Biblia ndani ya Kisiwa cha Pitcairn

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,414
Mabaharia waasi maarufu walioizamisha meli ya Kiingereza iliyoitwa Bounty waliishia kufanya makazi yao wakiwa pamoja na wanawake, wenyeji wa eneo lile katika kisiwa cha Pitcairn katika Bahari ya Pasifiki ya Kusini.

Kundi lile lilikuwa mabaharia tisa wa Kiingereza, wanaume wa Kitahiti sita, wanawake wa Kitahiti kumi, na msichana wa miaka kumi na mitano.

Mmojawapo wa mabaharia wale alivumbua namna ya kutonesha [kugeuza kuwa mvuke] alkoholi, na baada ya muda mfupi ulevi ukaliharibu koloni lile lililokuwa katika kisiwa kile. Ugomvi kati ya wanaume na wanawake ukageuka na kuwa wa kutumia nguvu.

Baada ya kupita muda fulani mmoja tu kati ya wanaume wale wa kwanza waliofika mle kisiwani ndiye alibaki kuwa hai. Lakini mtu huyo, Alexander Smith, alikuwa ameigundua Biblia katika mojawapo la makasha yaliyochukuliwa kutoka katika ile meli.

Alianza kuisoma na kuwafundisha wengine juu ya kile ilichosema. Alipofanya hivyo maisha yake yeye mwenyewe yakabadilika na hatimaye maisha ya wote waliokuwa katika kisiwa kile.

Wakazi wa kisiwa kile walikuwa wametengwa na ulimwengu wa nje mpaka ilipowasili meli ya Kimarekani iliyoitwa Topaz katika mwaka wa 1808.

Wafanyakazi katika meli hiyo wakakikuta kisiwa kile kikiwa na jumuia inayokua na kusitawi, bila ya kuwa na pombe kali (wiski), gereza, wala uhalifu. Biblia ilikuwa imekigeuza kisiwa kile kutoka jehanamu ya duniani kwenda katika kielelezo cha vile Mungu atakavyo ulimwengu huu uwe. Na mpaka leo hii kinaendelea kuwa katika hali hiyo.

Je, hivi Mungu bado anaendelea kusema na watu kupitia katika kurasa hizo za Biblia? Bila shaka anafanya hivyo.

Ninapoandika haya, naangalia karatasi lililotumwa kwetu na mfungwa mmoja ambaye tulimuhubiri Gerezani. Maelezo chini yake yanasema hivi

“Mimi nimo gerezani, niko katika orodha ya watu wanaostahili kunyongwa, nimehukumiwa kufa kwa kutenda kosa la jinai. Kabla ya kusoma Biblia, nilikuwa nimepotea lakini sasa ninacho kitu cha kutumainia tena nimeupata upendo mpya.”

Biblia inao uwezo unaoweza kuyabadilisha kabisa maisha ya watu. Kwa kweli, watu wanapoanza kujifunza Biblia, maisha yao hubadilika kwa namna ya kuvutia sana.

Kwa kweli Biblia ni maktaba ya vitabu 66. vitabu 39 vya Agano la Kale viliandikwa kuanzia karibu na mwaka wa 1450 K.K hadi 400 K.K, Vitabu 27 vya Agano Jipya viliandikwa kati ya mwaka wa 50 B.K na mwaka wa 100 B.K.

Nabii Musa alianza kuandika vitabu vitano vya kwanza wakati fulani kabla ya mwaka wa 1400 K.K. Mtume Yohana alikiandika kitabu cha mwisho cha Biblia, yaani, kitabu cha Ufunuo, karibu na mwaka wa 95 B.K.

Katika kipindi cha miaka 1,500 kati ya kuandikwa kitabu cha kwanza na cha mwisho cha Biblia, walau watu wengine wapatao 38 waliovuviwa walitoa mchango wao.

Wengine walikuwa wafanya biashara, wengine wachungaji wa kondoo, wengine wavuvi, wengine askari, matabibu, wahubiri, wafalme – wanadamu toka katika tabaka zote za maisha. Mara nyingi waliishi katika utamaduni na falsafa vilivyohitilafiana.

Lakini hapa ndipo yalipo maajabu ya maajabu yote: Vitabu hivyo 66 vya Biblia pamoja na sura zake 1,189 zenye idadi ya mafungu 31,173 vikiwekwa pamoja, tunaona umoja na mwafaka katika ujumbe vinaoutoa.

Maandiko ya mkono ya Kiebrania yanayorudi nyuma hadi ule mwaka wa 150 mpaka 200 kabla ya Kristo yalipatikana karibu na Bahari ya Chumvi mnamo mwaka 1947.

Ni jambo la kushangaza sana kwamba magombo hayo mawili yenye umri wa miaka elfu mbili yanazo kweli zile zile tunazozikuta katika Agano la Kale la Biblia zinazochapishwa siku hizi. Huu ni ushahidi wenye nguvu unaoonyesha jinsi Neno la Mungu linavyoaminika.

Mitume waliandika kwanza sehemu kubwa ya Agano Jipya kama nyaraka walizozituma kwa makanisa ya Kikristo yaliyoanzishwa baada ya kifo na ufufuo wake Kristo.

Zaidi ya maandiko ya mkono 4,500 ya Agano Jipya lote au sehemu yake yanapatikana katika nyumba za Makumbusho na maktaba za Ulaya na Amerika. Baadhi yake yanakwenda nyuma hadi karne ile ya pili.

Kuyalinganisha maandiko hayo ya mkono ya awali na biblia ya siku hizi, twaweza kuona kwa urahisi kwamba kwa kawaida Agano Jipya limeendelea pia kubaki bila mabadiliko yo yote tangu lilipoandikwa kwa mara ya kwanza.

Siku hizi Biblia au sehemu zake zimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 2,060 na (dialects). Ni kitabu kinachouzwa sana ulimwengu: zaidi ya Biblia milioni 150 na sehemu za Biblia huuzwa kila mwaka.

Usahihi wa Biblia kihistoria ni wa kushangaza sana. Uvumbuzi mwingi wa elimu ya mambo ya kale (akiolojia) umethibitisha kwa namna ya kuvutia sana usahihi wa Biblia. Wanahistoria wamevigundua vibao vya udongo wa mfinyanzi pamoja na majengo ya kumbukumbu ya mawe ambayo yameonyesha majina, mahali, na matukio yaliyojulikana kuhusu siku za nyuma kutokana na Biblia tu.

Kwa mfano, kulingana na Mwanzo 11:31, Ibrahimu na familia yake “wakatoka wote katika Uru… waende katika nchi ya Kanaani.” Kwa kuwa ni Biblia peke yake iliyosema juu ya Uru, mabingwa fulani wa Biblia walisema kwamba mji kama huo ulikuwa haujapata kuwako kamwe.

Ndipo wachimbaji wa mambo ya kale wakagundua mnara wa hekalu katika nchi ya Iraki Kusini ukiwa na kwenye msingi wake iliyoandikwa katika maandishi ya kikabari yaliyokuwa na jina la Uru.

Ugunduzi wa baadaye ulionyesha kwamba Uru ulikuwa ni mji mkuu ambao ulikuwa unasitawi wenye ustaarabu wa hali ya juu uliokuwa umefikiwa.

Sura ya mji ule ilikuwa imesahaulika ni Biblia peke yake iliyolihifadhi jina lake – mpaka pale koleo ya mwanaakiolojia mmoja ilipouthibitisha ukweli wa kuwako kwake. Na huo Uru ni mmoja tu miongoni mwa mifano mingi ya akiolojia inavyothibitisha usahihi wa Biblia.

Kutimia kwa usahihi kabisa kwa utabiri wa Biblia hukuonyesha wewe kwamba unaweza kuitegemea Biblia. Maandiko hayo yana utabiri mwingi wa kushangaza sana wa matukio ya siku za usomi ambayo hivi sasa yanaendelea kutimia mbele ya macho yetu.

Chini ni picha za Kisiwa cha Pitcairn

images%20(2).jpg
1417196503.jpg
1172919436.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    12.7 KB · Views: 7

View attachment 2603771View attachment 2603773View attachment 2603775

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana.
 
Asante mtumishi kwa baraka ya neno la faraja. Kumbe pamoja na vurugu zilizojaa juu ya ardhi, sisi binadamu tunaweza kubadilika kwa kuyachunguza maandiko.
 
Back
Top Bottom