Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Kwa Afrika,Karanga pori inalimwa Kenya,Malawi.Swaziland,Zimbabwe na Afrika ya Kusini.Karanga pori unaota kwenye eneo lolote la udongo na hali ya joto la kawaida kati ya 25c na 35c.Uzalishaji wa mimea inapendekezwa umbali kutoka usawa wa bahari mita 800.Hali ya hewa inachangia zaidi kuliko mwinuko kutoka usawa wa bahari katika kupata mazao bora.
Mvua katika maeneo yote ya uzalishaji kusini na mashariki ya Afrika,Mvua ni kati ya 800 na 1200mm kwa mwaka hivyo asilimia 70 zinanyesha katika kipindi cha kiangazi na ukame.Kumwagilia kunasaidia hasa kwa miti ile michanga ili kusaidia ikue haraka na kutoa mazao.
Aina nzuri ya karanga pori ni ile yenye uwezo wa kuzalisha tani 4 ya karanga kavu zenye maganda kwa hekta,mmea ukiwa umekomaa katika umri wa miaka chini ya 12 au juu kidogo.Aina bora ya karanga pori huanza kuzaa ukiwa na miaka mitatu au juu kidogo.
Mavuno hutegemea mbinu za uzalishaji na taratibu za maandalizi.Miti ikiwa na umri wa miaka 12-15 mazao huwa kilo 15-50 ya karanga kavu zenye ganda la ndani kwa mti.
Bei ya karanga pori ni dola za Marekani 2.1 kwa kilo kwa karanga zenye ganda la ndani.Wastani wa mazao kwa mti ni kilo 15 kama unachanganya karanga pori na mazao mengine inashauriwa kupanda miti 35 kwa ekari.
Kama huchanganyi na mazao mengine basi huoteshwa miti 270 kwa ekari ambapo pato lake hufikia hadi shilingi za kitanzania milioni 16 kwa mavuno.
Aina inayozalishwa kwa njia ya matawi huanza kuzaa ikiwa na umri wa miaka mitatu hadi minne,lakini mazao halisi hupatikana kati ya miaka 12 hadi 15.Mti wa mkaranga pori huishi kwa miaka 50.
Wadau wanaohitaji kufahamu kuhusu zao hili la macadamia
Wadau,
Kuna fursa kubwa kwenye kilimo cha matunda especially kwa nchi yetu ambayo ina ardhi nzuri na ambayo inafaa kwa mazao mengi.
Zao la Macadamia ni miongoni mwa mazao ya muda mrefu ambalo linaweza kubadirisha kilimo cha Tanzania, kwa sasa kuna mtaalamu ambaye ana kitalu cha miche ya macadamia (mche mmoja unauzwa shs 2,000) macadamia inaweza kustawi vizuri kwenye sehemu za baridi lakini siyo baridi sana hivyo kilolo, ifakara, morogoro, arusha, lushoto inaweza kustawi kwa uzuri zaidi.
Mimi nimechukua miche michache kwa ajiri ya kujaribu kwenye maeneo ya kisarawe.
WanaJF naomba mwenye uelewa wowote wa kilimo ch Macadamia anijuze. Najua kuwa ni zao ambalo bei yake ni nzuri kutosha. Mara ya mwisho nilizungumza na dada mmoja akaniambia kuwa kule Lushoto kuna watu wanalima hilo zao. hakuweza kunipa taarifa kwa kina cha kutosha.
Zao hili lipo Tanzania? Hali gani ya ardi inahitajika? Najua Kenya wanafanya export ya zaidi ya USD120m kwa mwaka.
Michango ya wadau
----Macadamia inatoa mbegu za mafuta kama ilivyo korosho. Hizo mbegu zinahitajika sana kwa watengenezaji wa chocolate vile vile unaweza kukamua mafuta na ubora wake ni sawa na mafuta ya mizeituni (olive oil). Bei ya Roasted and salted Macadamia Nuts kule Australia naona ni $18. Kule Kenya naona wanalamika utoroshwaji wa Macadamia kuja Tanzania kutayarishwa kwa kusafirisha nje.
Upekuzi zaidi unasema macadamia yanastawi sehemu ambazo avocado, mapapai, na ndizi hustawi. Wakulima wengi wa kenya wanang'oa kahawa ili kupanda macadamia.
View attachment 83425View attachment 83426View attachment 83427
Karanga pori,asili yake ni Australia.Mti wa karanga pori unatokana na jamii ya mimea ya proteaceae,aina zote zinalika ambayo mimea yote miwili ni Macadamia intergrifolia na Macadamia tetraphllya mchanganyiko wa mbegu zote mbili bado unafaa kama zao la kilimo la biashara.

Nawasilisha