Kipya kinyemi..

SI unit

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,953
766
Ktk harakati za maisha ya mjini, wengi wetu tunaanzia (pengine kuishia) maisha ya kupanga. Na ktk lyf stail hii, kuhama mtaa mmoja kwenda mwingine ni jambo la kawaida(coz wenye haus wengne ni wakorofi). Juzi kati kuna dada mrembo kahamia mtaani kwetu, urembo wake umekua tishio kwa vijana wa rika tofauti kuanza kumshobokea na kumtaka kimapenzi. Kiukweli anajipenda na anavutia, anajua kujiremba, anajua kutega walio rijali. Kwa bahati njema imetokea kuzoeana nae na hata kupiga story(za kawaida), coz anapenda kuwa up to date. Jana akaja rafiki yangu kunitembelea, baada ya ziara nikampa kampani jamaa yangu kwenda kituoni apande gari kurudi kwao! Ghafla mbele yetu anatokeza yule mrembo. Alahaula! Tabasam na konfidensi ikampotea tofauti na nilivyomzoea. Tulivyopishana hakunisalimia kwa bashasha kama nilivyozoea. Who cares, nikaipotezea. Mbele ya safari jamaa yangu akaniuliza, unamfaham yule dada? Nikamjibu bila shaka. Akanitupia swali jingine, anakuja mara kwa mara huku mtaani kwenu? Nikamjibu, si mtembezi bali ni mkazi! (kukawa na kimya kifupi like a commercial break). Then jamaa akaniambia yule dem ni "kicheche" ile mbaya afadhali wa kona bar/ambiance inajulikana wanajiuza. Kwa taarifa alizonipa ni kwamba CV ikishachafuka mtaa flan, fasta anafunga virago na kuhamia mtaa wa mbali na anaingia na swaga za "kilokole" flan siku za mwanzo. Dah! Nilichoka ghafla, lakini jamaa aliniambia ameprove hilo jambo na ana uhakika. Nikaanza ku"recall" alivopoteza cofidens wakat tunapishana coz labda alijua mtama ushamwagwa kwenye kuku wengi.
Kwa mtindo huu wengi si tutauziwa mbuzi kwenye gunia?

Watch out wanaJF ambao bado mna***! Hata mtaani kwenu VIPYA VINYEMI VIPO.

SI unit, nawasilisha!
 
ulishakula mzigo nn??
mbona naona kama umeshtuka sana kupata habari kamili za huyo mrembo
maana inaonekana ulibahatika mtaa mzima,kama kwel ni bahati au mautundu yako...ukazoeleka nahisi zaidi ya wengine...
kama ulitafuna,kapime
tehe..
 
ulishakula mzigo nn??
mbona naona kama umeshtuka sana kupata habari kamili za huyo mrembo
maana inaonekana ulibahatika mtaa mzima,kama kwel ni bahati au mautundu yako...ukazoeleka nahisi zaidi ya wengine...
kama ulitafuna,kapime
tehe..

Mkuu ni mazoea tu! Sikutaka kuingia kwenye vita baridi na vijana..
 
Kawaambia alikuwa rafiki wa kawaida mbona mwamlazimishia R.I.P mtoto wa mwenzenu?
 
Back
Top Bottom