Kisa cha Kafulila kuvuliwa uongozi hiki hapa

Umri wa umaarufu wa kisiasa wa Mh Kafulila ni mdogo kuliko umri wa NCCR Mageuzi...........muktadha hapani kwamba Mh alipohamia NCCR yamkini alitambua hilo kwamba mwenyekiti anayekwenda kujiunga naye ni kibaraka wa CCM kwamaneno mengine alijuya kabisa anakwenda kujiunga na CCM C.........cha kutuaminisha hapa ni kwamba huenda hakuona kimbilio lingine zaidi ya NCCR, vinginevyo ni mazungumzo baada ya habari.......hata hivyo naona ana msomamo thabiti na Mwenyezi Mungu amjalie autetee........
 
Mbatia ameshindwa kabisa kujua kwanini wabunge wote wa NCCR wanatokea Mkoa wa Kigoma?
Kweli sikio la kufa!
 
“Mbatia hata yeye ubunge anajua una hadhi kuliko hata uenyekiti wake, ndiyo maana aliomba kura Jimbo la Kawe lakini akashindwa. Ila anajua hali ni ngumu na anaweza kuangushwa kwenye NEC ijayo, hivyo anadhani mchawi wake ni mimi na Mkosamali,” alisema Kafulila.

sidhani kama kafulila yuko sahihi, what if mwkt akiamua kumvua uanachama je ubunge wake anaojivunia utakuwepo?
 
Kafulila ni mtu wa tamaa sanasasa ngoja tuone hatma yao maana wamezidi kutoboana macho wenyewe kwa wenyewe
 
kwasasa kuna chama kimoja tu cha upinzani,wengine wote fake...halima mdee alishasema tena kuwa mwenyekiti wa nccr ni kibaraka wa ccm..so kafulila karudia tu
 
Hata kama ni kweli Mbatia ana makosa pia Kafulila lazima atakuwa na matatizo kwa nini kila aliko chokochoko zinaanzishwa na yeye? Au ndiye Mrema mpya wa zama hizi?
 
Kafulila na mkosamali wakirudi chadema nani ataomba msamaha? slaa kwao au wao kwa slaa? strictly kwa wenye jibu tu.
Slaa ndiyo ataomba msamaha kwani alipokwenda kule jimboni kwa Kafulila alikiona cha moto wakati anamnadi mgombea wake wa ubunge
 
Slaa ndiyo ataomba msamaha kwani alipokwenda kule jimboni kwa Kafulila alikiona cha moto wakati anamnadi mgombea wake wa ubunge
Kwahiyo hiyo ndio sababu ya DR SLAA kuwaomba msamaha kina Kafulila na Mkosamali?Mi PU.M.B.A.V.U mingine bana!
 

Wakati hali ikiwa tete katika Chama cha CUF, mzozo mwingine mkubwa ambao umeibuka ndani ya Chama cha NCCR- Mageuzi umefikia hatua mbaya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Samuel Ruhuza, kumvua madaraka ya Ukatibu Mwenezi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.


Akizungumza na gazeti hili jana jioni kwa njia ya simu, Kafulila alikiri kupokea barua ya kuvuliwa wadhifa huo kutoka kwa Ruhuza, akisema ameambiwa kuwa hayo ni mamlaka ambayo anaweze kupewa na kuondolewa.

“Ni kweli nimepokea barua lakini mimi sijaona tatizo lolote kwani sikuomba nafasi hiyo bali niliomba ubunge. Ujue hadhi ya ubunge ni kubwa kuliko katibu mwenezi, hivyo nimejulikana na kuheshimika kwa wadhifa wa ubunge,” alisema.
Alifafanua kuwa ana uhakika shinikizo la kuondolewa kwake limetoka kwa Mbatia, kwani ameonesha wazi kuwa hamtaki yeye pamoja na Mbunge wa Mhambwe, Felix Mkosamali, kutokana na kutofautia naye.

“Mbatia hata yeye ubunge anajua una hadhi kuliko hata uenyekiti wake, ndiyo maana aliomba kura Jimbo la Kawe lakini akashindwa. Ila anajua hali ni ngumu na anaweza kuangushwa kwenye NEC ijayo, hivyo anadhani mchawi wake ni mimi na Mkosamali,” alisema Kafulila.

Alisema Mbatia hana jambo la kukwepa kuhusu kutumiwa na CCM bali anachotakiwa kufanya ni kuhamia huko ili akafanye kazi vizuri na kuiacha NCCR mikononi mwa watu wenye malengo ya mageuzi.
“Juzi nilihojiwa kuhusu wapinzani kukutana na Rais Jakaya Kikwete, nikatoa msimamo wangu kuwa sina imani na serikali ya CCM na nikasema NCCR-Mageuzi hatutakwenda Ikulu kuonana naye kwani hatuwezi kupangiwa ajenda na CCM. CHADEMA walikaa kwenye vikao wakaibuka na ajenda yao,” alisema.
Mwanasiasa huyo aliongeza kuwa baada ya kutoa msimamo huo, Katibu Mkuu wao, Ruhuza, alimpigia simu na kumlalamikia kuwa aliisema vibaya CCM na kuwahi kutoa msimamo wa kutokwenda Ikulu, hatua aliyoiona kuwa viongozi hao wana ajenda ya siri.

Kafulila ni miongoni mwa wanachama na viongozi wengi wa chama hicho wanaomshinikiza Mwenyekiti wao, James Mbatia, ajiuzulu nafasi hiyo kwa madai kuwa amekuwa akifanya kazi kama kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuvihujumu vyama vya upinzani, kikiwamo NCCR-Mageuzi.

Halmashauri Kuu ya chama hicho iliyoketi Novemba 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea malalamiko ya wajumbe hao ilimpa Mbatia siku 21 za kutoa utetezi wake kwa maandishi ili mkutano ujao Februari 3, mwakani uweze kutoa uamuzi ama wa kumuengua au la.

Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Mbatia anataka kuwafukuza wajumbe wote wa NEC aliowateua halafu wanampinga ili kuweka mazingira mazuri ya kutoenguliwa katika mkutano wa Februari.
Lakini kuhusu hilo, Kafulila alisema kuwa anajidanganya kwa mpango huo, kwani licha ya kumuondoa kwenye ukatibu mwenezi bado anabakia kuwa mjumbe wa NEC kwa wadhifa wake kama mwenyekiti wa wabunge wa chama hicho.

Source: Tanzania Daima



Kazi ipo!!



Jana nilisema hapa.Hivi vyama vyenu vyote vinavyolilia demokrasia kiukweli ndio vimekeua vya kwanza kuminya na kubaka demokrasia ndani ya vyama hasa katika chaguzi za ndani,ni jambo la kawaida sasa kwa wenyeviti wa vyama mbadala vya Tanzania kuiona nafasi ya uenyekiti kama ni taasisi yao binafsi,anapotokea mtu kutaka kuwapa challenge kwenye nafasi hiyo unapoitishwa uchaguzi kwa mujibu wa katiba za vyama hivyo wenyeviti wetu hawa hununa na kufanya hila za kuwazuia,hawapendi kuwa tested,wao wangependelea zaidi kuwa wenyeviti wa maisha;sizungumzi kwa majungu ipo mifano hai ambayo ndio hata imechangia wetu wengine kama mimi kutokua na vyama na kuamua kutofungamana na upande wowote kutokana na kutotaka kujiweka karibu na demokrasia za kinafiki,mifano ni kama ifuatayo:

Kila mtu aliona mutungirehi alivyonyanyasa na kugombana na mrema alipotangaza kugombea nafasi ya "mzee" kwenye uchaguzi mkuu wa tlp,mwanzoni walikua marafiki na mrema kumchulkulia kama kijana wake lkn aliposema mzee na mimi nataka nikupime ubavu akaonekana hana adabu!

Tukaja kuona jinsi profesa safari alivyodhalilishwa na cuf kisa kutaka kumpima ubavu Lipumba!wakasema eti kwa kutaka kuyumia haki yake ya kupigiwa kura ama kuchaguliwa ndani ya chama chake na wanachama wenzake eti ametumwa na adui(ccm)!!!!!!!

Pia kila mtu hapa anakumbukumbu ya kilichompata marehemu chacha wangwe pale alipojaribu kumpima ubavu "bwana mkubwa" wa chadema,kwanza alianza kwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti,mwenyekiti mboe akafanya kila analolijua kumzuia asigombee akashindwa,then akatumia kila mbinu chafu na safi ili jamaa asipate kura za kutosha pia ikashindikana marehemu chacha akaibuka kidedea bwana mkubwa akanuna sana,hakuipenda demokrasia iliyotumika kumuweka madarakani rasta,alitaka aweke mtu wake wanachama wakamwambia no mzee kura yako ni moja tu ndio unatakiwa uitumie hiyo kumzuia kwenye sanduku la kura!kura yake haikutosha kumzuia chacha bahati mbaya!chacha wangwe hakuishia hapo akamwambia mwenyekiti sasa naitaka nafasi yako!mwnyekiti akaona hii sasa balala,akaanza mikakati ya kumzuia,this time akafanikiwa!kweli chacha wangwe hakugombea uenyekiti wa chadema na hatakuja kugombea milele nafasi hiyo!

Ikawadia zamu ya zitto kumpima ubavu mwenye kigoda,kilichotokea wengi tunajua,kwani wengi humu kipindi hiki mlikua mmeshaingia chadema...rejea nini kilitokea!Halafu upime na hii ya mbatia,swahiba wangu mpenzi sam ruhuza na bwana kafulila.Kina kafulila inavyoonekana hapo wanataka kuleta mabadiliko na kukifufua chama kwa kuja na mawazo mapya,sam na mbatia inaonekana hawataki hilo litokee na mbaya zaidi inaonekana wako tayari kuibaka demokrasia isichukue mkondo wake kwa kuwafukuza kabla ya uchaguzi.

Rai yangu kwa wenyeviti wa vyama mbadala hapa wanacho angalau japo kidogo cha kujifunza kutoka magamba,japo nao wana kamchezo eti ka kumuachia mwenyekiti amalize muda wake! upuuzi mtupu,hakuna demokrasia ya namna hiyo,wenyeviti wakubali kuwa tested kwenye chaguzi za ndani.Nawasilisha.
 
Aseme tu samahani Chadema, then atapokelewa aongeze nguvu kwa makamanda! Lakini kama Mbatia ni kibaraka atakuwa anafanya usaliti sana kwa Taifa hili.
mkuu bado unajiuliza kama mbatia ni msaliti na kibaraka wa ccm?naweza kuwa na mashaka kidogo kuhusu ukibaraka wa zitto kwa ccm kuliko huyu mlaini mbatia...people will spill on mbatia's grave..
 
kafulila ni sawa na lusifa, anapenda sana madaraka, hata kwa magamba watamfukuza
right to the point mkuu.
ndo maana anasisitiza kwamba UBUNGE una HADHI kuliko UENYEKITI wa Mbatia.

lakini hajifunzi huyu. kupambana na Mbatia ni sawa na kupambana na Mrema,.......hawa ni viongozi wa vyama vyenye malengo maalumu.
 
"Mbatia hata yeye ubunge anajua una hadhi kuliko hata uenyekiti wake, ndiyo maana aliomba kura Jimbo la Kawe lakini akashindwa. Ila anajua hali ni ngumu na anaweza kuangushwa kwenye NEC ijayo, hivyo anadhani mchawi wake ni mimi na Mkosamali," alisema Kafulila.

sidhani kama kafulila yuko sahihi, what if mwkt akiamua kumvua uanachama je ubunge wake anaojivunia utakuwepo?

nani kakwambia mwenyekiti wa chama anaweza kuamka asubuhi na kumfukuza mwanachama?ingekuwa hivyo mbowe angekuwa kashalitimua lishibuda!au jk angeshamtimua lowassa kwa kumuita fisadi wa richmond!
 
Slaa ndiyo ataomba msamaha kwani alipokwenda kule jimboni kwa Kafulila alikiona cha moto wakati anamnadi mgombea wake wa ubunge
dah!!
kuna ongezeko kubwa sana la watu wanaofikiria kwa kutumia wowowo.
 
Back
Top Bottom