Kipindi cha Mpito kuelekea hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

...sherehe za Muungano zitafanyika kesho zanzibar,lakini cha ajabu hakutakuwa na hotuba kutoka kwa rais wa Mungano zaidi ya kupigiwa mizinga,kukagua gwalide,gwalide kupita kwa mwendo wa halaka na polepole mbele ya Rais wa muungano na kuangalia vikundi mbalimbali vya ngoma.waheshimiwa watakuwa wanatambulishwa kulingana na wanavyoingia.sijajua kama kutakuwa na sherehe fupi ya Muungano jioni pale ikulu.
Wangetumia nafasi hii kuzungumzia katiba,ufisadi na muungano.lakini hamna kitu kama hicho.
 
naambiwa zanzibar walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya kusikiza hotuba ya kikwete, lakini habari za uhakika ni kwamba hakutakuwa na kitu kinachoitwa hotuba wala kitu cha kufanana nacho. ni magwaride kwa kwenda mbele, kupoteza muda. basi!
 
Tumechoshwa na Muungano

Posted on April 25, 2011 by zanzibaryetu

http://zanzibaryetu.files.wordpress.com/2011/04/samia.jpg
Waziri wa anayeshungulikia masuala ya Muungano, Bi Samia Suluhu Hassan amekuwa katika wakati mgumu hasa katika kipindi hiki ambapo wazanzibari wamechachamaa kutaka ama heshima katika Muungano kama nchi mbili zilizoungana Zanzibar na Tanganyika au Muungano huo uvunjike
Inasikitisha kuwa Jamhuri ya Muungano imekuwa ikifanya mbinu na njama za makusudi kupopotoa mamlaka yaZanzibarilhali jeuri kubwa ikifanywa kwa kutumia nguvu za kisiasa na hila za kisheria na wakati huo huo wananchi kuwekwa kizani.

بسم الله الرحمن الرحيم
UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMUZANZIBAR
TAMKO LA JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBARJUU YA HALI YA MUUNGANO WA TANZANIAKATIKA
MAADHIMISHO YA SIKU YA MUUNGANO WA
TANGANYIKA NAZANZIBAR APRIL 26, 2011 LEO TAREHE 25/4/2011
Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Sala na salamu zimshukie kiongozi wa umma huu kiislamu Bwana Mtume Muhammad (S.A W) pamoja na masahaba zake na wote walio katika njia ya haki.

Ndugu Waislamu na Wazanzibari

Sisi viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Zanzibar tukiwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu tumeamua leo kutoa tamko juu ya suala la Muungano ambao leo hii unafikia miaka 47 tokea kuasisiwa kwake.

Kila mmoja kati yetu anajua fika juu ya hali ya Muungano huo na umri wake wote na jinsi ambavyo umekuwa na mashakila makubwa tokea kuanzishwa kwake.

Pia kila mmoja wetu anajua juu ya ukweli kuwa Muungano huu umekosa kukubalika na Wazanzibari toka siku yake ya kwanza hadi leo hii.
Ushahidi wa hilo ni kuundwa kwa tume kadhaa (tume ya Nyalali, Kisanga, Shelukindo, Salmini,Amina na n.k) za uchunguzi na kutafuta maoni ambapo siku zote Wazanzibari hawakuficha hisia zao.

Si madhumuni yetu kuhoji uhalali wa Muungano kisiasa, wala si madhumuni yetu kuhoji uhalali wa Muungano kisheria, lakini ni hakika kabisa kuwa Muungano huu wa Zanzibar na Tanganyika umekuwa na utata mkubwa kiasi ambacho umekuwa na tabia ya kuwachanganya wanasiasa na wanasheria na kwa hivyo wananchi siku zote wamekuwa katika giza.
Mbali ya ukweli huo, lakini pia imekuwa ni jambo la wazi kuwa Muungano huu unakiuka misingi yake ya awali ya kuwa na pande mbili za Muungano badala yake kila dalili zinaonyesha kuwa mamlaka ya Zanzibar yanapunguzwa na kutiwa katika mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa maneno mengine ni kusema kuwa nguvu za Zanzibar kama mshirika mmoja kamili katika Muungano huo hazipo kama zilivyokuwa April 26, 1964 kwa kuongezwa Mambo ya Muungano lakini pia hata mambo yasiokuwa ya Muungano yamekuwa yakiilemea Zanzibar.

Inasikitisha kuwa Jamhuri ya Muungano imekuwa ikifanya mbinu na njama za makusudi kupopotoa mamlaka ya Zanzibar ilhali jeuri kubwa ikifanywa kwa kutumia nguvu za kisiasa na hila za kisheria na wakati huo huo wananchi kuwekwa kizani.

Kwa karibu miaka yote 47 Muungano huu umekuwa ni miliki ya chama kimoja cha kisiasa cha CCM, ukitoa miaka michache kuanzia 1964-1977. Lakini hata wakati huo Katiba ya Muda na ile iliyofuatia ilisema wazi kuwa TANu ndio chama pekee cha kisiasa Tanzania ilhali ilikuwa ikieleweka kuwa Tanzania kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar basi kulikua na ASP ka upande wa Zanzibar.

Mambo ya msingi yamevunjwa kama vile kutoitishwa maoni ya wananchi mwanzo mwanzo kabisa katika Muungano huu lakini hilo pia halikufanywa hadi hivi leo na kwa hivyo Muungano huu haukidhi vigezo vya kisheria na kukosa Baraka za wananchi.

Hali kadhalika Muungano huu umekuwa hauna usawa basi angalau kungekuwa na uwiano, lakini hali hiyo haiko katika maeneo yote iwe ni kiuchumi, kielimu, kisiasa na hata kwenye kiutawala.

Na kwa sababu hiyo maamuzi ya Muungano huu kwa muda wake wote yamekuwa yakitoka kwa upande mmoja tu ambao ni wa Tanganyika uliovaa koti la Muungano na kwa hali hiyo Zanzibar kudhulumika katika utaratibu huo.

Kwa muda mwingi wa Muungano kumekosekana utaratibu wa wazi na wenye taaathira wa kutoa maoni na kwa hivyo sauti nyingi zilizokuwa zikitoelwa kuukosoa, kuulalamikia na hata kuukataa Muungano zimekuwa zikipotea kama moshi unaoingia katika mawingu.

Wakati hivi sasa tukikumbuka miaka 47 ya Muungano ni sadfa pia kumetokea fursa ya wananchi kutoa maoni yao jambo ambalo ni la nadra kuhusiana na Katiba ya Tanzania. Lakini sote tunajua dharau ambayo imefanyiwa Serikali ya Zanzibar na wananchi wake wakati Muswada wa kutoa maoni ya Katiba ulipoletwa kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu.
Tunaamini matukio yaliotokana na mijadla ya siku mbili ya Muswada huo bado yamo vichwani mwa wengi wetu na kwa hivyo iwe ni ushahidi kuwa Serikali ya Muungano haiko kabisa kwa maslahi ya Zanzibar kadri inavyoweza kuyakwepa.

Kwa hivyo sisi viongozi wa Kiislamu tukiwa na jukumu la kuhimiza waumini kudai haki zao na tukiwa na jukumu la kuwahamasisha raia tunatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kutodharau kabisa fursa ya kujitokeza kwa wingi wakati Muswada wa kuunda tume ya kuratibu maoni utakapokuja.

Ila wito wetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa mjadala wa muswada huo uwe mpana kuliko tulivyoona hali ilivyokuwa mwanzoni mwa mwezi huu na kwamba Muswada huo ukija tena uje na marekebisho yanayotokana na maoni ya wananchi yaliokwisha kutolewa na sio Serikali ya Muungano wa Tanzania kufanya kiburi cha kuidharu Serikali ya Zanzibar na kutenda itakavyo.

Kuhusiana na suala zima la Muungano sisi viongozi wa Kiislamu wa Zanzibar tunasimama katika mambo yafuatayo na tunawaomba Waislamu na wananchi wote wa Zanzibar waungane pamoja na kujenga hoja na sauti moja kwamba:

1. Mjadala wowote wa Muungano utanguliwe na Kura ya Maoni kwanza kuulizwa wananchi wa Zanzibar peke yao na wananchi wa Tanzania Bara peke yao iwapo wanautaka Muungano au hawautaki na kama wanautaka ni wa aina gani.

2. Kwamba njia bora kabisa ya kuanza mjadala wa washirika wa Muungano ni kurudishwa Serikali ya Tanganyika kwanza ili Zanzibar ipate mshirika wa kujadliana nae.

3. Mjadala wowote ule wa Muungano ni lazima uanzie kwenye makubaliano ya awali ya Muungano na si vyenginevyo.

4. Kwamba mjadala wowote wa Muungano ule urudishe nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano na sio ilivyo hivi sasa ambapo Rais wa Zanzibar hana nafasi ya maana wala amri yoyote ile katika Muungano.

5. Kwamba suala la Muungano lisijadiliwe kama kwamba ni la kisiasa lakini badala yake litizamwe kama ni suala la kinchi.

Mola wetu Mtukufu tunakuomba uibarikiZanzibar na watu wake na uwalinde dhidi ya maadui wa ndani na nje. AMIN

……………………………………
Sh Thabit Mohd Saleh
AMIR- UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMUZANZIBAR
 
Kwa mtazamo wangu sioni umuhimu wa kuwa na sherehe ya muungano-
maana naona muungano wenyewe una walakini sana-ni bora viongoz wangekaa na kusolve matatizo ya muungano ikibidi waufunje

inatakiwa sherehe za muungano viongozi watupe progress za mambo tunayoshirikiana na kama yameleta faida au la
lakini kama itakuwa ni swala la kuangalia halaiki na gwaride ni bora hizi sherehe zisiwepo na muungano wenyewe pia usiwepo
ngoja tuone hio kesho watakuwa na kitu gani kipya zaidi ya halaiki na ngwaride

Umenena mkuu.
Huu Muungano haujafanyiwa review tokea umeanzishwa.
Kama umefanyiwa basi itakuwa kama zinavyokuwa ripoti zote za tume na kamati nyengine,zinaishia kwenye meza ya rais na inasubiriwa kelele, malalamiko mengine na inaundwa tume au kamati nyengine...ubadhirifu na uharibifu tu wa fedha za walipa kodi, fedha za umma.

Kesho hakuna kipya zaidi ya kusema Muungano umekuwa wa kupigiwa mfano hapa duniani...bla.bla..bla...Muungano umeimarika....Tutalinda mapinduzi!....the same old song!

Wenyewe wanaelewa kwa jinsi ambavyo wameuendesha Muungano huu na uchakachuaji ambao wameufanya katika mkataba wa muungano na katiba kuwa hakuna muungano bali ni sinema tu, maigizo!
 
Ni kweli kabisa yani sisi ni watu wa ajabu sana, Tuna lala mika kuhusu East Africa Federadiont huku hatuoni malalamiko ya Zanzibar kuhusu muungano wa Tanzania
 
Miaka yote sherehe za Muungano wanatupiga dry,sijui kwa nini,ila najua JK anaogopa sana Muungano kufia kwake kama Mikael G.anasukuma gurudumu lije linmfie mwingine,labda atakuja kuwa Hussein Mwinyi wanaemuandaa mfupa alioushindwa baba yake yeye atauweza?
 
Na mara nyingi ndo kitu ambacho viongozi huwa wanafanya,hata kweny sherehe kama uhuru,ingekuwa busara wangekuwa wanatoa hotuba ili kuwapatia wananchi baadhi ya majibu ya manunguniko yaliyopo kwa uwazi.GWARIDE LITASAIDIAJE KUWAPUNGUZIA WANANCHI MATATIZO YA MUUNGANO?kwa dk 30 zake?

Ieleweke kuwa watu wengi hawakuwepo enzi muungano unaasisiwa, wangeweza kuelimishwa kuhusu maana na dhima ya muungano,ulikotoka,ulipo na tufanyeje ili tuuendeleze kuwaenzi wazee wetu waasisi!

Na ni wazi gharama za walipa kodi hutumika kuanzia maandalizi na posho na gharama zingine kibao,JE GWARIDE TU NDIYO DHIMA YA VIONGOZI KUCHOMA MAFUTA YA NDEGE ZETU HADI ZBAR KUKAGUA GWARIDE NA KUANGALIA HALAIKI YA WATOTO TU?

Mi nadhani kama kuna sherehe inahitaji hotuba ni hizi zenye maslahi kitaifa.

HATA HARUSI HUWA KUNA MUDA WA KUTOA NASAHA SEMBUSE MUUNGANO?
 
Ni kweli kabisa yani sisi ni watu wa ajabu sana, Tuna lala mika kuhusu East Africa Federation huku hatuoni malalamiko ya Zanzibar kuhusu muungano wa Tanzania
Hapa umekumbushia kitu muhimu.
usiri wanaoufanya kwenye muungano huu...pia wanaufanya kwenye mwenendo wa EAC na pengine kufika huko EA federation.

Kenya ,Uganda wanawahimiza na kuwapatia habari,taarifa wananchi wao jinsi ya kunufaika na EAC..sisi hata wabunge wetu kwenye EAC wanalalamika kuwa hawapati ushirikiano na serikali..na Sitta anasema vijana washirikishwe kwani EAC ni yao.

Siku tukianza kuwashirikisha wananchi, jamaa zetu wa Kenya na Uganda wameshatuacha masafa marefu!.....Hapo kweli tutaanza kuelewa vilio vya wazenj!

Kwa sababu serikali haituhabarishi vya kutosha ,watu tunaanza kupinga EA feredation kwa hofu ya kuzidiwa na Kenya, Uganda, ikiwa ni pamoja na kuporwa ardhi yetu au ugaidi wa Somalia...au migogoro ya Burundi na Rwanda. Na serikali inaonekana wala haijali katika hili.
 
Wazanzibari wanadanganywa na pesa za beach, watalii wataliano wanaojaza beach zao nzuri kupumziko, kuogelea na kuota jua, wengi wa mawaziri wa sasa walikuwa beach boys tu, yaani machinga wa kuwauzia vitu wazungu beach, lakini je bara ikizifungua beach zake na visiwa vyake mfano Mafia, Bongoyo, Mbudya na nyingine nyingi na kushawishi makampuni makubwa ya Italy kuwekeza bara kunako urahisi zaidi kwao na hamna udini, wazanzibari hapo watasemaje? zanzibar inaiona bara mpenzani wa kufa na kupona, wawekezaji wanaambiwa bora waende kuwekeza kenya sio bara, Tanzania bara wanaiona zanzibar kama ndugu, rafiki na mwenza wa kweli, na inadhihirisha wanapendwe na kuheshimiwa wazanzibari bara, ilhali watanzania bara zanzibar wanatukanwa kila pahala, kunyimwa fursa zote na kuonewa ovyo.

mtoa mada ameweka mambo ambayo yeye yamemfanya aamini wa zenj wanaonewa na Tanganyika, naona umeyakwepa.
 
Baada ya kusoma maoni ya jamaa wa kule Zenji wanaitwa MUWAZA nimeshawishika kuwa huu uonevu unaofanywa na watanganyika dhidi ya wazanzibar haukubaliki kwa nchi ambazo zilikubaliana kimsingi kuungana halafu nchi moja inajifanya kuwa kinara wa mwingine. Ingawa mimi binafsi sijawahi hata kukanyaga Zanzibar lakini haya mambo yanayolalamikiwa na wazanzibar yamenifanya niwaonee huruma na kupendekeza heri tuvunje muungano tu kila nchi ijiendeshe yenyewe licha ya kuwa CCM wanang'ang'ania sana muungano lakini hawauenzi. Hebu cheki huu ubazazi;

MUWAZA inashauri kwamba pana haja muhimu wa haya yote kutizamwa upya, hii inatokana na ukweli usiopingika kwamba kiini cha tatizo ni Muungano wenyewe na sio kero za Muungano tu. Kwa mfano:-
  • Muundo wa kumpora Rais wa Zanzibar Madaka ya kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais na kuanzishwa kwa cheo bandia cha Mwenza ni kati ya hatua haramu za kuvunja Makubaliano ya Muungano
  • Kumgeuza Rais wa Zanzibar kuwa Waziri wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Muungano ni kitendo kingine cha kuvunja Katiba
  • Kumshusha hadhi Rais Wa Zanzibar na kumkuza hadhi Rais wa Tanganyika ingawa hawa ni Ma- Rais wa nchi mbili huru katika suala hili la Katiba Mpya ni hatua isiyokubalika kwa Wazanzibari

Duh! Kwahiyo Tanganyika ina ikoloni Zanzibar1
 
Na mara nyingi ndo kitu ambacho viongozi huwa wanafanya,hata kwenye sherehe kama uhuru,ingekuwa busara wangekuwa wanatoa hotuba ili kuwapatia wananchi baadhi ya majibu ya manunguniko yaliyopo kwa uwazi.GWARIDE LITASAIDIAJE KUWAPUNGUZIA WANANCHI MATATIZO YA MUUNGANO?kwa dk 30 zake?

Ieleweke kuwa watu wengi hawakuwepo enzi muungano unaasisiwa, wangeweza kuelimishwa kuhusu maana na dhima ya muungano,ulikotoka,ulipo na tufanyeje ili tuuendeleze kuwaenzi wazee wetu waasisi!

Na ni wazi gharama za walipa kodi hutumika kuanzia maandalizi na posho na gharama zingine kibao,JE GWARIDE TU NDIYO DHIMA YA VIONGOZI KUCHOMA MAFUTA YA NDEGE ZETU HADI ZBAR KUKAGUA GWARIDE NA KUANGALIA HALAIKI YA WATOTO TU?

Mi nadhani kama kuna sherehe inahitaji hotuba ni hizi zenye maslahi kitaifa.

HATA HARUSI HUWA KUNA MUDA WA KUTOA NASAHA SEMBUSE MUUNGANO?

JK amegundua ya kwamba hotuba zake na viongozi wa CCM havioani na matendo yao na hali halisi na wakati wa porojo umepitwa na wakati.Wanaogopa kuzomewa live !Wakati wa Mwalimu wakati wa sherehe kama hizi alitumia jukwaa kutoa tathimini au ujumbe muhimu kwa taifa.JK katika sherehe hizo tunategemea aseme nini?CCM kujivua magamba??Katiba mpya?Kupambana na rushwa?Kelo za muungano?Ni wazi niliyoyataja hapo juu ni moja ya kelo za wananchi,lakini kutolewa kauli kero hizi toka kwa JK pamoja na CCM ni matusi kwa wananchi kwani wahusika wakuu ni wa wao wenyewe na kutoa hotuba bila kuzigusa kelo hizo haiwezekani.Hii ndiyo inaweza kua sababu kuu ya kukwepa hotuba.Ukimya pia ni majibu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Hakuna majibu ya kero za muungano, ndio maana labda ni gwaride tu!
 
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 25/04/2011 // Kitaifa // 2 Comments

بسم الله الرحمن الرحيم
UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR
TAMKO LA JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR JUU YA HALI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA
MAADHIMISHO YA SIKU YA MUUNGANO WA
TANGANYIKA NA ZANZIBAR APRIL 26, 2011 LEO TAREHE 25/4/2011
Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Sala na salamu zimshukie kiongozi wa umma huu kiislamu Bwana Mtume Muhammad (S.A W) pamoja na masahaba zake na wote walio katika njia ya haki.

Ndugu Waislamu na Wazanzibari
Sisi viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Zanzibar tukiwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu tumeamua leo kutoa tamko juu ya suala la Muungano ambao leo hii unafikia miaka 47 tokea kuasisiwa kwake.

Kila mmoja kati yetu anajua fika juu ya hali ya Muungano huo na umri wake wote na jinsi ambavyo umekuwa na mashakila makubwa tokea kuanzishwa kwake.

Pia kila mmoja wetu anajua juu ya ukweli kuwa Muungano huu umekosa kukubalika na Wazanzibari toka siku yake ya kwanza hadi leo hii.

Ushahidi wa hilo ni kuundwa kwa tume kadhaa (tume ya Nyalali, Kisanga, Shelukindo, Salmini,Amina na n.k) za uchunguzi na kutafuta maoni ambapo siku zote Wazanzibari hawakuficha hisia zao.

Si madhumuni yetu kuhoji uhalali wa Muungano kisiasa, wala si madhumuni yetu kuhoji uhalali wa Muungano kisheria, lakini ni hakika kabisa kuwa Muungano huu wa Zanzibar na Tanganyika umekuwa na utata mkubwa kiasi ambacho umekuwa na tabia ya kuwachanganya wanasiasa na wanasheria na kwa hivyo wananchi siku zote wamekuwa katika giza.

Mbali ya ukweli huo, lakini pia imekuwa ni jambo la wazi kuwa Muungano huu unakiuka misingi yake ya awali ya kuwa na pande mbili za Muungano badala yake kila dalili zinaonyesha kuwa mamlaka ya Zanzibar yanapunguzwa na kutiwa katika mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa maneno mengine ni kusema kuwa nguvu za Zanzibar kama mshirika mmoja kamili katika Muungano huo hazipo kama zilivyokuwa April 26, 1964 kwa kuongezwa Mambo ya Muungano lakini pia hata mambo yasiokuwa ya Muungano yamekuwa yakiilemea Zanzibar.

Inasikitisha kuwa Jamhuri ya Muungano imekuwa ikifanya mbinu na njama za makusudi kupopotoa mamlaka ya Zanzibar ilhali jeuri kubwa ikifanywa kwa kutumia nguvu za kisiasa na hila za kisheria na wakati huo huo wananchi kuwekwa kizani.

Kwa karibu miaka yote 47 Muungano huu umekuwa ni miliki ya chama kimoja cha kisiasa cha CCM, ukitoa miaka michache kuanzia 1964-1977. Lakini hata wakati huo Katiba ya Muda na ile iliyofuatia ilisema wazi kuwa TANu ndio chama pekee cha kisiasa

Tanzania ilhali ilikuwa ikieleweka kuwa Tanzania kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar basi kulikua na ASP ka upande wa Zanzibar.

Mambo ya msingi yamevunjwa kama vile kutoitishwa maoni ya wananchi mwanzo mwanzo kabisa katika Muungano huu lakini hilo pia halikufanywa hadi hivi leo na kwa hivyo Muungano huu haukidhi vigezo vya kisheria na kukosa Baraka za wananchi.

Hali kadhalika Muungano huu umekuwa hauna usawa basi angalau kungekuwa na uwiano, lakini hali hiyo haiko katika maeneo yote iwe ni kiuchumi, kielimu, kisiasa na hata kwenye kiutawala.

Na kwa sababu hiyo maamuzi ya Muungano huu kwa muda wake wote yamekuwa yakitoka kwa upande mmoja tu ambao ni wa Tanganyika uliovaa koti la Muungano na kwa hali hiyo Zanzibar kudhulumika katika utaratibu huo.

Kwa muda mwingi wa Muungano kumekosekana utaratibu wa wazi na wenye taaathira wa kutoa maoni na kwa hivyo sauti nyingi zilizokuwa zikitoelwa kuukosoa, kuulalamikia na hata kuukataa Muungano zimekuwa zikipotea kama moshi unaoingia katika mawingu.

Wakati hivi sasa tukikumbuka miaka 47 ya Muungano ni sadfa pia kumetokea fursa ya wananchi kutoa maoni yao jambo ambalo ni la nadra kuhusiana na Katiba ya Tanzania. Lakini sote tunajua dharau ambayo imefanyiwa Serikali ya Zanzibar na wananchi wake wakati Muswada wa kutoa maoni ya Katiba ulipoletwa kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu.

Tunaamini matukio yaliotokana na mijadla ya siku mbili ya Muswada huo bado yamo vichwani mwa wengi wetu na kwa hivyo iwe ni ushahidi kuwa Serikali ya Muungano haiko kabisa kwa maslahi ya Zanzibar kadri inavyoweza kuyakwepa.

Kwa hivyo sisi viongozi wa Kiislamu tukiwa na jukumu la kuhimiza waumini kudai haki zao na tukiwa na jukumu la kuwahamasisha raia tunatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kutodharau kabisa fursa ya kujitokeza kwa wingi wakati Muswada wa kuunda tume ya kuratibu maoni utakapokuja.

Ila wito wetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa mjadala wa muswada huo uwe mpana kuliko tulivyoona hali ilivyokuwa mwanzoni mwa mwezi huu na kwamba Muswada huo ukija tena uje na marekebisho yanayotokana na maoni ya wananchi yaliokwisha kutolewa na sio Serikali ya Muungano wa Tanzania kufanya kiburi cha kuidharu Serikali ya Zanzibar na kutenda itakavyo.

Kuhusiana na suala zima la Muungano sisi viongozi wa Kiislamu wa Zanzibar tunasimama katika mambo yafuatayo na tunawaomba Waislamu na wananchi wote wa Zanzibar waungane pamoja na kujenga hoja na sauti moja kwamba:
  1. Mjadala wowote wa Muungano utanguliwe na Kura ya Maoni kwanza kuulizwa wananchi wa Zanzibar peke yao na wananchi wa Tanzania Bara peke yao iwapo wanautaka Muungano au hawautaki na kama wanautaka ni wa aina gani.
2. Kwamba njia bora kabisa ya kuanza mjadala wa washirika wa Muungano ni kurudishwa Serikali ya Tanganyika kwanza ili Zanzibar ipate mshirika wa kujadliana nae.

Mjadala wowote ule wa Muungano ni lazima uanzie kwenye makubaliano ya awali ya Muungano na si vyenginevyo.
  1. Kwamba mjadala wowote wa Muungano ule urudishe nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano na sio ilivyo hivi sasa ambapo Rais wa Zanzibar hana nafasi ya maana wala amri yoyote ile katika Muungano.
  2. Kwamba suala la Muungano lisijadiliwe kama kwamba ni la kisiasa lakini badala yake litizamwe kama ni suala la kinchi.
Mola wetu Mtukufu tunakuomba uibarikiZanzibar na watu wake na uwalinde dhidi ya maadui wa ndani na nje. AMIN
……………………………………
Sh Thabit Mohd Saleh
AMIR- UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMUZANZIBAR
 
Back
Top Bottom