Kilimanjaro: Naomba tumsaidie Mwanafunzi Sifika Daniely Ruben apate haki yake na arudi shule

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,552
Mh Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda okoa mstakabali wa maisha ya binti huyu.

"Kaka Yericko pole na Majukumu, Naomba kaka nisaidie, mtoto huyu kwenye picha anaitwa SIFIKA DANIELY RUBEN, naomba apate Haki zake, Ipo hivi kaka, Nilikuwa natafuta binti wa kazi za ndani, Nikapata binti kutoka Hedaru, alipofika nikamuhoji ili kujua ametoka wapi hasa, na familia yake ipoje.

Akaniambia amemaliza Form Four, Ana Division One ya 10, Nikamuuliza Kwanini hujaenda shule, Akasema shule aliyopangiwa wameuza jina lake, Alipoenda kuripoti aliambiwa nafasi yake haipo. Nimeumia Kiukweli naomba nisaidie kwa wahusika binti apate haki yake, Mimi sina kipato kikubwa lakini kwa shule ya serikali nitamsomesha, lakini anapataje haki yake maana mimi kumpeleka shule binafsi uwezo sina.

Shule aliyomalizia Form Four ni MKOMBOZI SECONDARY SCHOOL ipo Hedaru Wilaya Ya Same. Shule aliyopangiwa aripoti Form Five Inaitwa NAMWAI HIGH SCHOOL Ipo Mkoa wa Kilimanjaro Sanya Juu,
Na Mchepuo aliopangiwa ni PCM
Namba yake ya Mtihani ni S.P. 0708/0136

Naomba Nisaidie Huyu Mtoto apate haki Yake Arudi shule Mimi nilitaka mfanyakazi ndo nimeletewa Huyo na Moyo wangu Umekosa Amani Nafasi yake Imeuzwa Kisa Alichelewa Kurepoti shule Wazazi wake Hawana Msaada Tena Maana Baba yake ni masini kabisa, na Mama Yake mzazi kwa sasa ni Mgojwa. Naomba Nisaidie apate hake yake Mimi Nitamsomesha Kwa hikihili kipato changu kidogo Nilichojaliwa".

Nimeitoa kwa Yericko Nyerere

FB_IMG_1695621523561.jpg
FB_IMG_1695621639161.jpg

=====

UPDATES;

======
Napenda kutoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto, Mh Doroth Gwajima kwa kuchukua hatua kwa haraka baada ya taarifa ya binti anayehitaji msaada wa kuendelea na masomo kitato cha tano baada ya mgogoro wa nafasi yake na shule aliyochaguliwa kujiunga.

Pia nimshukuru Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda ambae amechukua jukumu la kuwasiliana nami, na kuahidi kuwa Wizara imelichukua na ufumbuzi utapatikana haraka iwezekanavyo.

Lakini niwashukuru wadau kwa mamna mlivyolipokea na Wengine wameguswa hadi kufikia hatua ya kuwa tayari kumsomesha binti huyu kwa namna wawezavyo. Ni hatua muhimu sana ya kizalendo na ya kusaidiana kama Watanzania.

Kwasasa suala hili liko chini y Wizara hizi mbili, Tuziache zishughulikie na kutafuta ukweli wa mgogoro huu, na Haki ya mabinti hawa wawili (aliyechukua nafasi ya SIFIKA DANIEL RUBEN, na SIFIKA mwenyewe) wapate haki yao ya msingi ya kupata elimu bila kujalisha nani alifaulu au hakufaulu.

Lakini pia Viongozi wa Shule za Mkombozi Secondary na Namwai High School, Viongozi wa Elimu Wilaya na Mkoa, toeni ushirikiani kwa mamlaka bila kujalisha nyinyi ni walalamikiwa wa jambo hili. Muhimu zaidi ni mabinti hawa wapate elimu zao.

Na Yericko Nyerere.

Pia soma:
Taarifa kutoka shule ya Sekondari Mkombozi alikosoma Sifika Danieli Rubeni.
 
Hapa kumsaidia nenda naye shule wakujibu Kwa maandishi Kwa nn wasimpokee huyo mtoto.

Ukifanya masihara kesi inakubadilikia kukaa na binti ambaye anatakiwa akaripoti shule.

Mtego mwingine ni muda wa kuripoti ukiisha nafasi atapewa huyo na uzembe utaonekana n wa mtoto na wazaz
 
Mh Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda okoa mstakabali wa maisha ya binti huyu.

"Kaka Yericko pole na Majukumu, Naomba kaka nisaidie, mtoto huyu kwenye picha anaitwa SIFIKA DANIELY RUBEN, naomba apate Haki zake, Ipo hivi kaka, Nilikuwa natafuta binti wa kazi za ndani, Nikapata binti kutoka Hedaru, alipofika nikamuhoji ili kujua ametoka wapi hasa, na familia yake ipoje.

Akaniambia amemaliza Form Four, Ana Division One ya 10, Nikamuuliza Kwanini hujaenda shule, Akasema shule aliyopangiwa wameuza jina lake, Alipoenda kuripoti aliambiwa nafasi yake haipo. Nimeumia Kiukweli naomba nisaidie kwa wahusika binti apate haki yake, Mimi sina kipato kikubwa lakini kwa shule ya serikali nitamsomesha, lakini anapataje haki yake maana mimi kumpeleka shule binafsi uwezo sina.

Shule aliyomalizia Form Four ni MKOMBOZI SECONDARY SCHOOL ipo Hedaru Wilaya Ya Same. Shule aliyopangiwa aripoti Form Five Inaitwa NAMWAI HIGH SCHOOL Ipo Mkoa wa Kilimanjaro Sanya Juu,
Na Mchepuo aliopangiwa ni PCM
Namba yake ya Mtihani ni S.P. 0708/0136

Naomba Nisaidie Huyu Mtoto apate haki Yake Arudi shule Mimi nilitaka mfanyakazi ndo nimeletewa Huyo na Moyo wangu Umekosa Amani Nafasi yake Imeuzwa Kisa Alichelewa Kurepoti shule Wazazi wake Hawana Msaada Tena Maana Baba yake ni masini kabisa, na Mama Yake mzazi kwa sasa ni Mgojwa. Naomba Nisaidie apate hake yake Mimi Nitamsomesha Kwa hikihili kipato changu kidogo Nilichojaliwa".

Nimeitoa kwa Yericko Nyerere

View attachment 2761440View attachment 2761442
Maelezo mengiiii lkn kifupi hamna mwanafunzi anayehitaji msaada hapo na huyo aliyempokea pia hana uwezo wa kureason. Zama hizi hicho kitu hakipo kwa mifumo iliyopo HAIWEZEKANIKI hlf mtoto asome afaulu kwa hhsyo matokeo ndo akimbilie kwenye uhausigeli yaaani amekosa kaakili kabisa kawapi pa kupeleka tatizo lake mpaka aamue kukimbilia huko? Basi huo ufaulu aliopata ni non sense na elimu hiyo haina maana kwake.
 
Bosi la DP world ni Mikopo mitupu tena na ile kausha damu, usishangae huyo mtoto akipewa nafasi huyo Boss wa DPW akaja tena kupitisha bakuri humu na kumfanya huyo binti kitega uchumi na fursa zinginezo
Mkuu umesoma vyema au umekurupuka?
 
Kupitia ujinga kama huu ndio tunaishia kuwa na viongozi mithili ya Mzee wa Tozo na Bashite.

Jitu lina foundation mbovu ya elimu, linanunuliwa jina na matokeo halafu linakuja kufanya upumbavu kwa nchi nzima.

Hao wahusika kuanzia muuzaji mpaka mnunuzi wote wafungwe angalau miaka 10 jela.
 
Back
Top Bottom