EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
BARABARA ya Kilwa jijini Dar es Salaam itarudiwa kujengwa upya baada ya kubainika haina kiwango. Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya Kajima kutoka Japan iliyohusika katika ujenzi huo, imeomba radhi baada ya kubainika kuwa ndiyo yenye makosa na itaijenga upya kwa gharama zake. Pamoja na kampuni hiyo kuomba radhi Kampuni Mshauri wa mradi, Ingerosec ameondolewa. Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na Balozi wa Japan nchini, Hiroshi Nakagawa walitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Uamuzi huo unatokana na matokeo ya timu iliyoundwa kwa kushirikisha Shirika la Maendeleo la Japan (Jica), Kampuni ya Kajima, Ingerosec, Wakala wa Barabara (Tanroads) na wataalamu baada ya kuonekana kuwa barabara haina ubora. Timu hiyo iliyofanya kazi yake kwa takribani miezi mitatu, iliundwa baada ya kukutana na Balozi wa Japan. Serikali ya Japan ndiye mdhamini wa mradi huo wa ujenzi wa kilometa 10.1 za barabara hiyo iliyogharimu Sh bilioni 30. Wadau hao walikagua na kugundua kuwa barabara haikuwa katika kiwango. Walikaa wakakubaliana, Balozi ameleta barua, Kajima amekubali barabara itarudiwa upya, wameomba radhi, alisema Dk. Magufuli. Serikali imempa mkandarasi Kajima miezi miwili afanye upembuzi wa mradi na Oktoba 20, mwaka huu awasilishe taarifa ya maeneo yaliyolipuliwa kujengwa kabla ya kazi kuanza. http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=20906 |