Kimenuka mambo ya nje, vigogo wasimamishwa kwa ufisadi

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Wakati Kamati za Bunge zikiendelea kuchambua Bajeti za Wizara mbalimbali katika mchakato wa kuelekea Bunge la Bajeti, habari zilizotufikia zinaeleza kuwa vinara wanne Mambo ya Nje wamesimamishwa kutokana na matukio ya Ufisadi.

Kusimamishwa kwao kunakowahusu vigogo wa Idara mbili nyeti katika Wizara hiyo na Afisa mmoja mdogo kunatokana na tuhuma za kuvuna fedha pasipo kazi husika kufanyika.

Source: Mbopo aliyepo hapo Mambo ya Nje
 
Mkuu ni vizuri utupe majina ya hawa waliosimamishwa na kwakweli utoe evidence nzuri ili tuweze kuamini wana jf.
 
Mkuu ni vizuri utupe majina ya hawa waliosimamishwa na kwakweli utoe evidence nzuri ili tuweze kuamini wana jf.

Mkuu Ruhinda vuta subira punguza Presha Mbopo anakuja kuweka majina hapa akichelewa sana nitabidi kumsaidia kazi maana naona yuko busy anaandaa statement
 
Sasa kwanini usisubiri Mbopo alete taarifa kamili? Haraka ya nini? Aaaaaaaaaaaaaahhh
 
Sasa kwanini usisubiri Mbopo alete taarifa kamili? Haraka ya nini? Aaaaaaaaaaaaaahhh

Gerrard Mbopo yuko busy sana na mambo ya bajeti, sasa naanza na Wahasibu wawili na Bosi wa Idara ya Itifaki nadhani majina atayaweka sasa
 
  1. Vigogo Wizara ya Afya wasimamsihwa kazi
  2. Vigogo saba wasimamishwa kazi Tazara
  3. VIGOGO WATATU WASIMAMISHWA KAZI KASHFA YA WANYAMAPORI
  4. Wanne wasimamishwa kazi Tanapa.
  5. Mwakyembe awang'oa vigogo ATCL
  6. Waziri amtimua kigogo bodi ya pamba
Nchi iliyojaa usaniii, na sarakasi nyingi.....
 
hizi ni ndoto za mchana tena unaonga maji haiingii akili kuwa leo hii ccm ndio imeamka au ndio mfa maji?
 
Jamani kama ni kweli kwamba maafisa wanne wamesimamishwa kazi Wizara ya Mambo ya Nje basi uungwana ni vizuri kuipongeza Wizara hii kwa kuwa proactive kila linapotokea tatizo kama hilo. Na hii inaonyesha kwa kiasi gani Wizara hii risk register zake zinafanya kazi. Hazina Waliposema Wizara ya Mambo ya Nje ilikuwa ni Wizara ya kwanza kuwa na operationasation ya risk register sikuona umuhimu wake.

Suala la pili ni suala la semantics, huwezi kumsimamisha kazi mtu kwa ufusidi. Hawa watu watakuwa wamesimamishwa kwa sababu za uchunguzi. Huwezi kuitwa fisadi mpaka pale kamati inapobaini kwamba wewe ni kweli mwizi.

Lakini wanaJFK lazima tuipongeze Wizara hii kwa umakini mkubwa wa kuona viashiria vya Wizi badala ya kusubiri Mpaka wabunge ama CAG aseme.

Naona hata moto aliouwasha Kagasheki na Mwakyembe sasa na Membe unazudi kushika kasi.
 
  1. Vigogo Wizara ya Afya wasimamsihwa kazi
  2. Vigogo saba wasimamishwa kazi Tazara
  3. VIGOGO WATATU WASIMAMISHWA KAZI KASHFA YA WANYAMAPORI
  4. Wanne wasimamishwa kazi Tanapa.
  5. Mwakyembe awang'oa vigogo ATCL
  6. Waziri amtimua kigogo bodi ya pamba
Nchi iliyojaa usaniii, na sarakasi nyingi.....

Mzazi umemaliza kila kitu lol

Hamna kitu hii nchi.
 
Kila ukona Ufisadi wakati gharama za maisha zinazidi kupanda umeme haukamatiki, petrol iko juu, mafuta ya taa ndio hakuna kabisa,vyakula kila siku vinapanda. Ada za shule hii nchi ni nani anaishi kwa raha zaidi ya mafisadi?????
 
Hivi kuna wizara au kampuni ya umma ambayo haina ufisadi?
Serikali yote inanuka kama mzoga wa chura.
 
  1. Vigogo Wizara ya Afya wasimamsihwa kazi
  2. Vigogo saba wasimamishwa kazi Tazara
  3. VIGOGO WATATU WASIMAMISHWA KAZI KASHFA YA WANYAMAPORI
  4. Wanne wasimamishwa kazi Tanapa.
  5. Mwakyembe awang'oa vigogo ATCL
  6. Waziri amtimua kigogo bodi ya pamba
Nchi iliyojaa usaniii, na sarakasi nyingi.....

NI KWELI.... HALAFU SIJUI KIGOGO ilitoka wapi

kule kwetu boding enzi zile tulikua tunasema Gogo ni kimba; kwahiyo vigogo ni vikimba
 
Back
Top Bottom