Kiluvya vs Chanika

king90

JF-Expert Member
Apr 18, 2014
368
215
Wakuu habari ya muda huu, naombeni ushauri juu ya haya maeneo.nimepata viwanja viwili pande zote mbili vipo sawa kwa vipimo yani 30*40 na bei kote ni 6m cha kiluvya kipo kwa komba na chanika kipo mji mpya (kibaoni) naombeni ushauri wapi ni bora ukiangalia kuwa na maendeleo ya haraka.Natanguliza shukrani
 
Mkuu nimepata upande wa kushoto kama unaenda kibaha nadhani wanasema ni kisalawe

mkuu kiluvya yote haina shida kabisa, utakaa utafurahia. huduma zote muhimu zinapatikana kwa urahisi japo baadhi ya huduma kama bank tunazifuata mail moja ila sio mbali, kifupi utapapenda ila take care kama unakuja kuishi kwa malengo yako ni pazuri sana ila ukiwafuata vijana wa kiluvya ni kukaa vijiwen na kunywa pombe hadi kichefuchefu na hawana maendeleo kabisa, wageni ndio wanajitahidi kwa maendelea. nimeisha sana hapo napajua vizur
 
cheki access ya barabara za mitaa na umbali kutoka barabara kuu, cheki huduma za maji, umeme, shule, hospital kwa pande zote mbili, ila muhimu zaidi kuliko yote cheki ramani ya mipango miji kwa viwanja vyote viwili ujue matumizi ya hivyo viwanja kama yanaendana na lengo lako la kuvinunua.
 
Kila Mahali Pazuri
karibu Chanika Buyuni kwenye mradi viwanja vya kisasa kama europa ,...ila bei zimechangamka!
 
Chanika ina maji mengi chini ya ardhi. kama utachimba kisima kirefu au kifupi
Chanika ni mji nje ya Dsm unaokuwa kwa speed ya ajabu.
Huduma zote muhimu zinapatikana.
Mabomba ya gesi yanapita karibu, kama mipango ya kusambaza gesi majumbani itaanza, yatakuwa ni maeneo ya mwanzo kufaidika.

Karibu Chanika Town
 
Kiluvya ni zaidi mkuu. Kuna miradi mingi iko kule. NSSF wamepima viwanja zaidi ya 400. Tembelea website ya NSSF uone mradi wao wa "Kiluvya Hill" bei ilivyo kubwa (Tsh. 15000 kwa 1 sqm) mradi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili ( Mloganzila project) uko jirani na Kiluvya na umeshaanza, mradi wa Tanzania Building Agency (TBA), Chuo Kikuu cha Tumaini yote iko Kiluvya na mengine mengi. Kimbia haraka kuchukua kiwanja mzee
 
Wakuu habari ya muda huu, naombeni ushauri juu ya haya maeneo.nimepata viwanja viwili pande zote mbili vipo sawa kwa vipimo yani 30*40 na bei kote ni 6m cha kiluvya kipo kwa komba na chanika kipo mji mpya (kibaoni) naombeni ushauri wapi ni bora ukiangalia kuwa na maendeleo ya haraka.Natanguliza shukrani
Ulichukua wapi. Mrejesho?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom