mpaka hapa kwa boti ni dakika 30-45 tu. Nikishamaliza yote nitaweka na hesabu ya kufika hapa na nitakutembeza mm mwenyew kwa chaji ndogo tu, ya bia Moja (10 USD) hii itakuwa ofa ya wadau wa humu jf tu

Cc. Maxence Melo
 

Attachments

  • Screenshot_20240118-105743.png
    Screenshot_20240118-105743.png
    19.1 KB · Views: 5
Gharama za KUTALII na maisha ya hapa.
Kisiwa hiki hakina ruhusa ya Makazi binafsi Wala biashara nje ya mmiliki wa hiki kisiwa. Hiki kisiwa ni Mali ya serikali iliyoendelezwa na muwekezaji binafsi mwenye asili ya Italy. Kwa sasa pia amepewa kisiwa kingine kuebdeleza ili kiweze kuwa na uzalishaji. Kisiwa hiki hakina duka Wala loji ya kulala wageni, Kuna nyumba za staff tu. Wageni huja na kuondoka jioni

Kisiwa hakina duka, mahitaji ya muhimu yote yanatoka unguja na kuletwa kwa boti. Pia, kisiwa hiki kina maisha ya Kitalii, yani ghali kias. Matumizi ya kawaida ni vinywaji na vyakula pia na kulipa kiingilio na kumlipa mtembezaji.
Soda 7500
Bia 9500
Cappuccino na espresso 15000
Nk
Kuingia hapa KUTALII ni kias Cha shilingi za kitanzania 4000 kwa mtanzania na kias Cha 30 USD kwa mgeni.
Mtembezaji SI lazima, ila ni muhimu lakini pia bei zao ni marlewano huko mjini. Wengi hulipwa 10 USD mpaka 20 USD kwani sekta hii kwa Zanzibar ni cheap sana. Yeyote anawez kufanya. Wanalipia ushuru kwa mamlaka 120,000 tu mwaka mzima (kusajiliwa) na wengine wanazifanya kirnyeji tu. Kujua lugha ni muhimu zaidi... Vjana wengi wanaisihi vizuri hapa unguja kwa kazi hiyo....


TO BE UPDATED
 
Good morning Africa.
Hili ni eneo la kuingilia kisiwani na majengo mengine ni baadhi ya clinics zilizotimika kipindi hiko. Hili jengo liliprwa jina la mtu aliyrpendekeza na kusimamia ujenzi wa gereza hili. Jengo kinaitwa Mathew point

Jengo hili pia, ni Moja kati ya location zilizotumika katika nyimbo ya harmonize - Zanzibar.. ni kisiwa chenye location nzuri sana za bichi.


(More photo to be upload)
 

Attachments

  • IMG_20240119_065421_260.jpg
    IMG_20240119_065421_260.jpg
    554.7 KB · Views: 6
  • IMG_20240119_065333_851.jpg
    IMG_20240119_065333_851.jpg
    665.7 KB · Views: 6
  • IMG_20240119_065147_023.jpg
    IMG_20240119_065147_023.jpg
    713.7 KB · Views: 7
  • IMG_20240119_065139_331.jpg
    IMG_20240119_065139_331.jpg
    774.8 KB · Views: 7
  • IMG_20240119_065121_281.jpg
    IMG_20240119_065121_281.jpg
    499 KB · Views: 5
Gharama za KUTALII na maisha ya hapa.
Kisiwa hiki hakina ruhusa ya Makazi binafsi Wala biashara nje ya mmiliki wa hiki kisiwa. Hiki kisiwa ni Mali ya serikali iliyoendelezwa na muwekezaji binafsi mwenye asili ya Italy. Kwa sasa pia amepewa kisiwa kingine kuebdeleza ili kiweze kuwa na uzalishaji. Kisiwa hiki hakina duka Wala loji ya kulala wageni, Kuna nyumba za staff tu. Wageni huja na kuondoka jioni

Kisiwa hakina duka, mahitaji ya muhimu yote yanatoka unguja na kuletwa kwa boti. Pia, kisiwa hiki kina maisha ya Kitalii, yani ghali kias. Matumizi ya kawaida ni vinywaji na vyakula pia na kulipa kiingilio na kumlipa mtembezaji.
Soda 7500
Bia 9500
Cappuccino na espresso 15000
Nk
Kuingia hapa KUTALII ni kias Cha shilingi za kitanzania 4000 kwa mtanzania na kias Cha 30 USD kwa mgeni.
Mtembezaji SI lazima, ila ni muhimu lakini pia bei zao ni marlewano huko mjini. Wengi hulipwa 10 USD mpaka 20 USD kwani sekta hii kwa Zanzibar ni cheap sana. Yeyote anawez kufanya. Wanalipia ushuru kwa mamlaka 120,000 tu mwaka mzima (kusajiliwa) na wengine wanazifanya kirnyeji tu. Kujua lugha ni muhimu zaidi... Vjana wengi wanaisihi vizuri hapa unguja kwa kazi hiyo....


TO BE UPDATED

elfu 4 kwa Dola 30!!!!!!!!!!! hapo ndipo tunapofeli kwenye huu utalii wetu kwa kuvurumusha mabei ya ajabu kwa watalii
 
Updates.
 

Attachments

  • IMG_20240119_064432_875.jpg
    IMG_20240119_064432_875.jpg
    1.9 MB · Views: 2
  • IMG_20240119_064624_505.jpg
    IMG_20240119_064624_505.jpg
    2.2 MB · Views: 2
  • IMG_20240119_065421_260.jpg
    IMG_20240119_065421_260.jpg
    1.9 MB · Views: 2
  • IMG_20240119_080123_448.jpg
    IMG_20240119_080123_448.jpg
    2.5 MB · Views: 2
  • IMG_20240121_165140_839.jpg
    IMG_20240121_165140_839.jpg
    1.7 MB · Views: 2
  • IMG_20240114_125222_197.jpg
    IMG_20240114_125222_197.jpg
    2.2 MB · Views: 2
Miti
1. Mvinje (Cypress/ Casuarina)
2. Mijenga ua
3. Jasmine tree
4. French pan
5. mikunGu
6. mikoko
(To be updated)
 
Sasa elf 30 kwa mzungu si kama buku tu. Mana ni dola 12

Na hayo ndio matatizo yetu, sisi tunaona wazungu wana mahela tu kwahiyo vyovyote tutakavowavurumishia wanatoa bila ya shida.

Tunatakiwa tufahamu hao wazungu wapo wa level tofauti za kimaisha, kwahiyo sio kila mzungu atatumia tu bila ya hisabu.
Utalii ni ushindani kuna nchi nyengine ambazo zimetuzidi kila kitu kwenye hii secotr na gharama zao ni nafuu sana ukilinganisha na sisi.
Low thinking yetu ndiuo inayotuangusha, Tnabeba watalii 1m kwa mwaka tunajiona tunapata, kuna watu wana beba 10m+ kimasihara masihara tu mkuu kutokana na walivyojipanga pamoja na umakini wao.
 
Na hayo ndio matatizo yetu, sisi tunaona wazungu wana mahela tu kwahiyo vyovyote tutakavowavurumishia wanatoa bila ya shida.

Tunatakiwa tufahamu hao wazungu wapo wa level tofauti za kimaisha, kwahiyo sio kila mzungu atatumia tu bila ya hisabu.
Utalii ni ushindani kuna nchi nyengine ambazo zimetuzidi kila kitu kwenye hii secotr na gharama zao ni nafuu sana ukilinganisha na sisi.
Low thinking yetu ndiuo inayotuangusha, Tnabeba watalii 1m kwa mwaka tunajiona tunapata, kuna watu wana beba 10m+ kimasihara masihara tu mkuu kutokana na walivyojipanga pamoja na umakini wao.
Hujui kitu mkuu kuhusu utalii. Na social classes... Dollar 12 ni nyingi kwa waafrika. Ulizia bei ya bia Moja Uk ni kias gan alaf uje tuongee lugha moja
 
Hujui kitu mkuu kuhusu utalii. Na social classes... Dollar 12 ni nyingi kwa waafrika. Ulizia bei ya bia Moja Uk ni kias gan alaf uje tuongee lugha moja

sasa hiyo bia bia inayouza UK zitafafanaje na bia ya kwenu kigharama? kwa ubora upo sawa?
 
sasa hiyo bia bia inayouza UK zitafafanaje na bia ya kwenu kigharama? kwa ubora upo sawa?
Hujui lolote mkuu kuhusu class society. Kama unaijua nchi yenye utalii kuliko Zanzibar itaje tuijadili hapa, nadhani hata watu wa wizara wapi humu.. idadi ya watalii inaathiriwa na idadi ya vivutio vikivyopo. Huwez kufananisha vivutio misri au Seychelles na Zanzibar.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom