daraja la kigamboni
JF-Expert Member
- Apr 28, 2016
- 2,504
- 2,204
Sasa mwenye Akili ya matope hapo ni naniWenye akili za matope kama nyinyi hamuwezi kukosekana.
Mwandiko wenyewe kama wa mume wa zamaradi
Sasa mwenye Akili ya matope hapo ni naniWenye akili za matope kama nyinyi hamuwezi kukosekana.
Mwandiko wenyewe kama wa mume wa zamaradi
Nilisema hapaHakikisha na yeye hajakudanganya.
Sio tunasumbua watu kumbe mtoto hataki shule ama alifeli.
OFISI YA RAISAkaniambia amemaliza Form Four, Ana Division One ya 10, Nikamuuliza Kwanini hujaenda shule, Akasema shule aliyopangiwa wameuza jina lake, Alipoenda kuripoti aliambiwa nafasi yake haipo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo hayuko siriaz umeshaambiwa Baba yake ni maskini sana na mama yake ni mgonjwa unadhani kwa umri huo angeenda wapi kulalamika?Mtu nafasi yake inauzwa afu anaenda kuwa hausigel,hayuko serious huyo
Hataki shule
Kwa hiyo bado unamini dogo kadhulumiwa haki yake?Siyo hayuko siriaz umeshaambiwa Baba yake ni maskini sana na mama yake ni mgonjwa unadhani kwa umri huo angeenda wapi kulalamika?
Hii nchi kila mahali ili jambo lisogee ushikwe mkono au uwe na kitu mkononi sasa hivyo vyote hakuwa navyo angetoboa vipi?ila nichukue nafasi hii kumpongeza mama Gwajima anajitahidi sana kuwa active kwa mambo ya msingi ya kijamii (of course huko ccm naona wote wapiga debe na kujipendekeza lakini huyu mama kiasi anaujua wajibu wake ipasavyo)
Alafu badaye huyo aliyeuziwa jinaMichezo hii ilikuwepo sana zamani...hadi waziri mmoja alishafanya na alishajitetea sana hapa ...
Mtoto huyu anahitaji msaada zaidi ya huo wa kurudishwa shule maana anatokea familia masikini sana..
nimeona taarifa sehemu flani huyu inaedaiwa kudhurumiwa kapata 0 namba yake ni 135 na sio 136 na mama aliye taka msaidia kaishia kumpa vitabu na sare za shule muhusika aliye pata 1Kwa hiyo bado unamini dogo kadhulumiwa haki yake?
Mkuu mimi nime-comment kutokana na nilichokisoma main post sikuendelea na uzi sasa kama kuna mabadiliko uliyaona huko mbele mimi hayo sikuyaona.Kwa hiyo bado unamini dogo kadhulumiwa haki yake?
Kaongo, kametwanga ZEROMtu nafasi yake inauzwa afu anaenda kuwa hausigel,hayuko serious huyo
Hataki shule
Haya sasa taarifa ya Tamisemi umeisikia? Huyo mwanafunzi ni mwongo alidanganya wazazi wake na umma kwenye matokeo kala buyu. Wadanganyika ni rahisi tu kuwashikia akiliWenye akili za matope kama nyinyi hamuwezi kukosekana.
Mwandiko wenyewe kama wa mume wa zamaradi
Mh Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda okoa mstakabali wa maisha ya binti huyu.
"Kaka Yericko pole na Majukumu, Naomba kaka nisaidie, mtoto huyu kwenye picha anaitwa SIFIKA DANIELY RUBEN, naomba apate Haki zake, Ipo hivi kaka, Nilikuwa natafuta binti wa kazi za ndani, Nikapata binti kutoka Hedaru, alipofika nikamuhoji ili kujua ametoka wapi hasa, na familia yake ipoje.
Akaniambia amemaliza Form Four, Ana Division One ya 10, Nikamuuliza Kwanini hujaenda shule, Akasema shule aliyopangiwa wameuza jina lake, Alipoenda kuripoti aliambiwa nafasi yake haipo. Nimeumia Kiukweli naomba nisaidie kwa wahusika binti apate haki yake, Mimi sina kipato kikubwa lakini kwa shule ya serikali nitamsomesha, lakini anapataje haki yake maana mimi kumpeleka shule binafsi uwezo sina.
Shule aliyomalizia Form Four ni MKOMBOZI SECONDARY SCHOOL ipo Hedaru Wilaya Ya Same. Shule aliyopangiwa aripoti Form Five Inaitwa NAMWAI HIGH SCHOOL Ipo Mkoa wa Kilimanjaro Sanya Juu,
Na Mchepuo aliopangiwa ni PCM
Namba yake ya Mtihani ni S.P. 0708/0136
Naomba Nisaidie Huyu Mtoto apate haki Yake Arudi shule Mimi nilitaka mfanyakazi ndo nimeletewa Huyo na Moyo wangu Umekosa Amani Nafasi yake Imeuzwa Kisa Alichelewa Kurepoti shule Wazazi wake Hawana Msaada Tena Maana Baba yake ni masini kabisa, na Mama Yake mzazi kwa sasa ni Mgojwa. Naomba Nisaidie apate hake yake Mimi Nitamsomesha Kwa hikihili kipato changu kidogo Nilichojaliwa".
Nimeitoa kwa Yericko Nyerere
View attachment 2761440View attachment 2761442
=====
UPDATES;
======
Napenda kutoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto, Mh Doroth Gwajima kwa kuchukua hatua kwa haraka baada ya taarifa ya binti anayehitaji msaada wa kuendelea na masomo kitato cha tano baada ya mgogoro wa nafasi yake na shule aliyochaguliwa kujiunga.
Pia nimshukuru Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda ambae amechukua jukumu la kuwasiliana nami, na kuahidi kuwa Wizara imelichukua na ufumbuzi utapatikana haraka iwezekanavyo.
Lakini niwashukuru wadau kwa mamna mlivyolipokea na Wengine wameguswa hadi kufikia hatua ya kuwa tayari kumsomesha binti huyu kwa namna wawezavyo. Ni hatua muhimu sana ya kizalendo na ya kusaidiana kama Watanzania.
Kwasasa suala hili liko chini y Wizara hizi mbili, Tuziache zishughulikie na kutafuta ukweli wa mgogoro huu, na Haki ya mabinti hawa wawili (aliyechukua nafasi ya SIFIKA DANIEL RUBEN, na SIFIKA mwenyewe) wapate haki yao ya msingi ya kupata elimu bila kujalisha nani alifaulu au hakufaulu.
Lakini pia Viongozi wa Shule za Mkombozi Secondary na Namwai High School, Viongozi wa Elimu Wilaya na Mkoa, toeni ushirikiani kwa mamlaka bila kujalisha nyinyi ni walalamikiwa wa jambo hili. Muhimu zaidi ni mabinti hawa wapate elimu zao.
Na Yericko Nyerere.
Pia soma: Taarifa kutoka shule ya Sekondari Mkombozi alikosoma Sifika Danieli Rubeni.