Barabara ya Kilwa inapitika vizuri baada ya kazi ya ujenzi kumalizika. Ila tatizo ni mifereji. Kuna uzembe kiasi kwamba sehemu kadhaa zimeanza kuonyesha mmomonyoko hasa kuanzia kwa Aziz Ali hadi Mbagala Rangi Tatu.
Pili, baadhi ya madreva wanaegesha magari yao kwenye sehemu iliyoachwa wazi (katikati ya barabara) hasa kwa Aziz Ali, Mtoni-Mtongani na maeneo ya Mbagala Rangi Tatu.
Tatu, kwenye 'round abouts' kumeanza kuonyesha uharibifu pia. Kunakuwa na matutamatuta kwenye lami. Baadhi ya watu wanasema barabara haikujengwa kwa ubora unaotakiwa kwa vile ulikuwa msaada kutoka serikali ya Japan, hivyo wahusika hawana uchungu na fedha iliyotumika na ndio maana mifereji imeachwa bila kujengwa vizuri au sehemu zile ambazo imejengwa siyo kwa ubora unaotakiwa.
Nne, kwa vile barabara yenyewe imejengwa bila ya kuwekwe njia za dharura, madreva wanatumia nafasi inayotumiwa na waenda kwa mguu ili kugeuza gari kama wanataka kurudi walikotoka au kama kuna haja ya kwenda kwenye kituo cha mafuta.
Je, wengine ambao mmeshatumia barabara hiyo mnasemaje?
========
August 2011:
Magufuli kwa kuwafanya Kajima warudie barabara ya Kilwa, umeonyesha leadership!

Balozi wa Japan pamoja na Waziri Magufuli wametangaza kuwa barabara ya Kilwa iliyojengwa chini ya kiwango, kurudiwa tena kujengwa upya.
Balozi wa Japan ameomba msamaha kwa kampuni ya Kajima kutokujenga kwa kiwango barabara hiyo. Kampuni ya Kajima itarudia kujenga kwa gharama zake.
Ahsante Kikwete, ahsante Magufuli, ahsante Balozi wa Japan.
Makosa yametendeka, makosa yameonekana, makosa yamekubalika, makosa yanarekebishwa. Huo ndio uongozi mahiri na si kulalama tu kutwa kucha.