Kisa cha maiti ya Anna Fritz na vifo vya wanaume waliombaka

KIJAKAZI ANAPOCHOSHWA NA KAZI YA MAUAJI.


Renfield anajikuta matatani baada ya kutengeneza ushirika na Dracula, vampire mnyonya damu anayeishi bila ya ukomo.

Miaka hiyo ya zamani Renfield, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alijikuta katika mazingira ya kuhitaji msaada kwenye kufanikisha moja ya kazi muhimu sana. Haja yake ikamwangushia kwenye miguu ya Dracula ambaye anamsaidia kwa gharama moja.

Awe mshirika wake.

Msaidizi wake wa karibu.

Kazi yake ni kumlisha Dracula kwa kumletea watu wasio na hatia kwani damu zao ndizo zenye thamani. Anatengeneza mipango ya kumkutanisha Dracula na watu kadhaa, watu ambao mwisho wa siku wanaishia kunyonywa damu mpaka kufa.

Kama haitoshi, Renfield anamsaidia Dracula kupambana dhidi ya hunters, watu maalum wanaowinda vampires na kuwaangamiza. Watu hao walitega mtego murua wa kumnyaka Dracula na mtego ukafanikiwa lakini kabla hawajamwangamiza, Renfield anakomboa nchi.

Wawindaji hao wawanamwachia Renfield laana. Wanamwambia damu za watu wote watakaouawa na Dracula zitakuwa juu ya mikono yake.

Baada ya miaka kamingi ijayo, ambayo ndo’ miaka ya sasa, Renfield anachoka kushurutishwa. Anachoka kuwa kwenye mahusiano haya ambayo yanamfanya aishi kwa lengo moja tu duniani, kumhudumia Dracula.

Japo Draco alimpatia sehemu ya nguvu zake, moja anaishi milele na pili akila wadudu anapatwa na nguvu ya ajabu mwilini lakini bado anaona haitoshi kuwa mtumwa wa bwana huyo wa milele.

Renfield anajiunga na kikundi fulani cha kanisa ambacho huwa kinakutanisha watu wenye changamoto mbalimbali za kimahusiano, wanakutana hapo na kujadili maswahibu wanayoyapitia kisha wanapeana faraja na ushauri.

Akiwa hapo, anasikia story ya mwanamke mmoja anayesumbuliwa na mwanaume wake mwonevu, anaamua kumtafuta mwanaume huyo kwa lengo la kumwadabisha na kisha mwili wake aupeleke kwa Draco kunyonywa damu.

Anampata mwanaume huyo akiwa pamoja na wahuni wenzake. Wanaume hao wametoka kupiga tukio la wizi kwenye familia moja ya kimafia inayojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya, ‘Lobbo family’ inayoongozwa na mwanamama wa makamo, Bella Lobbo, na kijana wake mapepe, Teddy Lobbo.

Anapoanza kushughulika nao, anastaajabu anavamiwa na bwana mmoja, jitu la miraba minne ambalo ametumwa na familia ya Lobbo kuja kuwamaliza wezi wa mali zao.

Jitu hilo halichukui maelezo, linapambana na yeyote aliyemkuta hapa akiwamo na Renfield.

Renfield anapambana na anafanikiwa kummaliza.

Boss - Teddy Lobbo, alokuwa nje akimngojea muuaji wake, jitu la miraba minne limalize kazi, anastaajabu kichwa cha muuaji wake kinatupiwa nje. Upesi anawasha gari lake na kutimua mbio.

Njiani sehemu ya ukaguzi Teddy anakamatwa na askari, afisa Rebeka, kwa kukutwa na madawa kwenye gari lakini ajabu bwana huyo anaachiliwa na polisi muda mfupi tu akiambiwa hana kesi ya kujibu ingali mhusika mwenyewe alishakiri makosa yake.

Mkono mtupu haulambwi.

Afisa Rebeka anaapa kupambana na familia ya Lobbo hadi tone la mwisho mpaka walipie uhalifu wao, ikiwemo kumuua baba yake mzazi. Na katika haja yake hiyo ndo' anakutana na Renfield. Wote wanaungana kudai haki.

Lakini mbaya zaidi familia ya Lobbo nayo inakuja kukutana na Dracula, nao pia wanaungana kuwa kitu kimoja.

Sasa ni Rebeka na Renfield dhidi ya Dracula na familia ya Lobbo.

Mbaya zaidi Dracula anaiwezesha familia hii ya kihalifu kwa kuipa nguvu kama za ajabu.

Tafuta movie, tazama..
a351f8fd233ab3dee79dd519242470b8.jpg
69f4c657ce35161a581fc11be028f07c.jpg
 
Shusha mkuu
shusha uzi uishii huu,wapo wadau wengi wa hizi muvi.
hizi ndio muvi napenda kuishi nazo.
Umetisha mkuu. Na kuna movie inaitwa the messengers nayo inakisa cha kuogofya kwenye nyumba za nje ya mji
Mkuu Bora umerudi kitambo sana aisee movie kaliii sana hizi
Siangaliagi horror ila namna unavyosimulia nimetamani kuzitafuta zote
Mkuu umetisha sana
Bwana Steve naona umerejea vizuri,
Tuendelee na kisa kingine hapo juu.
 
Image ya kwanza juu kidogo ifanane na ya 'Jane Doe', mhusika maiti kwenye filamu ya kutisha iitwayo 'The Autopsy of Jane Doe (2016)'.

Weka mbali na watoto.
Najua huo msala aisee. Sio poa. Kuna El Cuerpo. Unaipata?
 
Nakumbuka 2003 -2006 ndio ilikuwa na trending ya horror movies
Dunia nzima kila movie inayotoka ilikuwa ya kutisha kama

Ghost Ship
SAW
White Noise
Hills have Eyes
Wrong Turn
Final Destination 2
Texas Chainsaw Massacre
 
KIMBUNGA KINAMTUPIA BAHARINI MAMA MJAMZITO ALIYEJIFICHA NDANI YA KONTENA.


Nico na Mia ni mtu na mkewe ambao wanaamua kutoroka nchi yao ya Spain kwaajili ya kutafuta mahali salama kwao na mtoto wao ambaye muda si mrefu atazaliwa.

Nchi yao pamoja na nchi zingine ulimwenguni zimepigwa na anguko kubwa la kiuchumi ambalo linapeleka ukata mkubwa; hamna chakula, hamna huduma za afya, maji na umeme ni taabu na hata huduma zingine nazo zimekuwa bahati nasibu ya kuku kudonoa funza ardhini.

Hivyo maisha ni magumu kupita kiasi.

Kila mtu anatamani hata kidogo alichokishika mwenziwe mkononi.

Nchi inageuka kichwa chini, miguu juu!

Hali hii inapelekea utawala uliopo madarakani, utawala wa kidikteta na wa kihuni, kuja na suluhisho la kutisha ili kuweka mambo katika mkondo wake.

Suluhisho la kumwaga damu.

Serikali inaazimia kupunguza idadi kubwa ya watu ili kukabiliana na uhaba wa rasilimali zilizopo, hivyo basi, wazee, watoto, walemavu na wanawake wajawazito wanauawa!

Halina simile, halina msalia mtume.

Nico na Mia washampoteza mtoto wao wa kwanza kwenye zoezi hili katili. Mia, ambaye ni mama, anaumia kila anapomkumbuka mwanae na bado hajaisamehe nafsi yake kwa kumpoteza mtoto wake mpendwa.

Kumpoteza tena huyu mwingine, hayuko tayari abadan!

Sasa mpango ni upi?

Nico anasuka mkakati wa kutorokea nchi ya Ireland kwa kutumia meli ya mizigo. Nchi ya Ireland ni moja ya nchi chache zilizoweza kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi na bado serikali yake ya kidemokrasia iko imara. Wanaamini huko ni paradiso na wakifika tu basi shida zao zitakuwa zimekoma.

Lakini hawako peke yao.

Watu wengi wanapanga kutoroka nchi hii isiyokalika kutafuta malisho upande mwingine wa dunia lakini zoezi hili limejawa na milima mikubwa na mabonde makali. Wanajeshi wametapakaa karibia kila kona, na punde watakapokubaini basi uhai wako ni mali yao.

Wanaranda huku na kule wakiwa wamebebelea bunduki zilizotumwa damu tu.

Nico na mkewe, kwa kutumia njia za panya, wanafanikiwa kupata nafasi kwenye moja ya kontena ambalo linasafirishwa kuelekea bandarini . Wanalipia pesa yote waliyotunza lakini bado haitoshi, inabidi waongezee pete yao ya ndoa ili waweza kupata nafasi hiyo adimu.

Wanaswekwa kwenye kontena ambalo ndani yake ni kiza na wamejaa watu wengine ambao nao wanatoroka.

Mara kidogo gari lililokuwa limewabeba linasimama. Wale maharamia walokuwa wamewapakiza humo ndani wanawaamrisha watu wapungue ndani ya kontena hiyo wahamie kwenye kontena nyingine. Miongoni mwa watu wanaohamishwa, bwana Nico naye yumo.

Anajaribu kusema kuwa yuko na mkewe, lakini hamna anayejali, anapigwa kitako cha bunduki na kutupiwa nje ya kontena kama kifurushi cha pumba. Kontena linafungwa huku mkewe, Mia, akiwa haamini kama tayari ndo’ ashatenganishwa na mumewe.

Anatazama na kumwona mumewe anaingia kwenye kontena la kijani lililoandikwa kwa maandishi makubwa meupe – 107.

Analia kwa uchungu.

Anapiga simu, Nico anamtia moyo watakuwa pamoja mbele ya safari na anamshauri asitumie simu ili kutunza charge kwani safari ni ndefu.

Baadae Mia akiwa ndani ya kontena, kwa kupitia tundu dogo, anapata kutazama yale yanayoendelea huko nje walipokuwa wakikatiza.

Mambo ni balaa.

Hali si hali.

Yani unajiona ni mwenye bahati kuwemo ndani ya kontena lenye giza ingali wenzako wapo mitaani.

Muda si mrefu, gari linasimama tena. Mara hii wamefika sehemu ya ukaguzi ambapo kuna wanajeshi wanaokagua mizigo kabla ya kupewa ruhusa ya kuvuka kwenda bandarini.

Mkuu wa kitengo anapewa nyaraka za mzigo. Anapitisha macho kukagua lakini anahisi kuna jambo la zaidi kwenye kontena. Watu wote wametulia tuli. Hata pumzi unahema kwa chini ili msije mkasikika huko nje.

Bwana mkaguzi anaingia ndani ya kontena.

Anatazama … Haoni mtu hata mmoja!

Kontena liko kimya kama kisima cha porini.

Lakini kuna kitu hakipo sawa hapa, naye anagundua hilo.

Ukubwa wa kontena kwa huko nje, si sawa na ukubwa wake kwa humu ndani. Hili kontena lina partition. Na huo upande wa pili kuna watu. Humo wamejibana. Wameziba midomo yao. Mioyo inaenda mbio. Maisha yako rehani mbele ya midomo ya risasi.

Bwana mkaguzi anaamuru risasi zimwagike kuua kila mtu aliye ndani ya kontena, na kweli inashushwa mvua ya vyuma.

Si kwa watoto wala watu wazima.

Hamna anayesalia hai isipokuwa Mia peke yake.

Yeye alijificha juu ya maboksi yaliyomo ndani ya kontena. Wakati wengine wanapiga makelele ya kukutana uso kwa uso na kifo, yeye anajibana akitulia kadiri anavyoweza.

Anatetemeka kwa hofu kubwa.

Wanajeshi wanamaliza kazi yao na miili inatolewa kisha safari ya kontena inaendelea. Kontena lile lililokuwa na watu rundo, sasa limebakiwa na mtu mmoja pekee na harufu ya damu.

Mia anajaribu kumpigia simu mumewe aliye kwenye kontena jingine ili amwambie ajifiche kwani kuna kuuawa eneo la ukaguzi lakini zoezi lake halifanikiwi.

Anahofia mumewe anaweza kuuliwa.

Analia kwa kwikwi.

Kontena linafika bandarini na linapachikwa kwenye meli kubwa kwaajili ya kuanza safari ya bahari. Safari ya kukata mawimbi kuitafuta ardhi salama huko ng’ambo.

Safari ya matumaini.

Kuacha ardhi hii ya Spain ni ushindi mkubwa kwa Mia na mwanaye aliye tumboni, lakini kabla hajafika kwenye nchi ya ahadi analetewa mtihani mwingine mezani.

Baada ya chombo kusonga ndani ya bahari, mwendo na mwendo, inatokea dhoruba kali kama ile ya hadithi ya mua ulozamisha meli.

Bahari inachafuka na mawimbi makubwa yanachapa chombo bila huruma. Meli inayumba kwenda huku na kule. Mia anapiga kelele kuomba msaada kwamba niko humu ndani, niko humu ndani nifungulieni!

Anasukumwa huku na kule ndani ya kontena.

Bahati yake mtu anamsikia na anataka kumsaidia lakini kabla hakijafanyika chochote, wimbi linapiga ubavu wa meli. Meli inalala upande na kumwagia makontena kadhaa baharini - PAKACHAA!

Moja ya kontena linalotumbukia ni lile la Mia.

Mama mjamzito.

Anajibamiza kwenye kuta ya kontena na kupoteza fahamu.

Anapokuja kuzinduka, anachungulia nje kupitia tundu na haamini kile anachokiona.

Yupo katikati ya bahari!

Ni maji marefu ndo’ yamemzunguka.

Safari yake ya kwenda Ireland imeishia hapa kwenye maji chumvi.

Taratibu maji yanaingia ndani ya kontena kupitia matundu ya risasi.

Je, mara hii atakiepuka kifo ingali hakuna wa kumsaidia na yuko mwenyewe katikati ya NOWHERE?

Tena usisahau, mimba yenyewe alobeba imebakiza masiku tu.

Tafuta leso ya machozi, cheki movie ...
fd71c28e757a3c29d9af5f7eca3b9aec.jpg
 
weka vitu meneja,kuna mauwa yenu spesho mtakutana nayo
Namimi kaka kama hutojal
me pia mkuu
Bwana Steve naona umerejea vizuri,
Siangaliagi horror ila namna unavyosimulia nimetamani kuzitafuta zote
Mkuu umetisha sana
Naomba unitumie pm mkuu
shusha uzi uishii huu,wapo wadau wengi wa hizi muvi.
Shusha mkuu
Tuendelee na kisa kingine hapo juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom