Kimbweka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2009
- 8,597
- 1,683
Hii imenitokea kipindi fulani nilipotembelea mbuga ya wanyama hifadhi ya taifa ya Ngorongoro. Katika sehemu ya kuingilia ambapo clearance zote hufanyika kuna sehemu upande wa kulia ambapo ni pa kujisaidia na kujiweka sawa kabla ya kuingia ndani ya hifadhi hiyo. Kilicho nishangaza zaidi katika sehemu ya msalani matangazo yote yamebandikwa na kusomeka kwa lugha ya kiswahili tu. Hasa yahusuyo usafi wa vyoo na matumizi ya maji kwa sehemu hiyo. Hii ilinishangaza kwa kuwa wanaoenda kutembelea huko kwa asilimia kubwa ni watu (wageni) wanaotoka nchi za nje km vile Amerika, Ulaya na Asia. Sasa Hawa wote hawajui lugha ya kiswahili na kama wanajua ni wachache mno! Hii inamaanisha waswahili ndio wachafuzi sanaaa wa msalani au imekaaje? Kwa kweli nilimaliza utalii wangu na kondoka bila kupata jibu" KWA NINI MATANGAZO HAYO YA MSALANI YAWE KTK LUGHA YA KISWAHILI TU? "