KINACHOWAANGUSHA WANASIASA KIMBIAKIMBIA HIKI HAPA

Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
541
175
TAMAA ya madaraka na fedha, ni sababu kubwa zilizowasambaratisha wanasiasa wengi waliowahi kuvuma ndani ya vyama mbalimbali vya siasa nchini tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kisha wakajisalimisha CCM.

Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitumia turufu hiyo kuwasambaratisha wanasiasa hao, wao hujielekeza kufikiria zaidi vyeo na fedha.

Wako viongozi wengi waliowahi kuvuma ndani na nje ya nchi wakiwa upinzani, lakini baada ya kurudi CCM, rekodi zao zimefifia kana kwamba hawapo tena kwenye ulingo wa kisiasa.

Orodha hiyo ni ndefu, lakini kwa kutaja japo kwa uchache wako wanasiasa kama Dk. Walid Aman Kabouru, Dk. Masumbuko Lamwai, Prince Bagenda, Tambwe Hiza na Daniel Nzanzugwako na Augustino Mrema

Wapo pia Danny Makanga, Teddy Kaselabantu, Fatuma Maghimbi, Makongoro Nyerere, Thomas Ngawaiya, Justin Sarakana, Frank Magoba na wengineo.

Hawa walipata kuwa viongozi ndani ya vyama vya NCCR-Mageuzi, CHADEMA, CUF na TLP, lakini baada ya kusaliti upinzani na kurudi CCM walivuma kwa muda mfupi kisha wakazimika kisiasa ikiwa ni pamoja na kushindwa kura za maoni ndani ya chama.

Katika kuzungumzia anguko hilo, baadhi ya wanasiasa waliowahi kufanya harakati za siasa na vigogo hao walitoa sababu kadhaa za kuporomoka kwa wenzao.

Mabere Marando ni mwanasheria na Katibu Mkuu wa kwanza wa NCCR-Mageuzi ambaye amefanya kazi za siasa na takribani wanasiasa wengi waliotajwa hapo juu.
aliwahi kutaja sababu tatu. Kwanza alisema wakati wapinzani wanasaka vyeo na fedha CCM, malengo ya chama hicho tawala ni kuwaangamiza kisiasa.

Marando ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, alisema kuwa sababu ya pili ni kwamba umaarufu wa mpinzani hutokana na chama pamoja na ukosoaji wa kutetea wananchi.

“Ukiwa CCM unatetea serikali si wananchi, ndiyo maana watu hawa wakienda huko wanapotea kabisa kisiasa,” alisema.

Katika sababu ya tatu, Marando alisema mpinzani akirudi CCM anakuwa mgeni, kwamba wapo baadhi ya wanachama wasiopenda wanasiasa wanaorudi huko wapewe vyeo, hivyo inakuwa vigumu kushirikiana nao.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, aliwahi kusema kuwa siasa ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu, ambapo CCM hulazimika kuwachukua wanasiasa wenye nguvu na kushindwa kuwapa nafasi katika chama hicho.
Lwakatare ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani bungeni 1995/2000, alipata kunukuu kuwa,hatua hiyo inasababisha wanasiasa waliohamia chama hicho kupotea katika medali ya siasa kutokana na kukaa benchi.

Alisema kuwa umaskini umekuwa tatizo kubwa linaloathiri wanasiasa hao kwa kuwa wanashindwa kuelewa suala wanalopigania kutokana na kutanguliza maslahi binafsi.
“Hata hivyo, wanasiasa hao wanapotea kutokana na kutofahamu nyumba aliyohamia, anashindwa kuifahamu sawa sawa,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, pia aliwahi kusema kuwa kuhama vyama kuna matatizo yake ambapo kunasababisha baadhi ya mashabiki wako kushindwa kukuamini na pia kupoteza heshima uliyokuwa nayo.

Mtatiro alisema kuwa mara nyingi mwanasiasa anakuwa na nguvu kutokana na itikadi yake kwa wakati ule, lakini anapoondoka ndani ya chama hicho hujikuta akipoteza wafuasi wote.

Alisema kuwa hatua hiyo inaweza kuwagharimu wanasiasa na hata kuchukua kipindi kirefu kuweza kurudi katika nafasi ya juu waliyokuwa nayo.

Pia kuna wanasiasa wengine ambao hawana ushwawishi wowote kisiasa hata wanapohama hawana madhara yoyote ndani na nje ya chama mfano ni baadhi ya wanasiasa wengi ambao walitimkia upinzani mwaka 2015 baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kujiunga na CHADEMA na kugombea urais na wakamfuata na bila wao kujua Lowassa alishakuwa na Political Supremacy yake ya toka muda mrefu wakifikiri kuwa itawabeba wao binafsi bila kufanya utafiti binafsi wa kisisasa.

Rekodi za walioanguka

Masumbuko Lamwai:
Huyu aliwahi kuwa mbunge wa Ubungo (NCCR-Mageuzi), mwanasheria wa chama kisha akarudi CCM na aliteuliwa kuwa mbunge, lakini sasa amepotea kisiasa.

Danny Makanga:
Alikuwa mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), akavurugana na mwenyekiti wake John Cheyo, kisha akavuliwa uanachama na kuhamia CCM.Akawa Mkuu wa Wilaya ila kisiasa havumi tena.

Marehemu:Hiza Tambwe:
Alikuwa NCCR-Mageuzi kisha akagombea ubunge Temeke kupitia CUF. Huyu alivuma na aliwahi kuapa kwamba kurudi CCM ni sawa na kulala na mama yake mzazi, lakini akaenda CCM baada ya uchaguzi wa 2010 baadaye akaenda CHADEMA akisema katika mkutano wa hadhara kuwa huwezi kwenda peponi ukiwa CCM.
alipokuwa CCM,alianza kupewa kitengo cha propaganda, lakini baadaye akaondolewa akawa mwanachama wa kawaida wa CCM asiyekuwa na umaarufu kama zamani. (Mungu amlaze pema peponi).


Thomas Ngawaiya:
Alianzia NCCR-Mageuzi kisha akageuka na Augustine Mrema kwenda TLP, akachaguliwa mbunge wa Moshi Vijijini 2000/2005 kisha akarejea CCM.

Huko alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa Kilimanjaro, lakini sasa ametupwa nje na hata alishindwa kura za maoni za kugombea ubunge wa Moshi Mjini ambapo katika kura za maoni aliambulia kura sifuri (0) na sasa haifamiki alipo.

Dk. Walid Aman Kabouru Marehemu:
Huyu alikuwa Katibu Mkuu CHADEMA na mbunge wa Kigoma mjini, lakini akarudi CCM na akawa mwenyekiti wa chama Mkoa wa Kigoma ingawa alififia kisiasa.

Daniel Nsanzugwako:
Alikuwa Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, baadaye akarejea CCM na kushinda ubunge Jimbo la Kasulu Vijijini, kisha akateuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Wakati wa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri alitupwa nje na mwaka 2010 akadondoshwa jimboni na Zeituni Buyogela wa NCCR-Mageuzi, sasa havumi tena.

Makongoro Nyerere:
Huyu ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Alivuma sana mwaka 1995 aliposhinda ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

Baadaye ubunge wake ulitenguliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kisha akarejea CCM na kuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa mbunge halafu akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara.

Kwa sasa Makongoro amepoteza nafasi hiyo akawa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia CCM, lakini nyota ya kisiasa imefifia.

Fatuma Maghimbi:
Huyu ni mbunge wa kwanza mwanamke wa upinzani kuchaguliwa jimboni huko Wawi visiwani Zanzibar 1995/2005 kwa tiketi ya CUF, lakini baadaye alirejea CCM na sasa amefifia.

Teddy Kaselabantu:
Alianzia UDP akiwa Katibu Mkuu na mbunge wa viti maalumu 2000/2005, kisha akahamia CCM na kushinda jimbo la Bukene mkoani Tabora 2005, halafu akashindwa kura za maoni 2010 na hivyo ikawa safari yake ya kupotea kisiasa.

Prince Bagenda:
Huyu alivuma ndani ya NCCR-Mageuzi. Mwaka 1995 aligombea ubunge Muleba Kusini na kushindwa kwa mizengwe na Wilson Masilingi wa CCM.

Mwaka 1997 matokeo hayo yalitenguliwa baada ya Bagenda kushinda kesi. Hata hivyo wakati wa uchaguzi mdogo chama chake kilikuwa na mgogoro na hivyo akashindwa kukidhi kigezo. Kwa sasa yuko CCM na kisiasa hakumbukwi tena.

Frank Magoba:
Alipata kuwa mbunge wa Kigamboni kupitia CUF 2000/2005 kisha akatimkia CCM na kugombea ubunge tena kwa CCM pia aliambulia kura sifuri(0) ya maoni akaenda kugombea ubunge Mbeya vijijini ambako alikosa na sasa kisiasa hajulikani tena.

Stephen Wassira:
Huyu pekee ndiye ameweza kuendelea kuvuma hata baada ya kutoka upinzani na kurudi CCM.

Alivuma akiwa NCCR-Mageuzi ambapo alishinda ubunge wa Bunda mwaka 1995, lakini baadaye akaenguliwa na Mahakama Kuu kufuatia kesi iliyofunguliwa na mshindani wake Jaji Joseph Warioba.

Baadaye alihamia CCM ambako amekalia jimbo hilo vipindi viwili huku akishika wadhifa wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu).

Agustino Lyatonga Mrema
Huyu aliwahi kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani akafukuzwa uanachama CCM,akaungana na NCCR mageuzi ambapo alisumbua mno katika uchaguzi wa mwaka 1995,ambako nakumbuka Mwalimu Nyerere alikosa usingizi baadaye uchaguzi uliofuata chama chake kilipoteza majimbo mengi na ukawa mwanzo wa migogoro katika chama chake baadae akatimkia TLP akawa mwenyekiti akagombea ubunge Vunjo mwaka 2005 akakosa,mwaka 2010 akarusha kete yake tena akafanikiwa akageuka mbuge wa chama tawala bungen,mwaka 2015 akagombea tena Vunjo huku akijipenyeza hadi kwa mgombea wa CCM Magufuli alipokuwa katika kampeni Rombo akamuomba amuombee kura lakini aliangushwa vibaya na bwana James Mbatia katika uchaguzi ule na miaka miwili iliyopita rais Magufuli akamteua kuwa mwenyekiti wa Bodi ya PAROLE lakini lyatonga Mrema yule wa kipindi kile kisiasa hayupo tena.
 
Back
Top Bottom