Kipande gani safarini huwa unakifurahia uwapo barabarani

Dom - Mbeya nafurahi sana kupita pale Mtera bwawani pia Kitonga napapenda kwa njia ya Mbeya- Dar. Furaha kubwa nikiwaga naingia mbeya pale Nanenane kwenye daraja la treni lenye kibao cha kukaribisha Mbeya
Vipi mkuu pale kwenye kona za milima ya Nyang'oro,huwa panafikirisha sana...?
 
Kuanzia Boma hadi Kia palikuwa na mashimo balaa, sijui kama siku hizi wametengeneza. Nilipita 2018 mwanzoni.
Hii road naona tanroad wanakula hela mwaka 2019 waliitengeneza ikawa nzuri mno cha ajabu haikuchukua muda mashimo yakaanza wakarudia tena saiz ipo mwake kiasi lakin viraka vimevimba uzur road imenyooka basi nikunyoosha tuu
 
Nilishwahi kusafiri kutoka Tabora hadi South Africa kwa kupitia Mozambique kwa gari hadi unahisi pumbu zinataka kutoka *****
Sijawahi kufurahia safari ya basi aisee ni shida tupu
 
1. Ikwiriri to Somanga pale baada ya kupita daraja la Mkapa kuna lami fulani hivi kama brown imetulia sana
2. Mangaka to Tunduru mkeka umetulia mbaya
3. Itigi kuelekea Tabora kabla ya ile vumbi kuna lami moja imetulia sana
4. Igunga to Nzega
5. Njombe - Makambaku yale mashamba ya chai daah huwa na enjoy kuyaona yalivyonyooka
 
Kutoka kigoma>kasulu via kibondo to kakonko hadi nyakanazi raha sana na migebuka yangu na huku natafuna kabalanga nashushia na maji, vumbi likija naachama kabisa,huwa sitaki kuona mtu mbele yangu ,
 
Sipendi kusafiri kwenye barabara safari ndefu, hivyo huwa ninalala tuu na kama ninaendesha basi nitakuwa kwenye mawazo mengine ninachopenda na kutamani nikiwa juu kiasi kutoka usawa wa bahari basi macho yangu yakutane na river basins
 
Tupeane uzoefu katika Tanzania yetu hii na dunia kwa ujumla. Mara nyingi huwa tunasafiri katika kutafuta mahitaji yetu mbali mbali ndani ya miji yetu, mikoa na hata nje ya nchi.

Hayo ya kukwea mapipa wengine hatujayaonja, tunayaona tu kwenye mamuvi. Hivyo wacha nizungumzie kuhusu suala lililopo ndani ya uwezo wangu katika safari nayo ni mabasi ya abiria.

Leo Niko safarini kutoka MBEYA kuelekea CHALINZE.

Hua mafurahi sana nikipita maeneo ya Mto Ruaha pale. Ukishamaliza kushuka kitonga Hadi unaikamata miku mijini.

Kipande kile bwana nakipenda Sana mandhari yake na gari jinsi inavofunguka.

Hebnchi u twambie ni sehemu gani unaielewa zaidi unapo safiri?
Nchi gani?
 
Tupeane uzoefu katika Tanzania yetu hii na dunia kwa ujumla. Mara nyingi huwa tunasafiri katika kutafuta mahitaji yetu mbali mbali ndani ya miji yetu, mikoa na hata nje ya nchi.

Hayo ya kukwea mapipa wengine hatujayaonja, tunayaona tu kwenye mamuvi. Hivyo wacha nizungumzie kuhusu suala lililopo ndani ya uwezo wangu katika safari nayo ni mabasi ya abiria.

Leo Niko safarini kutoka MBEYA kuelekea CHALINZE.

Hua mafurahi sana nikipita maeneo ya Mto Ruaha pale. Ukishamaliza kushuka kitonga Hadi unaikamata miku mijini.

Kipande kile bwana nakipenda Sana mandhari yake na gari jinsi inavofunguka.

Hebu twambie ni sehemu gani unaielewa zaidi unapo safiri?

songea - njombe ukipita asubuhi zile kona na milima hatari sana.
mikumi - ifakara pale gari zinajiachia sana.
Mikumi - Iringa kile kipande ya mto Ruaha ndani ya Super Feo raha sana.
 
Back
Top Bottom