Serikali iondoe ushuru wa kutoa maiti hospitalini

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,283
2,043
Wadau nawasabahi.

Juzi nimesikia kwenye Vyombo vya habari kuwa kuna familia imeshindwa kuchukua Mwili wa mpendwa wao baada ya kufariki.

Sababu za kushindwa ni ukosefu wa Fedha za kuikomboa hiyo Maiti Hospitalini kuwa kubwa.Baada ya kuhojiwa kwa Uchungu mkubwa walisema ndugu yao kafariki kwa kukosa Fedha za Matibabu ikiwa pamoja na kufanyiwa Upasuaji.

Wakaendelea kuhoji Kama Kuokoa Uhai wa ndugu yao Wameshindwa ambao ulikuwa ni muhimu sana iweje wawe na Pesa za kuchukua Maiti Hospitali?

Kwa uchungu mkubwa Wakaiomba Serikali iiondoe Kodi hii ya Maiti kwa Misingi kuwa Fedha nyingi zinatumika Kumuuguza Mgonjwa hivyo Maiti zitolewe Bila Ushuru wowote.

Ombi kwa Serikali iliangalie Suala la Maiti kutolewa kwa Fedha japo ni Mapato ya Serikali lakini linakuwa gumu kwa Wafiwa kwani wanakuwa Wanetumia Fedha nyingi katika kumtibu Mgonjwa wao.
 
Back
Top Bottom