Kile unachoandika mtandaoni kinasadifu jinsi ulivyo

trudie

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
3,338
7,675
Jana usiku wakati nimekaa na mdogo wangu wa kiume mkubwa anayenifwata kuzaliwa akaniambia "Dada kumbe baba fulani (akamtaja baba mtoto wangu) ndio hana akili hivyo? Yaani jinsi nilivyokuwa namheshimu kumbe ndio ujinga anaouandikaga mtandaoni?

Kwanza shem alivyo busy vile muda wa kuandika ujinga ule anapata wapi, huoni kama anakuaibisha hata wewe? Yaani kusema kweli baada ya kusoma threads zake leo nimemdharau sana. Kweli unaweza kuwa umesoma, una kazi nzuri na pesa ila kichwa hakina akili."

Nikamuuliza umeijuaje ID yake mbona zaidi yangu hakuna anayeijua au ulipekua simu yangu kusoma PM zangu eeh? Akajibu hapana, sehemu nyingi sana anatagiwa hata kuna uzi wake pia alijisema yeye ndio baba wa anko wangu. Kweli Shemeji anajiaibisha sana hata kama tunatumia fake IDs (Mimi na dogo tunazijua ID's zetu).

Baada ya hapo ikabidi nianze kumuelekeza kwamba huyo chizi anayejiaibisha sio baba wa anko wake kabisa, nikamuelekeza kwamba shemeji yake hana ujinga huo. Hata kama simpendi namchukia ila ukweli hawezi kuonyesha ujinga wake hadharani hivyo.

Hata kama ni malaya pia hawezi kujisifia hadharani kubadilisha wanawake kila siku. Yeye yupo busy kwenye majukwaa ya Jamii intelligence na nyuzi za sports. Hata kwa Rick boy kwenye kula kimasihara anaonyeshaga ushamba wake hadharani wa kuwashangaa wenzie wanavyokula mitaro nje nje.

Jamani wanajukwaa mitandao ya kijamii inadefine sana jinsi ulivyo. Kile unachokiandika humu kinadefine uhalisia wako kwa hiyo tujitahidi sana kuandika vitu vyenye tija na vya maana. Unaweza kuwa mtu unayeheshimika kweli ila mitandao ikakufanya ujishushie heshima yako.

Kuna watu wengine huwa najiuliza hivi bahati mbaya hata mdogo wake au mwanae akashika simu yake akijua upuuzi anaoandika humu ataendelea kumuheshimu kweli? Tuangalie maudhui tunayoyaandika jamani.
 
Jamani wanajukwaa mitandao ya kijamii inadefine sana jinsi ulivyo. Kile unachokiandika humu kinadefine uhalisia wako kwa hiyo tujitahidi sana kuandika vitu vyenye tija na vya maana. Unaweza kuwa mtu unayeheshimika kweli ila mitandao ikakufanya ujishushie heshima yako
Huu ni uongo 😃

Mf Romeo National Anthem kuna muda anajizima data anaandika upupu mtupu. Lakini tunaomjua in person tunaona kabisa wa jF sio yule tunayemjua sisi huku nje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom