Kilaini: Kikwete bado ni chaguo la Mungu

Wapendwa jamvi ili liwe la kumkomboa mtz wa anayenyanyaswa na maafidhina na mafisadi lkn matusi na au kukosoana nakusababisha chuki s vema sote wapiganaji sote na wajeshi na wanawasiasa safi na uongozi bora na si bora uongozi.
 
hakuna ulichoandika ni upuuzi na uzandiki tuu!!!!
Kama ulikuwa unataka kumjibu dabomani si ungemjibu ktk ukumbi WAke kitugani kilichokufanya uanzishe mada nyingine mpya wakati tayari ilishaanzishwa? Watu wengine akili huja saa 6 za usiku!!!


Kumbe na wewe ndo Mdogo wake na RIdhiwani na Miraji eh? Baba yako analo mwaka huu ndugu yangu...hata iweje mvua la Dakta Slaa litamelnino kisawasawa...
 
Dr. Slaa huyu ALIYEKI-BLACKMAIL chama chake kimlipe Tzs 12,000,000/= kwa mwezi ndipo akakubali kugombea uraisi?!!!!!!!!!!!. HUYU NDIYE ALIYEJITOLEA MUHANGA KUKUKOMBOENI KWELI? DON'T MAKE ME LAUGH!!! Tzs 12,000,000/= ni zaidi ya 15% ya ruzuku ya CHADEMA kwa mwezi! CHADEMA itapata wapi fedha za kumlipa na hapo hapo zibaki za kuendeshea chama? Au zitatoka VATICAN???
 
Hao ma-genious unaowazungumzia wa marks 120 kati ya 150 ndiyo waliotuulia nchi. Leo hii reli hamna, maji hamna, umeme hamna, barabara zote alizoziacha mkoloni zikiwa na lami zimekuwa kama zimepigwa mabomu nakadhalika. Miji inapanuka lakini badala ya kuwa na barabara inakuwa na vichochoro kama miji iliyojengwa karne ya 16!
Heri wale waliokosa hiyo elimu maana hawatachangia lawama!!!!
 
This is the most WORSE thread i guess. If written by a Tanzanian, then, he/she is in the Mirembe hospital? Pls edit your minds! Udini hauna nafasi ktk kampeni za 2010.
 
kuna mambo nakupa pongezi ila kuna mambo umejichanganya.katika hao unaowataja hakuna mkamilifu kiimani hata mmoja kikwete kashindwa kutuongoza wewe unasema amepeleka kesi za ruswa mahakamani naomba unitajihata moja kwa sababu mpaka sasa kesi ninazozijua ni za kutumia madaraka vibaya na kuendesha gari viba na kusababisha ajali.unaposema ameruhusu bunge kujadili kashfa hatma yake imekuwa nini?bunge liliona watu wamekula rushwa sasa nani kashtakiwa?RA anapeta EL yupo uraiani sasa kama huo si unafiki ni nini?akina MSABAHA NA KARAMAJI bado wanakula mema ya nchi pale bandarini.leo anatutukana kama asingesafiri nje tungekufa njaa.
2.LIPUMBA hajawahi kushika madaraka yoyote katika hii nchi ili tumpime na yo anaweza kuwa mwadilifu hilo hatulijui lakini kbla hatujamjaribu tuangalie mazingira aliyonayo.tazama sura ya cuf tanzania ni nchi isiyo na dini hilo wote tunalikubali sasa hao cuf wameshindwa kujipambanua kwenye hilo chama kilitakiwa kiwe na sura ya kitaifa kwa kuanzia ili dini nyingune ziwe na imani nacho.halafu kila kitu ni lipumba hata kamkutano kadogo na waandishi wa habari.
3.DR SLAA amefanya kazi kama mbunge kwa miaka 15 hakuna ambae hajui alichokifanya kwa ajili ya watanzania(kwa sababu angeweza kufanya kwa ajili ya wana karatu na asingekuwa na kosa)dr amekuwa mwadilifu kwenye mali za uma kuliko angekuja na kutuambia amezitii amri zote 10 ila ameiba mali ya uma kwa sababu nchi yetu ni muhimu kuliko imani ya mtu.
sasa kwa maelezo hayo hapo ukianza kutoa maksi kwa kila kipengele utagundua hakuna wa kumfikia dr. prof si mbaya ila tatizo lake kwa sera hatofautiani sana na dr ila yeyey anataka kutuaminisha kwamba ataweza ila dr ameshaanza kufanya kwsa hivyoni rahisi zaidi kumwamini dr.ukweli kama tz tulikuwa tunamtaka muumini mzuri wa kutuongoza ingekuwa kaazi kwelikweli na maadamu rais anatakiwa kutoka kati ya hao watatu ndio maana akapendekezwa dr.kikwete alisema hajui umasikini wetu unatokana na nini pamoja na kuwa na rasilimali za kutosha. kwa hiyo mpaka hapo amefeli mtihani wa kutuongoza.huwezi kuongoza watu ambao hujui wanakwena wapi? Lipumba sina shida nae sana akirekebisha mambo madogomadogo kwenye chama atafaa baada ya Slaa.
na kwa taarifa yako kila rais ana kashfa katika ndoa kuanzi awamu ya kwanza hadi hii kama unahitaji nitakuletea hapa.
 
Mungu wangu! Tumeshakosa hoja namna hii.
Daboman mi nitahoji kitu kimoja tu. Kuwa unasema shule za kata na chuo kikuu cha Musoma vitasaidia kupunguza matabaka ya elimu nchini. Utangoja sana. Hizo shule za kata chuo kikuu hawafiki@. Mkoa kama Kilimanjaro mwaka 1994 ulikuwa na shule za Secondary 240 sijui sasa ziko elfu ngapi. Good private schools watu pale hawaendi voda fasta. Utawakuta chuo kama hawana akili nzuri. Kahawa imeshuka bei lakini ukiangalia kinaga ubaga wapo kila mahali ambapo hela inaweza tengenezwa Tanzania. Ukienda mahali unataka kuishi ukikuta hamna mchagga kimbia ufe maana hapo hamna kitu.
Mwishow a siku vyuo vitaangalia watanzania waliofaulu kinachagua waingie Chuo na wengi watatoka huko huko kwa wasomi.
Kama wewe ni strategist wa usawa sema kuwe na quota system kuingia chuo kikuu kama ilivyokuwa wakati wa secondary za bweni za serikali. Kila mkoa ulikuwa na fungu lake. Na unajua nini? Hiyo iliongeza sehemu zilizochanuka kwenda Chuo kikuu.

Mwaka 1989 nikimaliza darasa la saba ili uende shule ya serikali kilimanjaro ulikuwa unatakiwa uwe na 120 kati ya 150 marks. Mwaka huo hio Mtwara walikuwa wanachukua watu wenye 65/150 kuingia boarding school. Watu wengi wenye 115 -100 wa Kilimanjaro walioenda Private school baada ya miaka mi4 wanapiga div 1/2 wanaingia form 5 ya bure ya serikali aka ada 1500. Yule aliyeingia form one na 65 kwa vile alikuwa na maandalizi pungufu anaishia kupata 4 anarudiu kuwa katibu wa kijiji chao. Vichwa vya form 5 na six vinapasua unakutana nao Mlimani wanadunda. Hao ndo sisi unasikia we kilaza?

Umejenga hoja yenye uongo wa hali ya juu. Tukiwa na watu 20 wenye mawazo kama yako vita haipo mbali. You need to think again maana siku hizi watu wanakwambia NGASHTUKA!

kanisa likisema muislam ni chaguo la mungu ni sawa lakini likisema fanya mabadiliko ni kuleta vita. kweli wewe una uchungu na nchi.
 
Dr. Slaa huyu ALIYEKI-BLACKMAIL chama chake kimlipe Tzs 12,000,000/= kwa mwezi ndipo akakubali kugombea uraisi?!!!!!!!!!!!. HUYU NDIYE ALIYEJITOLEA MUHANGA KUKUKOMBOENI KWELI? DON'T MAKE ME LAUGH!!! Tzs 12,000,000/= ni zaidi ya 15% ya ruzuku ya CHADEMA kwa mwezi! CHADEMA itapata wapi fedha za kumlipa na hapo hapo zibaki za kuendeshea chama? Au zitatoka VATICAN???[/SIZE]


Siamini kama ndiye wewe uliyeandika hiyo article hapo juu, au kuna mtu kakuibia ID yako.....................Nilikuwa nafikiria kuandika kutetea hoja zako lakini kama hii ndiyo misimamo yako, it is just absurd and pathetic.

Hivi hii habari ya dini ambayo umeielezea vzuri madhara yake katika suala zima la ukombozi inakuwa hatari ikiwa ni ukristo tu??? Umenisikitisha sana mkuu
 
ila huyo mungu, ni wa yule mchawi maarufu afrika mashariki - shehe yahaya wa husein

Angalizo - mods, hii mada haina uhusiano na mada yoyote ile hapa jukwaaani. Natumaini itaachwa hapa kwenye jukwaa la siasa ikiwa peke yake.

Ukitaka kuuliza kama hii ni siasa, jibu swali hilo hilo kama mada ya kikwete kutokuwa chaguo la mungu iliyoanzishwa na dobomani ni ya siasa au la. Hiyo mada imekaa jukwaani kwa zaidi ya masaa 24.
 
Dr. Slaa huyu ALIYEKI-BLACKMAIL chama chake kimlipe Tzs 12,000,000/= kwa mwezi ndipo akakubali kugombea uraisi?!!!!!!!!!!!. HUYU NDIYE ALIYEJITOLEA MUHANGA KUKUKOMBOENI KWELI? DON'T MAKE ME LAUGH!!! Tzs 12,000,000/= ni zaidi ya 15% ya ruzuku ya CHADEMA kwa mwezi! CHADEMA itapata wapi fedha za kumlipa na hapo hapo zibaki za kuendeshea chama? Au zitatoka VATICAN???

My Dear, Naamini wewe ni beneficiary wa Uongozi Mbovu na wa Kifisadi Ulioko Madarakani. Pamoja kwamba unabefit, nikuombe epuka kitumia huruma ya Mungu kwenu nyinyi mnaoinyonya nchi kwa kauli za namna hii. Maana iko siku yatakufika na utajutia maneno yako.

Ninaamini mtu yeyote mwenye akili timamu hahitaji propaganda ili kujua uwezo na uzuri wa Dr. Slaa.
Ukikaa chini ukatafakari vizuri utaona mbele ya maisha yako kama mtanzania ni giza pamoja na kwamba sasa hivi unafurahia hicho ulichonancho.
 
amiri jeshi mkuu na mlinzi mkuu wa jamaa amemchagua tena kuiongoza tanzania,namaanisha sheikh yahaya
 
Ina maana Obama na ndugu zake weusi kule Marekani waliuzwa kule kutokea Zanzibar? Very Funny! Zanzibar ya kiislamu ina share yake katika utumwa kama ilivyo kwa wakatoliki na waprotestant wa ulaya ambao nao wana share yao pia. Hivi unadhani watu weusi kule Marekani, West Indies, Carribean na South America wametoka wapi?
In any case 99% ya watumwa wote waliokuwa wanauzwa Zanzibar walikuwa wananunuliwa na wazungu kwenda kwenye mashamba ya miwa kule Mauritius na South Africa. Ndiyo maana leo pale Durban, South Africa kuna watu wanaitwa Wazanzibari pamoja na kwamba hiyo Zanzibar yenyewe hawaijui hata kidogo.
 
Umesema Lipumba na Georgina?
Ni lini Lipumba alifunguliwa kesi mahakamani kwamba katorosha mke wa mtu? Au ni lini Lipumba aliishi na kimada, akazaa naye kisha akamtosa na kuvamia mke wa mtu mwingine? Tena bila kujali kuwa huko nyuma alishakula nadhiri ya useja?
Ukisikia utovu uliokubuhu wa maadili ndiyo huo!
 
Kwa taarifa yako:
1. CUF ina sura ya kitaifa mara elfu moja kuliko CHADEMA - Tofauti na CHADEMA, CUF Ina strong presence pande zote mbili za muungano
2. Pili, CUF ina mtandao ulioenea nchi nzima na hakitegemei kununua viongozi wa vyama vingine kufacilitate mikutano yake kama ilivyokuwa inafanya CHADEMA wakati wa operesheni Sangara.
3.Tatu, 75% ya viongozi wake katika ngazi ya wilaya ni wakristo, ila ni wale wakristo wanaojua kuwa mustakabali mwema wa nchi utatokana na ujenzi wa jamii inayozingatia kanuni ya HAKI SAWA KWA WOTE.
 
Dabomani nimekusoma ila kuna kitu nakuona unaingiza hapo katikati ya hoja zako.Ulichoingiza ni swala zima la udini ukristo na uislamu.Inaonekana wewe ni muumini wa dini,na kwa kufanya hivyo huwezi kabisa kufika.Issue sio udini,kuwa ni muislamu au la.Issue ni kuhusu mustakabali wa Taifa letu.Kwenye historia wapo watu waliwahi kuchaguliwa na Mungu na waliposhindwa kazi Mungu aliwaondoa,mfano Mfalme Sauli ambaye aliondolewa na Mfalme Daudi.Hivyo sio ajabu 2005 akawa chaguo la Mungu na sasa akakataliwa kutokana na utendaji wake.
Kuhusu mashindano ya kidini uliyojaribu kuyaanziasha,hayo tuyaache maana unaulaumu ukristo wakati ndio wanaotoa dira ya dunia,kwani hata huyu aliyekuwa anaombaomba kila mahali hakupewa msaada na hao wakristo?Hata huko marekani anakojisifu kuwa wa kwanza kufika ni wa kina nani??
Dabomani MFUPA ULIOMSHINDA FISI..............Muda usingetosha,niseme nini basi maana ni mengi ila tusiende kwenye issue za Ukristo na Uislamu.
 
Kama alikuwa Chagua la Mungu sijui ni wa mungu wa mabaali au wa kutazama Nyota, basi haikosi kuwa CCM kwa kutaka sifa waliwanuunua hao walisema hivyo, lakini kama alipata neema ya kuongoza kwa miaka hiyo aliyopewa aligeuka kam Saukli na kutokuwa Chaguo la Mungu Wa ISRAEL bali akaifuata njia ya wapiga ramli na watazama bao na nyota , na kuindeleza udini na si kusimamia Taifa lenye neema kama Tanzania n Sijui mwaka huu nani ataiongoza Tanzanai na pia kuwa rais si kuwa Chaguo la Mungu ila ni Kipajia nachokuwa nacho mtu Hata Absolum alitawala ila hakuwa Chaguo la Mungu ndio maana akauwawa Ndivyo ilivyokuwa kwa kikwete na hata akijaribu kutumia Nguvu ya kuiba kura na kuwapiga wananchi atakufa yeye na watu wake. hao viongozi wa dini wasiwapotoshe watu kuwa mtu anapovuma si kuwa ni chaguo bali ni ile Kipajia alichosaliwa nayo mtu hata kama ni muovu maana neema ya Mungu huwaangazia waovu na wenye haki,
 
Hoja za udini hazina nafasi kwenye JF. Umeandika mlolongo wa hoja zilizojaa udini na upendeleo kwa Serikali inayoishi kwa propaganda badala ya ku-concentrate na utatuzi wa matatizo ya kichumi ya nchi yetu. Kwa nini hutaki kuamini kwamba kikwete na ccm yake nchi imewashinda? Watanzania wa leo hawaaminishwi na hoja kama zako zisizo na kichwa wala miguu. Wanachotaka sasa ni mabadiliko. Dr. Slaa kwa nafasi ya Ubunge tu ameonesha mwanga kwamba sauti ya wananchi ina nguvu kuliko nguvu ya kifisadi. Tunachofanya mwaka huu ni kumpatia mamlaka kamili na ya juu ili aturejeshee kwenye misingi yetu ya kujenga uchumi imara na endelevu iliyoachwa na Mwl. Nyerere na kutelekezwa na chama cha mafisadi.
 
Hoja za udini hazina nafasi kwenye JF. Umeandika mlolongo wa hoja zilizojaa udini na upendeleo kwa Serikali inayoishi kwa propaganda badala ya ku-concentrate na utatuzi wa matatizo ya kichumi ya nchi yetu. Kwa nini hutaki kuamini kwamba kikwete na ccm yake nchi imewashinda? Watanzania wa leo hawaaminishwi na hoja kama zako zisizo na kichwa wala miguu. Wanachotaka sasa ni mabadiliko. Dr. Slaa kwa nafasi ya Ubunge tu ameonesha mwanga kwamba sauti ya wananchi ina nguvu kuliko nguvu ya kifisadi. Tunachofanya mwaka huu ni kumpatia mamlaka kamili na ya juu ili aturejeshee kwenye misingi yetu ya kujenga uchumi imara na endelevu iliyoachwa na Mwl. Nyerere na kutelekezwa na chama cha mafisadi.

mods wa hii forum wanapenda hizi mada za udini..... strategy ya ccm hiyo na mods wanafurahia upupu kama huu
 
Mwaka 2005 maaskofu walijifunga vibwebwe na kufanya kile ambacho kisingetarajiwa kifanywe na viongozi wa dini. Bila kujali kuwa walichokuwa wanakifanya ni kinyume kabisa na maadili ya 'FAIR PLAY', yaani kutocheza rafu ya makusudi, walijitoa hadharani na kudai kuwa Taifa lilikuwa linahitaji kiongozi mwadilifu na mcha Mungu; na huyo hakuwa mwingine bali Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye aliyekuwa 'CHAGUO LA MUNGU'!

Hakuna shaka yoyote kuwa kwa kitendo kile maaskofu walicheza rafu ya makusudi. Ni kwa nini nasema hivi? Nasema hivi kwa sababu kwa jinsi mfumo wa uendeshaji wa dini ya kikiristo ulivyo, na hasa kwa dhehebu la Roman Catholic, mlei, yaani muumini wa kawaida, mahusiano yake na muumba wake ni lazima yapitie kwa kiungo ambaye ni padri au askofu. Wabunifu wa utaratibu huu wameweka kanuni mbili muhimu ambazo zinawahakikishia utiifu wa waumini wao kwa muda wote.

Kwanza ni kanuni ya kujumuika kundini. Kwa mujibu wa kanuni hii utahesabiwa kuwa wewe ni muumini wa kweli na mwenye haki za kiroho sawa na waumini wengine, pale tu viongozi wa kanisa watakapojiridhisha kwamba umo 'kundini'; kwa maana ya kuwa unashiriki kikamilifu katika shughuli za kanisa lako chini ya miongozo ya padri wako. Kwa kutumia kanuni hii, wale wanaokwenda kinyume na miongozo ya mapadri na maaskofu wao hujikuta wakipewa adhabu ya kutengwa; na hii ni adhabu kubwa sana kwa sababu unatengwa ukiwa hai mpaka maiti yako!

Kanuni ya pili, ni ile ya mapadri na maaskofu kuwa na mamlaka ya kupokea toba za waumini wao. Kwa mujibu wa kanuni hii, waumini wakifanya dhambi, suala la toba siyo la binafsi kati ya mfanya dhambi na muumba wake, bali ni lazima toba ipitie kwa padri au askofu; ambaye baada ya kusikiliza ungamo lako ana mamlaka ya kutamka kuwa umesamehewa.

Mfumo huu unaozuia mawasiliano ya moja kwa moja kati ya muumini na muumba wake umeweza kujenga utii mkubwa sana wa waumini kwa mapadri na maaskofu wao na kusababisha kanisa kuwa na nguvu ya ajabu. Nguvu hii inatokana na ukweli kuwa kwa kutumia mfumo huu mapadri na maaskofu wamekuwa na mamlaka makubwa sana juu ya waumini wao kuhusu nini wafanye na nini wasifanye.

Maaskofu waliposema kuwa JK ni 'CHAGUO LA MUNGU' ilikuwa ni rafu ya makusudi kwa sababu walikuwa wanajua fika kuwa kwa mamlaka waliyonayo juu ya waumini wao tamko lao lilikuwa ni agizo kwa waumini wao kuhakikisha kuwa siku ya kupiga kura, kura zao zinaenda kwa JK.

Kwa mkristo mkereketwa kutotii agizo la askofu wake siyo tu kuwa ni dhambi, lakini pia ni kutafuta kufukuzwa kutoka 'kundini'. Sasa nani yuko tayari kufanya 'dhambi' ya waziwazi kabisa kama hiyo na kutengwa akiwa hai hadi maiti yake?

Tatizo la kanisa kuwachagulia waumini wao viongozi ni la kihistoria na wala halijajifunga katika mipaka ya kijiografia. Wakina Vladmir Lenin kule Urusi mwanzoni mwa karne ya ishirini walipokuwa wanafanya jitihada za kuwazindua wafanyakazi na wakulima wa huko kuupindua mfumo wa kibwenyenye uliokuwa unawatawala na kuwanyonya, kikwazo chao kikubwa kilikuwa ni viongozi wa kanisa.

Utiifu wa walalahoi hao wa kirusi kwa viongozi wao wa kanisa ulikuwa mkubwa kiasi cha kumlazimisha Lenin kutamka hadharani kwa uchungu kuwa 'DINI NI KASUMBA YA WATU'. Kasumba kama vilivyo vilevi vingine, kazi yake kubwa ni kumzuia mtu kujitambua na kuyatambua mazingira yake katika uhalisia wake.

Wakati vichwa vikiwauma wakina Lenin na Trosky kule Urusi jinsi ya kufuta kasumba ya ukristo kwenye akili za Warusi, kasumba hiyo pia ilikuwa imekamata akili za watu wengi katika mataifa mengine ya Ulaya. Kwa mfano, pamoja na kwamba kule nchini Uingereza hali ya wafanyakazi wengi ilikuwa ni duni sana, jitihada za chama chao cha Labor kushika madaraka ya dola ili kuboresha hali zao za maisha zilikuwa

zinakwamishwa na wafanyakazi wenyewe! Makada wa Labor walikuwa wakitukanwa, kubezwa na hata wakati mwingine kupigwa. Hali kwa makada wa Labor waliokuwa wanaendesha 'Operesheni Zinduka' hiyo iliendelea kuwa mbaya hadi mwaka 1914 pale kitabu cha hadithi cha mwandishi Robert Tressel, kinachoitwa 'The Ragged Trousered Philanthropists', yaani, 'Wasamaria wema waliovaa viraka', kwa tafsri isiyo rasmi, kilipochapishwa.

Kwa kifupi kitabu hiki kilikuwa kinawazungumzia wafanyakazi wa Uingereza ambao hali zao za kimaisha zilikuwa duni sana. Kilikuwa kinawaashangaa ni kiasi gani walikuwa HAWAJIONEI au KUWAONEA HURUMA WATOTO WAO kwa kuleta mabadiliko ya kisiasa, ukizingatia kuwa uwezo wa kufanya hivyo walikuwa nao kupitia kura zao.

Juu ya hali hiyo, mwandishi wa kitabu hicho, Robert Tressel, alielekeza lawama zote kwa kwa kanisa. Alilituhumu kuwa lilikuwa linatumiwa na watawala mabwenyenye na wakandamizaji waliokuwa wameshikilia mamlaka ya kisiasa kuwadanganya waumini wao - kuwa kuendelea kuwatii waliokuwa na mamlaka ya kisiasa juu yao ni KUMTII MUNGU - kwa sababu ati mamlaka zote za kisiasa zimewekwa na Mungu! Kupitia mhusika mkuu ndani ya hadithi hiyo, Tressel aliwaambia wafanyakazi kuwa njia nyepesi ya kuthibitisha kuwa makasisi wao walikuwa wanasema uwongo ni kuwapa changamoto ya kunywa sumu hadharani kwa sababu Bibilia inasema wazi kuwa muumini wa kweli kabisa hata akinywa sumu haitamdhuru!

Wachambuzi wa siasa za Uingereza za kipindi hicho cha mwanzoni mwa karne ya ishirini wanaamini kuwa kitabu hicho cha Tressel kilikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa chama cha Labor pale chama hicho kiliposhinda kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuunda serikali mnamo mwaka 1924.

Mkakati wa watawala na mabwenyenye ya Ulaya kutumia ukristo kama 'kasumba' ya kuwaleweshea watu ili watawalike na kunyonywa kwa urahisi haukuishia kwenye mipaka ya bara hilo. Wakati tawala za Ulaya zilipokutana na kuamua kugawana bara la Afrika, wamishenari walitumiwa kama 'advance party', yaani wasafisha njia.

Kutokana na uzoefu ziliokuwa nao, tawala hizo zilijua fika kwamba itakuwa ni rahisi zaidi kwa wenyeji wa bara hili kuukubali ukoloni iwapo wenyeji hao tayari watakuwa wametiwa kwenye ukristo.

Afrika Mashariki ni mfano mzuri. Mnamo mwaka wa 1863, makasisi wa Holy Ghost Fathers walitua Zanzibar - nchi ya kiislamu – na kuomba waruhusiwe kufungua kituo chao. Tukio hili ambalo lilikuwa la kwanza la kurasimisha ukristo katika ukanda wa Afrika Mashariki lilitokea takriban miaka 20 kabla ya mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Mkutano huu ndio ulioigawa rasmi ardhi ya Afrika katika mapande mapande na kila tawala iliyohudhuria mkutano huo kukabidhiwa kipande au mapande yake ili kusimika ukoloni.

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia, Marekani ilianza kuweka shinikizo kwa mataifa ya Ulaya ili yatoe uhuru wa bendera kwa makoloni yao; na kupisha njia ya kusimikwa kwa ukoloni mamboleo. Kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni mkongwe, ukristo ulitumiwa tena kama mbeleko ya kuubebea huo ukoloni mamboleo.

Zilitumika juhudi kubwa kuhakikisha kuwa takriban viongozi wote wa mwanzo wa zile nchi ambazo zilikuwa zimekabidhiwa uhuru wa bendera ni wakristo, ambao pamoja na mambo mengine, wana jukumu pia la kulinda maslahi ya ukristo dhidi ya yale ya Taifa.

Tanzania ni mfano mzuri. Pamoja na jitihada kubwa sana zinazoendelea usiku na mchana za kumtukuza Mwal. Julius Kambarage Nyerere, Nyerere alikuwa ni mmoja wa viongozi hao. Mwandishi Jan P van Bergen katika kitabu chake Development and religion in Tanzania, amefichua taarifa za kikao cha siri Ikulu ya Dar es Salaam mnamo Agosti 3, 1970 kati ya Rais Julius Nyerere, Padri Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa, Giovanni Cerrano. Kwa mujibu wa van Bergen, katika kikao hicho Nyerere aliwaeleza viongozi wake wa dini kuwa ameunda idara ya elimu ya siasa katika TANU na amemuweka Padri aiongoze kwa sababu ya imani yake madhubuti. Aliwaeleza pia kuwa katika Kamati kuu ya chama ameweka Mapadri lengo likiwa kulipa Kanisa fursa na uwezo mkubwa hapa Tanzania.

Kutokana na matendo na kauli za maaskofu mbalimbali katika kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea hivi sasa inaonekana dhahiri kuwa rais Kikwete hatakiwi tena na maaskofu. Moja ya matendo ya dhahiri kabisa kufanywa na maaskofu yanayoonyesha msimamo wao ni lile tukio la kuukataa mwaliko wake wa kufuturu naye kule Mbeya wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani uliomalizika hivi karibuni.

Lakini ukitaka kujua kuwa kweli safari hii hawamtaki, rejea matamshi ya askofu Zakariah Kakobe wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwa waumini wake, ambapo pia aliitumia fursa hiyo kufuta ibada katika makanisa yake yote siku ya Jumapili ya uchaguzi, ili tu awe na uhakika kuwa kila muumini wake hatakuwa na kisingizio cha kuacha kwenda kupiga kura.

Kakobe amenukuliwa akiwataka waumini wake wasitilie maanani tabia binafsi za wagombea zinazohusu mahusiano yao ya kingono, na badala yake waangalie kile ambacho amekiita, 'kipaji' cha mgombea. Pamoja na kwamba hakumtaja kwa jina, lakini kwa kuzingatia kuwa kati ya wagombea wote wanaowania nafasi ya uraisi kwa sasa, ni Dr. Slaa pekee ndiye aliyekumbwa na kashfa ya ngono, moja kwa moja inaonyesha kuwa Kakobe alikuwa anawapa maagizo waumini wake wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura na kumpigia Dr. Wilbrod Slaa.

Jambo la kushangaza sana kwa ndugu zangu maaskofu ni kwamba, ukiondoa mambo kadhaa yanayomwongezea sifa, 'Kikwete chaguo la Mungu' wa 2005, ndiye huyo huyo ambaye tunaye mwaka 2010. Hata hivyo tofauti na Kikwete wa 2005, hivi sasa Kikwete amekomaa zaidi, kwa maana ya kwamba ameongezeka umri na pia amepata uzoefu wa ziada. Katika tamaduni zetu za Kiafrika 'Mtu mzima ni dawa' , na katika taratibu za uendeshaji wa mambo 'uzoefu wa kina' ni jambo linalotukuzwa.

Aidha Kikwete na serikali yake wameweka mtandao mkubwa wa shule za sekondari za kata na kuongeza kwa kiwango kikubwa sana nafasi za masomo katika taasisi za elimu ya juu, hususan kupitia ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma kinachochukua zaidi ya wanafunzi 40,000 na kile ambacho kiko mbioni kujengwa mkoani Mara kitakachochukua idadi hiyo hiyo ya Wanafunzi. Ni wazi kabisa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo mtandao huu wa shule za sekondari na vyuo vikuu utakuwa umefuta kabisa pengo kubwa la kielimu lililopo siyo tu kijiografia, lakini pia kati ya jamii mbalimbali nchini.

Miaka kumi ijayo jamii ya Waislamu haitakuwa tena na sababu za kusema kuwa serikali inawapendelea Wakristo katika nyanja ya elimu; na viongozi wa serikali nao hawatakuwa tena na wakati mgumu wa kuwaambia Waislamu kuwa 'tatizo lao ni la kihistoria' kila wanapofikishiwa malalamiko ya Waislamu. Bila shaka hali hii siyo tu kuwa itaimaarisha mshikamano nchini, lakini pia itakuwa imeweka msingi mzuri kutuhakikishia kuwa amani tuliyonayo nchini inazidi kudumu.

Kikwete pia ametoa mchango mkubwa sana kwa demokrasia nchini kwa kitendo chake cha kubariki maridhiano baina ya vyama vya CCM na CUF kule Zanzibar. Tofauti na Watangulizi wake ambao walikuwa wakifanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa Zanzibar muda wote inaendelea kuwa chini ya genge la CCM wahafidhina, Kikwete kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu amejenga mazingira ya kuhamisha kitovu cha madaraka kutoka kwenye mikono ya wahafidhina hao, na kukiweka kwenye mikono ya Wananchi. Kama jina lake lilivyo, Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar itakuwa ni serikali ya Wananchi kwa kila hali.

Aidha, tofauti na Mkapa ambaye aliunda tume ya Warioba kwa nia ya kutambua vyanzo na mianya ya rushwa na kisha baada ya kukabidhiwa ripoti akaifungia kabatini na kuisahau; Kikwete kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi amethubutu kuondoa kulindana na u-mwenzetu katika vita dhidi ya ufisadi.

Kitendo chake cha kuruhusu kesi kadhaa za vigogo wa serikali yake na ile ya mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, kufikikishwa mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi; ni kielelezo cha wazi cha mabadiliko hayo ya msingi yanayolenga kuondoa dhana kuwa kuna watu 'wasioguswa' na sheria.

Thamani ya kitendo chake haimo kwenye utambulisho binafsi wa nani kafikishwa mahakamani na nani hajafikishwa, ila iko katika 'ujasiri wa kuvunja mwiko' ambao tumeuzoea kuwa siku zote wanaokamatwa na kufikishwa mahakani ni vidagaa tu wakati mapapa, masangara na manyangumi ya ufisadi yanaachiwa yaendelee 'kutesa'.

Aidha kitendo chake cha kuliachia bunge lichunguze kwa kina zabuni ya ukodishaji wa mitambo ya umeme iliyozaa kashfa ya Richmond na kupelekea aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowasa na mawaziri wenzake wawili kujiuzulu, ni moja ya vielelezo vya 'ujasiri huo wa kuvunja mwiko'.

Kashfa ya Richmond haina tofauti sana na kashfa ya ununuzi wa meli ya MV Bukoba enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere. Hata hivyo tofauti ni kwamba enzi ya Nyerere bunge halikuwa na uhuru wa kujadili lolote kwa kina; na kwa maana hiyo basi mjadala wa kina juu ya kashfa ya meli hiyo ukaepukwa.

Enzi ya Nyerere zilikuwepo pia kashfa za kukodi ndege mbovu, kashfa ya farasi wa makatibu kata, nakadhalika. Utawala wa Nyerere ulikwepa kashfa hizi kwa sababu tu vyombo huru vya habari havikuwepo; na pia kwa sababu Nyerere hakuona haya kutumia mamlaka ya kikatiba aliyokuwa nayo kutishia kuvunja bunge pale lilipoonekana kutaka kuchafua hali ya hewa. Tusisahau kuwa hadi leo raisi wa Tanzania bado ana mamlaka hayo kikatiba, na Kikwete angeweza kuyatumia kama angetaka.

Kama nia ni mabadiliko, huenda maaskofu wangehangaika kumpigia debe Prof. Lipumba kwa kigezo cha sifa huenda kidogo tungewaelewa; kwani hakuna mtu yeyote mkweli ambaye hatakiri kuwa Prof. Lipumba kawazidi sifa kwa kila hali wagombea wenzake wanaowania nafasi ya uraisi kwa sasa.

Lakini maaskofu hao wanapojifunga vibwebwe kujaribu kuwaghilibu wafuasi wao kuwa 'wasiangalie mambo binafsi ya wagombea' wakati wa kupiga kura, hata kama mambo hayo yanakiuka zile AMRI KUMI ZA MUNGU, hapo ni lazima tupate wasiwasi juu ya ajenda halisi ya maaskofu wetu. Ndiyo maana tunauliza: Hivi kweli hizi ni kampeni, au ni vita ya msalaba?
huu upupu! naomba kukuuliza kwanza kama kulikuwa na kashfa kipindi cha Nyerere does that make Kikwete any better? does 1 + 1 = 1/2 ? or 2 ? naomba ujiulize!
pili je serikali huendesha na sheria za dini? kama mgombea amevunja amri kumi inahusu nini kuendesha serikali! au ndo wale mnaopigania sharia laws hamjui kutenganisha serikali na dini? hizi ndo tunaita fikra zilizokosa akili zinazokimbilia mambo ya msahafu kwenye mambo ya dunia!
 
Dabomani,

..elekeza mashambulizi yako kwa chama tawala CCM.

..unapoteza mvuto kwa chama chako, CUF, kwa kushambulia Wakristo na kanisa Katoliki.

..hii ni makala ya pili naisoma imeandikwa na kada wa CUF na ina maudhui ya udini-udini.
 
Back
Top Bottom