Kisa cha Ukweli cha Binti Mcharuko....

Chipolopolo

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,425
725
Nipo stand isiyo rasmi ya basi.Ni kijijini. Natoka Tanganyika kuelekea Tanzania.Punde anasogea binti mdogo, kati ya umri wa darasa la saba na kidato cha kwanza. Nikiwa kijijini, sikujali kukata ndevu. Zimekuwa.Binti ananisalimia: "Habari za leo kaka?" Nilishangaa kidogo. Kaka yake mimi?Niliwaza moyoni. Nilimjibu, nzuri. Punde basi linafika.Tunapanda.

Watu wamejaa pomoni katika kibarabara cha siti za gari. Ninapata siti nina kaa. Yule binti mdogo hana siti. Anapambana kupata upenyo japo wa kusimama. Basi linaendelea na safari. Kondakta anapita kukagua tikiti. Anawapanga watu wajibane ili aweze kupakia abiria wengine.Kondakta ni mrembo. Kama chotara flani hivi. Ni mkali. Hajali wanaume au wanawake. Yeye kazi ni kazi. Wanaume wengi eneo hili hawajazoea mambo haya ya amri toka kwa wanawake. Wanafoka kila akitoa amri.

Amefika kwa binti mdogo anaelekezwa kurudi nyuma. Anatii. Hata hivyo anakutana na kadhia.Amemkanyaga mzee mzima. Mzee anafoka. "Binti huna adabu eti?Kwanini umenikanyaga wewe mtoto?" Ni hapo kisa kilipoanzia. Binti akacharuka. "Kwanini unaniita mtoto?" Mzee anamjibu, "kwa umri wako hufai hata kuwa mwanangu. Wewe ni mjukuu." Binti aliponyokwa na maneno makali yasiyo na tafsida kabisa. "Ukubwa wako nini? Ukubwa huko huko kwa wanao.

Unaniita mtoto mimi? Kama mimi mtoto, tushuke tukifika. Uchukue chumba guest. Nikakuonyeshe kazi.Na ninakwambia utalia kama mtoto kwa kazi nitakayokuonyesha ndipo utakapojua mimi si mtoto!" Watu karibu wote kwenye basi walipigwa na butwaa.

Hawaamini wanachokisikia. Mzee wa busara. Alijisikia aibu kupindukia. Alisema maneno machache huku akiwa mwenye mawazo tele. "Huu ni mkosi." Alimua kushuka kituo kinachofuata, japo kuwa hata nusu ya safari alikuwa hajafika. Vituko vya binti mcharuko havikuishia hapo. Ila mimi ninaishia hapa kwa leo! Moral of the story: Kuwa mwangalifu unapoongea na usiowajua. Wanaweza kukuharibia siku yako hivi hivi--kama huyo binti at her pretty foolish age!
 
heheheh disign kama huyu mzee ndo ulikuwa wewe hivi maaana wote mlikosa siti kwenye basi.pole sana kwa mkasa
 
Tabia hizo ni function ya maeneo mliyokuwa!
Kuna maeneo ya nchi hii ambako kitu cha aina hiyo hakiwezi fanyika hadharani namna hiyo!
Abiria wote watamgeuka binti na anaweza kushushwa yeye kwenye gari!...!
Huko ni Pwani fulani bila shaka, bara kwetu ukinyanyua mdomo kumjibu mzee masuala ya hivo unajuta dakika!
 
Tabia hizo ni function ya maeneo mliyokuwa!
Kuna maeneo ya nchi hii ambako kitu cha aina hiyo hakiwezi fanyika hadharani namna hiyo!
Abiria wote watamgeuka binti na anaweza kushushwa yeye kwenye gari!...!
Huko ni Pwani fulani bila shaka, bara kwetu ukinyanyua mdomo kumjibu mzee masuala ya hivo unajuta dakika!

@Pakajimmy. Umenchekesha mkuu. Kisa kilichoendelea mbele, kinafanana na ushauri wako!haha
 
Hiki ndicho kizazi cha leo wengine wanakiita kizazi cha bongo fleva.watoto hawana tena adabu.tatizo wazaazi nao mambo yao si mazuri kwa watoto wanaowalea
 
Vizee vingine navyo vikome.......si ajabu aliwahi kukutana nacho kikagoma kupokea salamu eti 'kitazeeshwa' (lol hapo kinajiona kijana bado), alafu kwenye basi ndo kinamwita binti wa watu 'mtoto'!!! Lol

@ Kipipi: unawezakuwa sahihi. ila kwa ushahidi wa mazingira, nkama hawafahamiani! anaogopa kuzeeshwa au vp?hahaha
 
Back
Top Bottom