kina mama nawaulizeni.........

it's complicated I guess.

Kuolewa si bahati, bahati kumpata mwenza wa kaliba unayoitaka.
Unaweza jikuta umezungukwa na akina karum.ekenge tu.
kama ni hivyo mbona wanawake wengi wanakubali kuolewa at any cost mradi avae shela?
 
Kuolewa ni bahati kama uko nyumbani unasubiri kuolewa,kama unakazi yako sidhani kama ni bahati manake huwi tegemezi kwa mume.
 
Kuolewa ni Bahati??? Bahati ya nini sasa!!!

Mpango mzima ni kumpata mume/mke bora na si mradi ndoa tu

Bishanga una kesi ya kujibu
 
kuolewa sio bahati Bishanga, bahati ni kumpata wa kufa na kuzikana. kuna dada 1 ye anasema me nataka kuolewa ndio. ila naolewa ili niachike ili niondoe nuksi kwetu. so kuolewa sio bahati kuna wanaoolewa kusafisha jina na kupata michango miingi ilhali mind set zao hazipo kabisaaaa ktk ndoa. ....
 
Last edited by a moderator:
"Binafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati". Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake, anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake, anaemsikiliza mwenzake, anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . . wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu.

Kuoa/kuolewa sio bahati hivyo usibahatishe" Lizzy

Hii nimeichukua kwny uzi wa Lizzy na ni kwa faida ya wale wooote ambao hawajaisoma na we Bishanga hebu rejea hapo!
 
Last edited by a moderator:
Wewe Bishanga umeoa? Je una uhakika mai waifu wako ana bahati kuolewa na wewe na kwa vipi? Ukijibu hili utakuwa umeelewa kama kuolewa ni bahati au la.
 
sasa Purple utaishije bila mme mji huu,na ham ya kudo unaikabili vipi bila mwenza,au ndo yale ya Darlingtone na @serafina ?

Bishanga mpango mzima kwenye dunia ya leo ni pesa,hayo mengine yanarekebishika studio,mume wa kazi gani zaidi ya kukusababishia mtikisiko wa ubongo?mara leo karudi na ndom yenye mchuzi,kesho kanishushia kipondo,kesho kutwa anarudi asubuhi tena akiwa kaibiwa everything na amelewa chakali! Sasa waume wa dizaini hii ndo wamejaa tele huko kwenye ndoa bahati itatoka wapi??
No thank you!
 
Last edited by a moderator:
Kuolewa ni bahati kama uko nyumbani unasubiri kuolewa,kama unakazi yako sidhani kama ni bahati manake huwi tegemezi kwa mume.
mmmmmhhhh haya bana ila najua wasomi kibao nao wanasema kuolewa ni bahati.
 
Lizy, nadhan bahati aisemeayo bishanga ni hata wewe uliempata anaekufaa na yule ambaye amempata asiemfaa. Sasa bas bahati yenyewe inakuja vipi? 1.nzi "Dungadunga sepa" wamekuwa wengi. Wanatua kwenye msosi wakishachafua wanakimbia 2. Maisha utata hvo kla mmoja kuogopa kuingia ktk majukumu ya ziada. 3. Beijing imewaharbu wengi wanawake hvyo wanaume wanaogopa vita. 4. Wanaume wamekuwa wachache na uchache ukzdishwa na wanaume mashababi wamepungua...naruhusu kukosolewa
 
Last edited by a moderator:
Kuolewa ni Bahati??? Bahati ya nini sasa!!!

Mpango mzima ni kumpata mume/mke bora na si mradi ndoa tu

Bishanga una kesi ya kujibu
nimekosa nini tena shem wangu mpenzi,kwanza hata simu ulizima wewe.
 
Back
Top Bottom