Baadhi ya vijana kutokea Ngorongoro wadai uwepo wa ukiukwaji wa haki za binadamu

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU KATIKA
WILAYAYA NGORONGORO;

UTANGULIZI

Ndugu Watanzania wenzangu sisi ni wakazi wenyeji wa Tarafa ya Ngorongoro iliyopo ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika wilaya ya Ngorongoro. Aidha mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni hifadhi mseto ambapo hujumuisha uhifadhi na uwepo wabinadamu.

Majukumu ya NCAA ni Pamoja na uhifadhi, utalii na kuendeleza jamii (ustawi wa jamii). Jukumu la kuendeleza jamii inayoishi ndani ya tarafa ya Ngorongoro ni kuwapatia huduma za maendeleo miradi ya maendeleo kama vile elimu,afya , maji , miundombinu ya barabara N.Khaya yanabainishwa na sheria iliyoanzisha hifadhi ya Ngorongoro yamwaka1959 sura
namba 284.

Aidha tangu Rais samia aingie madarakani na serikali yake Ianzishe zoezi la kuhamisha watu kuwapeleka katika eneo la msomera fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo yaliyokuwa katika akaunti za shule za misingi,sekondari , vituo vya kutolea huduma za afya , miradi ya maji , miradi ya ujenzi na ukarabati wa ofisi za serikali za vijiji yote yalihamishwa na kuepelekwa katika halmashauri ya handenimkoani Tanga.

Jumla ya shilingi billioni mbili na million sitini na moja (2,061,000,000Tsh) yalihamishiwa halmashauri ya wilaya ya handeni , ambapo 820,0000,000/= ya miradi ya Afya, 611,000,000/= ya miradi ya maji, 630,000,000/= ya miradi ya elimu.Kwa makusudi serikali ilianzisha uhamisho huu kwa kile walichokisema ni wa hiari na wala si wa mabavu.

Wananchi wanaoendelea kuishi Ngorongoro wamewekewa vikwazo vya maendeleo.Mara kadhaa,wamekuwa wakifanya mikutano na kuomba serikali kuwapatia vibali ili wakarabati majengo yaliyoharibika na ambayo yanahatarisha usalama wa wanafunzi mashuleni, kuhatarisha afya ya wagonjwa hasa wakina mama wanaojifungua katika vituo vya kutolewa huduma za afya uwezekano wa milipuko ya magonjwa kutokana na kukosekana kwa vyoo katika shule za msingi na sekondari baada ya yaliyokuwepo kujaa.

wananchi waliendelea kuomba kusikilizwa kulingana na madai ya kuomba kupatiwa vibali kwa ajili ya miradi ya maendeleo na ambazo wangejenga kwa gharama ya michango yao wenyewe.

Hata hivyo,bado serikali haijawahi kwenda kuwasikiliza na kutatua changamoto
zao.Tumeendelea kuona waandishi wa Habari wanaingia kwenye maeneo yetuna kuendelea kufanya propaganda dhidi ya uhalali wa watu wetu kuendelea kuwepo katika makazi yao.

Aidha,serikali inaingia madarakani kuwajibika kwa ajili ya wananchi wake na kuendeleza ustawi wao na hili ni takwa la kikatiba( haki ya kupatiwa huduma za kijamii).

Ndugu waandishi wa Habari, tumeona propaganda zikifanywa dhidi ya Maisha ya jamii inayoishi loliondo na Ngorongoro na kwa ajili ya kuhalalisha uporaji /utwaaji wa ardhi yao kwa lengo la kuyapa wawekezajikutokanje.

Katika Tarafa ya Ngorongoro siku za hivi karibuni wananchi wa endulen waliandamana kuanzia tarehe 31 julaihadi 11 agosti 2023,wakiandamana kila siku kuombausikilizwaji juu ya madai yao, hata hivyo hawakusikilizwa.

Ndugu waandishi wa Habari,mnamo tarehe 10Agosti2023 Mbunge wa jimbo la Ngorongoro alifika Kijiji cha endulen kuwasikiliza na kuwatuliza wananchihao, na Kimsingi waliazimia kuunda kamati ndogo ya watu 14 watakaokwenda kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kuomba vibali kwaajili ya ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi ndian ambazo yalikua na nyufa kubwa na kupelekea wananchi kuhofia usalama wa watoto wao. Sambamba na hilo, mnamo tarehe 15 mwezi huu wa nane katika mnada wa endulen ilitokea vurugu majira ya jioni,baina ya vijana waliokuwa na watu wanaodaiwa ni waandishi wa habari.

Baada ya vurugu hizo jioni hiyo hiyo magari yajeshi lapolisi na maskari wa Wanyama pori katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro walifika mnadani na madukani katika Kata ya endulen wakiwasaka na kukamata vijana na wazee waliokutananao mahala popote walipowakuta.Ukamataji huo holela uliendelea hadi leo ambapo wanaume wote wamekua wakiishi porini kwa siku nne sasa kwa kuhofia kukamatwa bila kosa.

Toka operesheni hii ianze watu zaidi ya 35 wamekamatwa na kupelekwa vituo vya polisi karatu, manyara kibaoni wilayani karatu na wengine kusikojulikana.

Kamata kamata hii imekua haifuati sheria kwakua wanakamata mpaka wazee na Watoto wa kiume wanaochunga mifugo na wagonjwa wazee ambao kimsingi hawakuhusika kwenye vurugu kulingana na maelezo ya mkalimani na mwandishi wa Habari.

Ndugu waandishi wa habari tukio hili limesababisha taharuki kubwa sana kwenye jamii nzima kwakua utaratibu unaotumika hauzingatii sheria na haki za binadamu.

Ndugu waandishi wa Habari,Mnamo tarehe 19agosti2023majira ya saa moja usiku magari sabayenye askari wa jeshi la polisi na askari wa Wanyama pori wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,walifika nyumbani kwa mbunge wa jimbo la Ngorongoro mhe Emanuel oleshangay na kutishia kukamata familia yake[mke wake]kwa kurusha risasi hovyo na
kupelekea mama yake mzazi wa mbunge kupoteza fahamu , usiku huo huo saa tisa kitendo hicho kilirudiwa na kundi hilo la askari mchanganyiko wa jeshi la polisi na rangers.

Mapendekezo

1.Kusimamishwaopereshenihiyo[kuondoa askari wa wanyamapori na polisikatika
makazi ya watu

2.Wananchi waliokamatwa tayari wafikishwe mahakamani kwani wameshikiliwa kwa zaidi ya saa 48 na wengine hawafahamiki walipo hadi sasa, hivyo ni vyema jamii ifahamishwe walipo ndugu zao waweze kupata msaada wa kisheria na mahitaji kutoka kwa ndugu na familia zao.

3.Kutokumtishia au kumdhuru mbunge Pamoja na familia yake kwa vyovyote vile.

4.Kuendesha zoezi la uhamaji kwa hiari kwenda msomera kwa uhuru, uwazi, uhiari wa kweli na bila ya propaganda au kuwanyima haki za wale wanaoendelea kubaki au wale ambao hawajawiwa kujiandikisha kuondoka.

5.Kurejesha huduma za maendeleo kwa watanzania waishio Ngorongoro ambao
kimsingi ni haki yao kupatiwa kama walivyo watanzania wengine nchini, ikiwa ni pamoja na kutoa vibali vya ujenzi wa madarasa, vyoo na ukarabati wa vituo vya
kutolea huduma za Afya.

6.Uwekezaji wowote unaofanyika katika maeneo ya wananchi isiwe sababu ya
kuwaondoa watu katika maeneo yao au kuondosha haki za wananchi wa eneo husika bali ni iwe wenye kuendeleza ustawi wao na vizazi vyao.

7.Kwa watu wote waliokamatwa na walioendelea kukamatwa wasifanyiwe vitisho, kuteswa ili kuwashawishi walazimike kukubali kuhamishwa katika maeneo yao kwani inaondoa uhiari wao wenyewe na kuhalalisha uhiari wa mabavu.

8.Kwa tamasha/mikutano yeyote yatakayoratibiwa kwa kuhusisha wamasai wa nje ya Ngorongoro na loliondo, au kutoka maeneo mengine kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono unyakuaji wa maeneo ya wakazi wa loliondo na Ngorongoro ifahamike wazi kuwa si wa hiari wa watu wetu na kwamba tunapinga kuondolewa au kumegwa kwa maeneo yetu kwa ajili yawawekezaji wa mataifa mengine.

HITIMISHO

Ndugu waandishi wa habari, watanzania wote, sisi ni wenyeji wazawa wa Ngorongoro na ni watanzania wa kuzaliwa na siyo wakujiandikisha au kuomba, Haki ya kuishi, kupatiwa huduma za kijamii ni haki yetu kikatiba kama walivyo watanzania wengine, tunastahilihaki zoteza msingi kama raia wengine wa Tanzania. Ustawi wetu usiangamizwe sababu ya aina ya rasilimali tulioyatunza kwa miongo na hata karne wakati wote.

HAKI HUINUA TAIFA,BALI DHAMBI NI ADUI KWA WATU WOTE -(Methali 14:34)

- Tamko limesomwa na Kisota Mollel, Melobo Ndara Poshe na Ezekiel Olemangi

Tarehe 21/8/2023
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU KATIKA
WILAYAYA NGORONGORO;

UTANGULIZI

Ndugu Watanzania wenzangu sisi ni wakazi wenyeji wa Tarafa ya Ngorongoro iliyopo ndani ya mamlaka ya hifadhi ya

Tarehe 21/8/2023
TEC ndiye mtetezi wetu kwa Sasa nchi hii
 
Swala la bandari limetonesha na hiki kidonda cha ngorongoro, kuna watu wako fasta kutaka kutajirika kwenye rasilimali za watanganyika.
 
Njia sahihi ya kupata haki wakati mwingine uwa sio rahisi.. ina vikwazo na maumivu mengi.
 
Mama sio msikivu na kuna wajanja wachache wana mframe na kajaa. CCM ninayo ijua mm tukutane 2025
 
Mama sio msikivu na kuna wajanja wachache wana mframe na kajaa. CCM ninayo ijua mm tukutane 2025
Kashasema amesikia kila kitu bali ameamua kukaa kimya na akaendelea kusema kwamba hakuna mtu mwenye Misuli na mabavu kuiuza nchi, kuigawa nchi, kufuruga amani na kadhalika
 
Swala la bandari limetonesha na hiki kidonda cha ngorongoro, kuna watu wako fasta kutaka kutajirika kwenye rasilimali za watanganyika.
Na wapiga debe ni walewale akina kitenge na wengine ambao hata kwenye hili la dpw ndio vinara wa kupayuka
 
Na wapiga debe ni walewale akina kitenge na wengine ambao hata kwenye hili la dpw ndio vinara wa kupayuka
Kitenge hata kule ngorongoro alikuwa kimbelembele, ni wazi hawa watu wanalipwa kufanya propaganda kwa maslahi ya mwarabu halafu wanataka kila mtu aunge mkono madili yao.
 
Back
Top Bottom