Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

mfumo wa kukusanya kodi kutoka kwa watu wa kipato cha chini ni hatari sana kwani hugusa maisha yao ya kila siku na kipato chao na hawataweza kuvumilia hali hii kwani mizigo ya kodi imewalemea ni wakati wa kusema ccm tosha toka 2015
 
Hapo una deni la zamani, hizo fixed amount, umeme ulionunuwa ni huo 2,676.72 tu.

we dada unaishi Tz au? mimi pia nimenunua umeme wa sh 10,000 nimepata units 8.7, hakuna deni la zamani hapo. hiyo fixed amount huwa inakatwa (kama servise charge) kila mwanzo wa mwezi unaponunua umeme kwa mara ya kwanza. lililopo, fixed amount imepanda na price per unit imepanda pia.
fixed amount (service charge) + kodi inafika shs 6700 kwa sasa. ukilipa hiyo ndio unaanza kununua units za umeme
 
ulipata zile t shirt za bodaboda alizogawa makamba jr mwanza?
yaani mi.aisee naipenda ccm kweli mara t shirt mara kofia mara khanga mara viji hela!
Hakuna kama ccm!!
Nimepata mashaka na uraia wako, lazima nikulipue uhamiaji aisee!
 
Mafuta ya taa yalipopanda bei watu wa mjini mlikua kimyaaa..! Sasa zamu yenu. Mwaka mpya oyeeeeeee
 
Naona Service Charge imepanda kutoka 300 na sasa ni 6700.

Hizo unit nane ni umeme wa shilingi 3300.

Kiukweli hali ni mbaya maana kwangu kwa siku natumia UNIT 15. Inamaana naitaji shilingi 6500 kwa siku sawa na 195,000/= kwa Mwezi.

Nimegundua Pia na Bili ya Maji imepanda Unit zilezile nilikuwa nalipa kitu kama 17,000/ kwa Mwezi sasa ni 33,000/ kwa mwezi.

Nasubiri Bunge la Bajeti mwezi wa sita sijuhi wa saba hakika kila kitu kitakuwa JUUUUU.

Kifupi CCM Oyeeee
Chagua CCM kwa Maisha Bora(Mateso ya Kiuchumi) kwa Kila mtanzania hakika haya Maisha bora(Mateso ya Kiuchumi) hayabagui ni kwa kila mtu kwa aliye CCM na asiye CCM.

Tumethubu, Tumeweza na sasa Tunasonga Mbele.
 
Mijitu inaishi mjini kimagushi magumashi tu wewe baba mzima unanuaje umeme wa 10000? Si muache kwani umeme lazima?
 
pamoja na majigambo yote ya kuwa na gesi nyingi hapa nchini na iyo uranium lkn kwa mtanzania wa hali ya chini anazidi kuumizwa zaidi!
 
Mkuu nikushukuru kwa kuungana na mleta hoja, kwa hali ilivyo sasa mbadala lazima upatikane hata kwa lazima CCM. Chama Kikongwe kimechoka na kinapumua pumzi ya mwisho mwisho.
Chama gani ambacho kinachoweza kuwaunganisha watanzania ambacho ni mbadala wa CCM?
 
Mimi nilipata hivyo pia inamaana kuna makato ya mwezi uamepita kama 6000.wabongo walipigia debe sana tozo la simu wakayaka kugoma kutimia simu lakini hili la umeme nobody cares! Sisi tumerogwa

Sijalogwa kaka hii hatariii
 
CC: Nape Nnauye

Hivi ndugu Nape na MACCM wengine wote Mnajisikiaje? Au hata Bei ya Umeme hamijuhi mnaishi nyumba zile za Aprtment kodi kwa mwezi Dola 2000 ?

Hata kama ni hivyo.
Wazazi wenu je wanaishi huko kwenye Apartment pia?

Sawa kama na wazazi, wakwe zenu? Wajomba, babu, Bibi, shangazi au Ndugu yeyote hawa waambii kweli kuwa Maisha ni soo huku Uswahilini?
 
Last edited by a moderator:
Mijitu inaishi mjini kimagushi magumashi tu wewe baba mzima unanuaje umeme wa 10000? Si muache kwani umeme lazima?

Asante kwa Matusi lakini ukweli ni huo kuwa Maisha ni Magumu na Tunachopata leo kina liwa leoleo.

So nikipata La Kumi leo basi ndio nannunua umeme, Nikikosa mwendo wa Giza na Fanilia ipo kama kawa na Inadunda.

Sijuhi wewe ndugu yetu wakwenye Apartment unaijua bei ya Umeme?
 
we dada unaishi Tz au? mimi pia nimenunua umeme wa sh 10,000 nimepata units 8.7, hakuna deni la zamani hapo. hiyo fixed amount huwa inakatwa (kama servise charge) kila mwanzo wa mwezi unaponunua umeme kwa mara ya kwanza. lililopo, fixed amount imepanda na price per unit imepanda pia. fixed amount (service charge) + kodi inafika shs 6700 kwa sasa. ukilipa hiyo ndio unaanza kununua units za umeme
Huyu dada yetu hanunui huwa ananunuliwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom