Kilichonishangaza Ngorongoro entrance point

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Hii imenitokea kipindi fulani nilipotembelea mbuga ya wanyama hifadhi ya taifa ya Ngorongoro. Katika sehemu ya kuingilia ambapo clearance zote hufanyika kuna sehemu upande wa kulia ambapo ni pa kujisaidia na kujiweka sawa kabla ya kuingia ndani ya hifadhi hiyo. Kilicho nishangaza zaidi katika sehemu ya msalani matangazo yote yamebandikwa na kusomeka kwa lugha ya kiswahili tu. Hasa yahusuyo usafi wa vyoo na matumizi ya maji kwa sehemu hiyo. Hii ilinishangaza kwa kuwa wanaoenda kutembelea huko kwa asilimia kubwa ni watu (wageni) wanaotoka nchi za nje km vile Amerika, Ulaya na Asia. Sasa Hawa wote hawajui lugha ya kiswahili na kama wanajua ni wachache mno! Hii inamaanisha waswahili ndio wachafuzi sanaaa wa msalani au imekaaje? Kwa kweli nilimaliza utalii wangu na kondoka bila kupata jibu" KWA NINI MATANGAZO HAYO YA MSALANI YAWE KTK LUGHA YA KISWAHILI TU? "
 
mhh naona hauko sahihi nenda nchi za wenzetu ambao hawaongei kiingereza wao kila kitu kinaandikwa kwa lugha yao,wanajivunia lugha yao na sisi pia tunajivunia ya kwetu,mbuga ni ya kwetu tunaienzi kwa lugha yetu,tunadumisha utamaduni wetu,mgeni anapaswa kujifunza lugha yetu.saa wewe unataka tuandike kiingereza kwani mbuga ni ya kwaoooo???? sifia chako acha kuwa mtumwa wa lugha za wengine.
 
jamani huu ni uzalendo...mbona ukienda ufaransa kila kitu kimeandikwa kifrench?.....ndio hadi chooni.
 
mhh naona hauko sahihi nenda nchi za wenzetu ambao hawaongei kiingereza wao kila kitu kinaandikwa kwa lugha yao,wanajivunia lugha yao na sisi pia tunajivunia ya kwetu,mbuga ni ya kwetu tunaienzi kwa lugha yetu,tunadumisha utamaduni wetu,mgeni anapaswa kujifunza lugha yetu.saa wewe unataka tuandike kiingereza kwani mbuga ni ya kwaoooo???? sifia chako acha kuwa mtumwa wa lugha za wengine.

Kwanini sehemu nyingine tofauti na pale kwa mfano kwenye mahotel ya serena, wild life, kila kitu kimeandikwa kwa kiingereza na baadhi ya lugha nyingine isipokuwa kiswahili. Lakini pale entrance pointi msalani waandike kiswahili peke yake? kwanini wasiandike na kiingereza? ama kule mahotelini kwa nini wasiandike kiswahili pia? That's my major concern guys!!!
 
Unajua wengi tunakimbilia kusema uzalendo wakati uzalendo wenyewe hatuujui maana yake ila tunakuwa bendera fuata upepo
 
kunasababu nyingi ambazo zinaweza kuwasababu: 1. Siyo kweli kwamba waopita wengi wao ni wazungu..kuna watanzania wasio pungua 300 hupita hapo kila siku, sasa ukichukua waingereza + wafaransa -wajerumani+ waitaliano nk hawawezi kuwafikia idadi ya waswahili
2. wazungu wengi huwa na maguide hivyo hupata maelekezo kutoka kwao,
3. Ni lugha yetu ya taifa
4. .......
 
4. Kwa nini iwe choooni tu na siyo mahotelini?
5. Lugha yetu ilianzia chooniii ama?
 
Kwanini sehemu nyingine tofauti na pale kwa mfano kwenye mahotel ya serena, wild life, kila kitu kimeandikwa kwa kiingereza na baadhi ya lugha nyingine isipokuwa kiswahili. Lakini pale entrance pointi msalani waandike kiswahili peke yake? kwanini wasiandike na kiingereza? ama kule mahotelini kwa nini wasiandike kiswahili pia? That's my major concern guys!!!

Kuna watanzania wangapi wanafika kwenye hotels/lodges zenye level ya serena...na ukiona wanafika hapo ujue kimombo kina panda...teh teh
 
Kuna watanzania wangapi wanafika kwenye hotels/lodges zenye level ya serena...na ukiona wanafika hapo ujue kimombo kina panda...teh teh

Ni wengi sana kwenye group yetu tulikuwa 50, toa wale tuliokutana nao pale
 
4. Kwa nini iwe choooni tu na siyo mahotelini?
5. Lugha yetu ilianzia chooniii ama?
naomba tuanzie hapa: niambie vyoo hivyo watumiaji wakubwa ni Watanzania, waingereza, Wafaransa, wahispania....vinginevyo unajibu lako unalolitaka
 
Waafrika ndio tunaofanya wazungu watuone tu manyani
hii imenitokea kipindi fulani nilipotembelea mbuga ya wanyama hifadhi ya taifa ya ngorongoro. Katika sehemu ya kuingilia ambapo clearance zote hufanyika kuna sehemu upande wa kulia ambapo ni pa kujisaidia na kujiweka sawa kabla ya kuingia ndani ya hifadhi hiyo. Kilicho nishangaza zaidi katika sehemu ya msalani matangazo yote yamebandikwa na kusomeka kwa lugha ya kiswahili tu. Hasa yahusuyo usafi wa vyoo na matumizi ya maji kwa sehemu hiyo. Hii ilinishangaza kwa kuwa wanaoenda kutembelea huko kwa asilimia kubwa ni watu (wageni) wanaotoka nchi za nje km vile amerika, ulaya na asia. Sasa hawa wote hawajui lugha ya kiswahili na kama wanajua ni wachache mno! Hii inamaanisha waswahili ndio wachafuzi sanaaa wa msalani au imekaaje? Kwa kweli nilimaliza utalii wangu na kondoka bila kupata jibu" kwa nini matangazo hayo ya msalani yawe ktk lugha ya kiswahili tu? "
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom