Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi

Jafari Haruna

JF-Expert Member
Jun 18, 2017
347
962
Narudia tena ni Udhalilishaji, Upuuzi, Ushenzi, Uchonganishi na Utapeli.

Nimefika mkoa wa Kigoma Tokea Majuzi nilicho Kikuta huku Sielewi Huku ninchi Nyingine au ni Tanzania hii hii !

Kuna kitu kinaitwa  KAMCHAPE, hawa wapuuzi nani kawaleta, Hili kweli nani kalipa Baraka kufanyika karibu mkoa mzima wa Kigoma?

Kinachofanyika Ni Udhalilishaji na Uchonganishi kwa jamii.

Kwanza Wanachangisha Tsh 5,000 kila kaya kwa lazima sio ombi.

Kisha Wanapita kila nyumba Eti wanatoa Uchawi na wachawi! Tena utake usitake lazima.

Wakifika kwako wanasema hapa kuna uchawi Lazima uchapwe kisha unanyolewa Nywele Mbele ya umati wa watu kisha kunyweshwa Kile wanachoKiita Dawa hautakuwa mchawi tena!

Nimefuatilia kinachofanyika pale ni Mazinga Ombwe na Kujipatia Pesa kwa Utapeli!

Wakati Yakifanyika hayo Kijiji Jirani, Nyie mnaanza jiandaa na kama mwenyekiti hata Wakaribisha hao watu au kuchangisha hizo pesha kila kaya naye Anajumuishwa kwenye Kundi moja la Wachawi !

Kuna vitu vya Ajabu sana Vinafanyika mpaka nimeshikwa na Butwaa. Nimeuliza nikaambiwa Serikali Ndio Imeruhusu hili Lifanyike Mkoa mzima kweli?

Mbona Sioni Dodoma na Mbeya Kwanini Kigoma?

Kwasasa zoezi limepamba Moto Vijiji vya Nyarubanda, Kalinzi, Mukigo, Muhinda, Nyaruboza, Rukoma, Igalula, Mgambo, Katumbi, Kalya Nk.

Huko kumechafukwa hali ni mbaya na lisipofanyiwa kazi na kuacha litaleta shida kwa watu

======================
UPDATE: 13/09/2023
Hatimaye Jeshi la Polisi limeingilia Kati jambo Hili

Pia soma
- Mfahamu 'Kamchape' mkamata wachawi na shughuli zake kwa ujumla kutokea hapa Mkoani Kigoma
 
Haya yanafanyika hata huko songwe na chunya.Ni nani huwa anawaruhusu hawa wapuuzi? Hivi wakuu wa mikoa na wilaya ambao ndo wakuu wa ulinzi na usalama kazi yao ni nini dhidi ya kuwalinda wananchi hasa kwenye upuuzi kama huu?

Tanzania nchi ya hovyo sana
 
Narudia tena ni Udharilishaji,Upuuzi, Ushenzi,Uchonganishi na Utapeli.

Nimefika mkoa wa Kigoma Tokea Majuzi nilicho Kikuta huku Sielewi Huku ninchi Nyingine au ni Tanzania hii hii !

Kuna kitu kinaitwa  KAMCHAPE,
hawa wapuuzi nani kawaleta, Hili kweli nani kalipa Baraka kufanyika karibu mkoa mzima wa Kigoma?

Kinacho fanyika Ni Udharilishaji na Uchonganishi kwa jamii.

Kwanza Wanachangisha Tsh 5000 kila kaya kwa lazima sio ombi.

Kisha Wanapita kila nyumba Eti wanatoa Uchawi na wachawi!
Tena utake usitake lazima.

Wakifika kwako wanasema hapa kuna uchawi Lazima uchapwe kisha unanyolewa Nywele Mbele ya umati wa watu kisha kunyweshwa Kile wanacho Kiita Dawa hautakuwa mchawi tena!

Nimefuatilia kinacho Fanyika pale ni Mazinga Ombwe na Kujipatia Pesa kwa Utapeli!

Wakati Yakifanyika hayo Kijiji Jirani
Nyie mnaanza jiandaa na kama mwenyekiti hata Wakaribisha hao watu au kuchangisha hizo pesha kila kaya naye Anajumuishwa kwenye Kundi moja la Wachawi !

Kuna vitu vya Ajabu sana Vinafanyika mpaka nimeshikwa na Butwaa.
Nimeuliza nikaambiwa Serikali Ndio Imeruhusu hili Lifanyike Mkoa mzima kweli?

Mbona Sioni Dodoma na Mbeya
Kwanini Kigoma?

Kwasasa Zoezi limepamba Moto Vijiji vya
Nyarubanda,Kalinzi,Mukigo,Muhinda,Nyaruboza,Rukoma,Igalula,Mgambo,Katumbi,Kalya Nk.

Huko Kumechafukwa hali ni mbaya na Lisipo Fanyiwa kazi na Kuacha Litaleta Shida kwa watu
Hawajakutana na watu jeuri. Kuna sehemu ilikuwa inafanyika huu ujinga, mzee mmoja akatoka na gobole apiga risasi moja hewani wacha watimue.
 
Wakati Yakifanyika hayo Kijiji Jirani
Nyie mnaanza jiandaa na kama mwenyekiti hata Wakaribisha hao watu au kuchangisha hizo pesha kila kaya naye Anajumuishwa kwenye Kundi moja la Wachawi !
Wenyeviti wa CCM hawa
 
Upuuzi huu niliwahi kuuona ukifanyika vijiji fulani moshi vijijini ukanda wa chini. Sikukubaliana nao kuchanga pesa kwa ajili ya kutoa uchawi kwenye nyumba za wanakijiji. Mbaya zaidi wanakijiji walichanga ili uchawi utolewe kwenye shule yao. Waliingia hadi ofisi ya mkuu wa shele wakidai bosi wetu ni mshirikina kuna uchawi kauhifadhi ofisini kwake na nje ya shule kachimbia uchawi hivyo ufukuliwe. Wenye akili hatukumuogopa huyo mganga tuliishia kumcheka kwa maigizo yake kuwa amefukua jini na kuanza kufukuzana nalo eti alikamate na kuliteketeza kwa madawa yake. Uongo mtupu wajinga wanadanganywa kwa kukosa elimu
 
Upuuzi huu niliwahi kuuona ukifanyika vijiji fulani moshi vijiji ukanda wa chini. Sikukubaliana nao kuchanga pesa kwa ajili ya kutoa uchawi kwenye nyumba za wanakijiji. Mbaya zaidi wanakijiji walichanga ili uchawi utolewe kwenye shule yao. Waliingia hadi ofisi ya mkuu wa shele wakidai bosi wetu ni mshirikina kuna uchawi kauhifadhi ofisini kwake na nje ya shule kachimbia uchawi hivyo ufukuliwe. Wenye akili hatukumuogopa huyo mganga tuliishia kumcheka kwa maigizo yake kuwa amefukua jini na kuanza kufukuzana nalo eti alikamate na kuliteketeza kwa madawa yake. Uongo mtupu wajinga wanadanganywa kwa kukosa elimu
Zamani sana nikiwa primary school niliwahi kuona huo ujinga huko Moshi kuna lijamaa lilikuwa linajiita profesa maji marefu linazungukia vijiji eti kutoa uchawi.
 
Hawajakutana na watu jeuri. Kuna sehemu ilikuwa inafanyika huu ujinga, mzee mmoja akatoka na gobole apiga risasi moja hewani wacha watimue.
Mm naona Hilo jambo liendelee....Kule Kuna Imani za kishirikina sanaa....Kuna Vizika wazima...Kuna jamii Kule Huwa hawarudigi kwao.... kwenye mtiani wa form 6 Kuna jamaa mmoja wa Kigoma gafla akaanza kuanguka mapepo miaka 20 iliyo pita...

Yaan alifanya mitiani Kwa mbinde mapepo hayataki asome......

Hii ardhi hii imebeba mengi yaan acha tu.....DUNIA INA MAMBO KAMA WASEMAVYO WATU PORI...
 
Upuuzi huu niliwahi kuuona ukifanyika vijiji fulani moshi vijiji ukanda wa chini. Sikukubaliana nao kuchanga pesa kwa ajili ya kutoa uchawi kwenye nyumba za wanakijiji. Mbaya zaidi wanakijiji walichanga ili uchawi utolewe kwenye shule yao. Waliingia hadi ofisi ya mkuu wa shele wakidai bosi wetu ni mshirikina kuna uchawi kauhifadhi ofisini kwake na nje ya shule kachimbia uchawi hivyo ufukuliwe. Wenye akili hatukumuogopa huyo mganga tuliishia kumcheka kwa maigizo yake kuwa amefukua jini na kuanza kufukuzana nalo eti alikamate na kuliteketeza kwa madawa yake. Uongo mtupu wajinga wanadanganywa kwa kukosa elimu
Sasa Kigoma Anachukiliwa Chura Wale Wakubwa sana
Kawekwa kwenye Kitambaa chekundu Kisha wakiingia Ndani wanatoka eti wamenasa Kitu kibaya Wanakiweka Chini kina ruka au Kutikisika Basi Wananchi wanaamini Kimetilewa Kitu
 
Mm naona Hilo jambo liendelee....Kule Kuna Imani za kishirikina sanaa....Kuna Vizika wazima...Kuna jamii Kule Huwa hawarudigi kwao.... kwenye mtiani wa form 6 Kuna jamaa mmoja wa Kigoma gafla akaanza kuanguka mapepo miaka 20 iliyo pita...

Yaan alifanya mitiani Kwa mbinde mapepo hayataki asome......

Hii ardhi hii imebeba mengi yaan acha tu.....DUNIA INA MAMBO KAMA WASEMAVYO WATU PORI...M
Kwenye Hayo Mapepo Basi Hujui Ukanda wa Pwani Na Zanzibar ww
 
Ukikataa kuwapa hio 5000 wanakufanya nin ? ..

Wanakupeleka polisi ?

Wanakupeleka mahakamani ?

Wajinga ndio waliwao ...
Iliwahi kutokea huko Ruvuma miaka kama 5 iliyopita. Kuna dogo mmoja alikuwa anaitwa Faki ndiye aliyekuwa mganga wa kuumbua wachawi (kama wajinga wanavyoamini). Gharama kila kaya ilikuwa tsh 5000. Asiyetaka kutoa alipigwa au kunyang'anywa kitu cha thamani ya 5000 au zaidi. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa wasioyataka mambo hayo walokole na wengine. Mkuu wa mkoa wa wakati huo ndg Saidi Mwambungu aliokoa jahazi kwa kuzuia. Mabomu ya mchozi yalihusika ...
 
Usikie tu uchawi na wachawi, hawafai kutengamana na jamii. Hukumu ya mchawi ni kuuwawa. Hawa ndiyo visababishi vya umasikini. Utakuta wanaroga watoto wanashindwa kwenda shule. Wachawi wanakwamisha maendeleo ya watu. Kwa maoni yangu washughulikiwe kwa nguvu ili waache uchawi. KAMCHAPE OYEE
 
Back
Top Bottom