2024 Uwe ni mwaka wa kuuimarisha muungano wetu zaidi na zaidi.

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,656
20,989
Kama raia mwema na mzalendo na mpenda taifa hili la Tanzania, ipo haja ya dhati kabisa kuuimarisha muungano wetu ikiwepo kuondoa dosari zote zilizopo au zinazokinza muungano huu ili kila upande wa muungano uweze kufaidi matunda ya muungano huu adhimu,
Ipo haja pia serekali zetu kuondosha nyaraka mbalimbali ambazo wakati mwingine zimekuwa zikisambazwa mitandaoni na maadui wa umoja huu adhimu wenye jicho la husda, tunaomba waziri anayeshughulikia muungano awe makini na haya yote kwani bara na zanzibari zimeshafungamana kwa kina,
Ipo haja pia yakuweka usawa ambao utasababisha watu wa pande zote mbili kujiona ni wenye furaha ndani ya Tanzania yao,
Mfano sera za ardhi hazina budi kubadilika ili kila mtanzania aweze kanunua ardhi popote pale bara au zanzibar na akaishi kwa amani, na huu ndio muungano wa kweli, kuondosha dhana zote zenye chembechembe za mifarakano, baina ya pande mbili,
Mwaka 2024 ukawe mwaka wa kuongeza mshikamano zaidi baina ya pande mbili,
IDUMU JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
Back
Top Bottom