Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Balozi wa Japan pamoja na Waziri Magufuli wametangaza kuwa barabara ya Kilwa iliyojengwa chini ya kiwango, kurudiwa tena kujengwa upya.
Balozi wa Japan ameomba msamaha kwa kampuni ya Kajima kutokujenga kwa kiwango barabara hiyo. Kampuni ya Kajima itarudia kujenga kwa gharama zake.
Ahsante Kikwete, ahsante Magufuli, ahsante Balozi wa Japan.
Makosa yametendeka, makosa yameonekana, makosa yamekubalika, makosa yanarekebishwa. Huo ndio uongozi mahiri na si kulalama tu kutwa kucha.
Mh. Kikwete kupongezwa kwa hili ni jambo jema na ni stahili yake, kama tu vile anavyopaswa kukosolewa na kubebeshwa lawama za kero na adha zisizopungua zitokanazo na ukosefu wa maadili ya uongozi ya watumishi mbalimbali aliowateua na ulegelege uliodhahiri katika majukumu yake mengi hapa nchini!!