Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 912
- 4,249
Mzee Kinana akizungumza na viongozi wa CCM DAR es salaam ameeleza kwamba CCM imeondoa kesi tisa za jinai walizowafungulia chadema mahakamani na sasa hivi wanaangalia namna ya kufuta kesi mbili zilizobaki.
Kwa kauli ya Kinana ni kwamba anajivunia CCM kuwafungulia kesi za jinai wanachama wa chadema na kisha kuzifuta na kwamba kufanya hivyo wana Chadema wanapaswa kumpongeza mwenyekiti wa CCM
Tujiulize upo wapi uhuru wa mahakama? Je, tulifahamu kwamba kesi 11 za wanachama wa chadema zilifunguliwa kwa maelekezo ya kamati kuu ya CCM? Tulifahamu kwamba katika majadiliano chadema walitlelekezwa kukaa kimya bila kufanya siasa ili kesi zifutwe?
Je , CHADEMA wakiendelea kufanya siasa na kupata nguvu awawezi kufunguliwa tena kesi kama zilivyofunguoiwa awali?
Kama mwenyekiti wa CCM anaweza kufuta kesi za jinai, anatumia kifungu gani cha sheria?