Kipande gani safarini huwa unakifurahia uwapo barabarani

kwenda moro dar ukiwa na private car kula lunch ile restaurant pale msolwa filling station so relaxing alafu mule ndani unakutana na ma VIP tu nishakaa meza moja na mawaziri wawili tukawa tunapiga story kama wanachi wa kawaida tu
Mawaziri ni watu tu kama wengine wala usi-complicate
 
Dom - Mbeya nafurahi sana kupita pale Mtera bwawani pia Kitonga napapenda kwa njia ya Mbeya- Dar. Furaha kubwa nikiwaga naingia mbeya pale Nanenane kwenye daraja la treni lenye kibao cha kukaribisha Mbeya
 
Kwa madereva wa IT na malori, mlima Chiweta Malawi ni zaidi ya kuwa ndani ya Bombardier, hapa ziwa Nyasa linaonekana kama limeinuka, nyumba na watu huko chini hawaonekani kwani wadogo kama sisimizi.
Mlima Kawetere Mbeya kwenda Chunya, hii ndiyo sehemu ya barabara iliyo kina kirefu kwenda huu kutoa usawa wa bahari Afrika, hapa ukuta wa bonde la ufa unaonekana vizuri sana ambapo bonde la Usangu linaonekana kama uwanja wa mpira wa Mkapa.
 
Zipo nyingi ila hizi tatu kwangu ni bora zaidi;

1: Muleba to Chato
Hapa utaona view zuri ya Ziwa victoria alafu na milima pia Mbuga mpya. Ukipita mida ya saa mbili to saa nne utaweza pata kijua kitamu cha asubuhi kutoka ziwani

2: Katoke to Muleba via

Hapa kama unauoga lazima utajikojolea, kwa maana unapita katika Biharamulo game reserve, msitu ambao upo kimya alafu kila baada ya kilometer fulani unakutana na Berria ya wanajeshi alafu umezungukwa na milima tuuh

3: Kateshi to Babati

Hapa utakutana na mlima Dareda ambao una S na kona kali sana pia road yake bado ni mpya alafu hali ya ubaridi na ukungu...
 
Korogwe - mombo - same hii road pita jion muda traffic hakuna n kupepea tuu ila kwenye basi baada ya kula mombo abiria hutulia wakishikilia Roho zao sababu ya dereva na spidi mana abiria hawajui kuwa barabara inakuita
 
Makambako - Njombe, maeneo yale huwa nafurahia sana.
Lamadi - Bunda safi kabisa, nikifika eneo hiki akili yangu huwa inatulia sana.
 
Sema barabara ikiwa nzuri unamwagika hatari nishwah tumia Dakika saba kutoka mwenge BP (saiz Puma) mpaka bunju ndan ndan huko panaitwa minazini kipindi ndo ile double road imekamilika
 
kwenda moro dar ukiwa na private car kula lunch ile restaurant pale msolwa filling station so relaxing alafu mule ndani unakutana na ma VIP tu nishakaa meza moja na mawaziri wawili tukawa tunapiga story kama wanachi wa kawaida tu

Lile chimbo ni taam sana na pale unakutana na watu wenye hadhi tu, mimi nikimaliza kula nyama naingia supermarket yao napata juice baridi ya ceres halafu naondoka
 
Back
Top Bottom