El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 263
- 502
Wakati wa siasa za mwanzo wa vyama vingi na kabla kidogo ya kuanza mfumo wa vyama vingi awamu ya pili, James Mbatia alionekana kuwa mwanasiasa shupavu na kama ungemuona miaka hiyo, siasa zake zilikuwa na mwelekeo na zenye mguso.
Ndo maana katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 James Mbatia alishinda Kwa kishindo nafasi ya ubunge wa Jimbo la vunjo kirahisi sana na baadae alikuwa mmoja wa wabunge ambao ungependa kuwasikiliza kwa hoja zao na kusimamia mambo ya msingi.
Baada ya muda na hasa baada ya kuwa mwenyekiti wa Nccr mageuzi ,umaarufu wake uliporomoka ghafla na akakosa ushawishi alokuwa nao mwanzoni.
Nataka kuamini kwamba nafasi ya uenyekiti aliyoipata ilimfanya atake kujenga zaidi hadhi (status quo) na akasahau kuendeleza siasa za masuala (issues).
Mbatia alisahau kwamba yeye alikuwa mpinzani na akataka kujifananisha na watawala. Alianza kutaka kusifiwa kama kiongozi msitaarabu . Na kweli ikawa hivyo, maana ungesikia kweli watawala wakimsifia sana.
Na kwa Sababu alitaka kuwa na hadhi baridi (relevance) siyo tu kwamba uwezo wake wa kisiasa wa ndani yake ulishuka, bali alijikuta akipoteza pia akipoteza mguso Kwa wananchi.
Wananchi hupenda kusemewa na kukuona huyumbi katika kusema masuala muhimu yanayowahusu wakati huo.
James Mbatia badala ya kuwa na makali ya kisiasa kama alivyokuwa, baadae akaanza kuwapinga wapinzani wenzake waziwazi huku akitafuta kuonekana hana shida na watawala. Na kwa kuwa asili ya upinzani ni harakati (activism) na kusimamia hoja za wakati, Mbatia alishuka kabisa ngazi aliyokuwa amekwea kisiasa na ghafla akaanza kupuuzwa na watu wake ndani ya Chama bila yeye kutambua hilo mapema.
Matokeo tunayoyaona sasa ya yeye kupingwa chamani yanatokana na ukweli kwamba,
James Mbatia amepoa sana kisiasa (no longer politically and ideologically active) hali inayofanya akose mashiko ( impact) chamani na katika siasa za upinzani kwa ujumla.
Mbatia havutii tena kuwa kiongozi mpinzani ukiachia kuongoza chama Cha upinzani chenye uhai( active).
Mbatia aliye kuwa na hoja zenye mashiko, hivi sasa kabaki tu na sentensi yake ya " mama Tanzania".
Mahali pa kukasirikia maovu utamsikia akiweka neno " mama Tanzania".
Mahala pa kuungana na wapinzani wenzake Ili wailete serikali mezani kuongea, utamuona akiwaruka wenzake na lugha ya " kwa maslahi ya mama Tanzania".
Kinachomkumba sasa ni Kwa Sababu aliacha wito wake wa kuwa mpinzani halisi na kuanza kulinda hadhi tu. Kwa maama hiyo hana ushawishi (Influence).
Katika dhana ya kuongoza kupoteza ushawishi (Influence) ni kupotea uongozi moja kwa Moja.
The real leadership is all about influence.
Na kwa kuwa Sasa Yuko wastani (mediocre) namshauri awapishe watu wenye wivu( zeal) ya kisiasa na ambao Wanamoto wa kisiasa ili kuifanya Nccr great again.
Kutafuta kukubalika (Approval) na watawala au labda na kikundi Cha watu fulani na kusahau wito wa asili wa upinzani ndo chanzo cha kuporomoka kwa Mbatia
Nashauri asitaafu siasa.