Kila siku ni 'wasaidizi wake'... KWANINI SIYO KIKWETE mwenyewe?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995

Tangu 2006 kuna mengi yametokea kuhusiana na utendaji na uongozi wa Rais Kikwete. Kuna imani ambayo imejengeka kuwa Rais "anashauriwa vibaya" na hivyo huwa anasema au anafanya vitu kwa sababu 'wasaidizi' wake wamemuelekeza vibaya n.k Kuanzia sakata la mapanki na mwitikio wake kuhusu filamu ya Darwin's Nightmare hadi hii ziara ya Marekani kuna vitu vinafanyika na mara zote watu wote hulaumiwa isipokuwa rais mwenyewe.

Tumeona kwenye CCM kama ilivyo kwenye serikali wanalaumiwa watu wengine wote isipokuwa mtu pekee ambaye anastahili kulaumiwa. Mawaziri mara nne wamelaumiwa na wananchi na mara nne ndani ya miaka sita Rais amelazimika kufanya mabadiliko. Lakini mara hizo zote wanalaumiwa ni mawaziri na watendaji isipokuwa mtu pekee mwenye uwezo wa kuwawajibisha.

Sasa itachukua muda gani kwa watu wengine kuelewa na kukubali kuwa tatizo yawezekana ni Rais mwenyewe na namna (manner) ya uongozi wake wa kukaa pembeni (hands off approach)? Yawezekana amekuwa akiachilia vitu vitokee kwa sababu hataki kubeba lawama na hivyo watu wengine kabisa walaumiwe? Kwa mfano la Lowassa analaumiwa Mwakyembe, la mawaziri wanalaumiwa watendaji wa chini, la watu kuwajibishwa wanalaumiwa wabunge n.k? Yeye mwenyewe mara zote anakuwa mtu wa kunung'unika asiyekubali kosa lolote au kuwajibika kwa lolote?

Inawezekana pia ni jitihada ya kumuonesha kuwa ame-delegate power na hivyo haitaji kujishughulisha na mambo hayo yote?
 
Ubarikiwe sana kwa kusema ukweli mchungu.

Ni kweli mara zote hii hoja imekosa mashiko na miguu, lakini nashangaa imeendelea kutumika. Kuna mambo mawili, nionavyo:
1) JK anaogopwa sana (ni dikteta wa hisia); kiasi kwamba hakuna mwenye kudiriki kumkosoa ktk ccm na serikali.
2) Ni kweli kuna wasaaidizi wanam-sabotage kwa vile ameshindwa kusimamia mambo fulani muhimu ya kitaifa
 
Mkuu kama ni delegation of power sidhani hivyo. Mfano mawaziri wamevurunda waziwazi na uozo wao umeanikwa hadharani na wabunge. Tulitegemea on the spot kuchukua hatua kuwawajibisha lakini ikawa ndivyo sivyo hadi mwishoni baada ya kuonekana anabanwa ndo akaomba idhini ya kuwawajibisha.
Sehemu kubwa ya malalamiko hayo anayafumbia macho sababu nae anaguswa na maslahi husika ndo mana anashindwa kufanya maamuzi magumu kama alivyoahidi.
 
Tangu 2006 kuna mengi yametokea kuhusiana na utendaji na uongozi wa Rais Kikwete. Kuna imani ambayo imejengeka kuwa Rais "anashauriwa vibaya" na hivyo huwa anasema au anafanya vitu kwa sababu 'wasaidizi' wake wamemuelekeza vibaya n.k Kuanzia sakata la mapanki na mwitikio wake kuhusu filamu ya Darwin's Nightmare hadi hii ziara ya Marekani kuna vitu vinafanyika na mara zote watu wote hulaumiwa isipokuwa rais mwenyewe.

Tumeona kwenye CCM kama ilivyo kwenye serikali wanalaumiwa watu wengine wote isipokuwa mtu pekee ambaye anastahili kulaumiwa. Mawaziri mara nne wamelaumiwa na wananchi na mara nne ndani ya miaka sita Rais amelazimika kufanya mabadiliko. Lakini mara hizo zote wanalaumiwa ni mawaziri na watendaji isipokuwa mtu pekee mwenye uwezo wa kuwawajibisha.

Sasa itachukua muda gani kwa watu wengine kuelewa na kukubali kuwa tatizo yawezekana ni Rais mwenyewe na namna (manner) ya uongozi wake wa kukaa pembeni (hands off approach)? Yawezekana amekuwa akiachilia vitu vitokee kwa sababu hataki kubeba lawama na hivyo watu wengine kabisa walaumiwe? Kwa mfano la Lowassa analaumiwa Mwakyembe, la mawaziri wanalaumiwa watendaji wa chini, la watu kuwajibishwa wanalaumiwa wabunge n.k? Yeye mwenyewe mara zote anakuwa mtu wa kunung'unika asiyekubali kosa lolote au kuwajibika kwa lolote?

Inawezekana pia ni jitihada ya kumuonesha kuwa ame-delegate power na hivyo haitaji kujishughulisha na mambo hayo yote?

You've hit the nail squarely on its head!
 
kwani kenye ripoti ya CAG wapi rais katajwa? kwani hajui/hapati mgao yanayo yanayotendwa na kina maige n co.
 
Mfano mzuri ni Prof Magembe, Mkuchika na Hawa Ghasia. Wizara zao za mwanzo zimejaa uozo na CAG report imeweka mambo hadharani. Kwa nini wengine wachukuliwe hatua na wengine wabaki? Hii ni kuleta mtafaruku ndani ya chama maana wabunge wa CCM wataambia nini wananchi kuhusu hao mawaziri waliobaki?
 
Tusitake kuyumbusha akili za watu wenye kufikiri sawasawa.Udhaifu anao rais toka mwanzo wa utawala wake.Rais kwa mujibu wa katiba yetu anao uwezo wa kumteua mtu yeyote katika nafasi anayoona inafaa na anao uwezo wa kumfuta kazi mtu yeyote aliyemteua bila kutoa maelezo yoyote kwa mtu yeyote.Hivyo kushauriwa vibaya na watendaji wake ili hali yeye anajua wanamshauri vibaya huo ni udhaifu wake kiuongozi.
 
Kiini cha tatizo ni KIKWETE. Nashangaa watu na akili zetu tunapoteza muda wa kuwalaumu akina Magembe, Mkuchika, Lowassa, n.k. Hata upande wa chama chake cha magamba, kiini ni hicho hicho kinachoitwa KIKWETE. Ni kama kirusi kinachoua nchi lakini wanachi wanapoteza muda kukitafuta. Sasa nataka niwaambie kirusi ndiyo hicho na tutaendelea kuteseka kwa kuwaonea mawaziri na viongozi wengine wa ccm bure.
 
JK amedhalilisha sana taasisi ya urais kiasi cha kufanya watendaji nao waone bora liende tuu. Ona familia ilivyo na nguvu kuliko watendaji kadhaa wakuu. Tumeona Mama Salma akifanya ziara mikoani na Wakuu wa mikoa wakisimama mguu sawa kumsomea taarifa za mikoa kwa jinsi ile ile anayosomewa Rais au PM. Jee hiyo ni sawa?
Teuzi mbalimbali zikiwemo hizi za MaDC tumesikia kwa uwazi kabisa kuwa kijana wake Ridhiwani kama huivi naye hupati uDC hiyo inamaanisha majina mengine yalipelekwa naye au baadhi walichujwa na Ridhiwani kwa vile hawaivi naye.
Udhaifu huo ndani ya CCM wanauona na chanzo wanakijua ni nani ila wametengeneza wimbo kuwa "ni wasaidizi wake na watendaji ndio wabovu" huu ni unafiki mkubwa sana na ndio chanzo cha matatizo mengi ya nchi hii.
Lowasa kasema CCM inatatizo la Uongozi sio watendaji, ona kauli zinazotolewa sasa! eti akitaka aende aendako kama vile chama ni cha hao wachache wasiotaka kumfunga kengele paka.
 
mtu akikushauri jambo la kijinga na wewe ukakubali kulitekeleza huku ukujua ni la kijinga basi wewe ni mjinga kuliko aliyekushauri! Rais unatakiwa kwanza wewe mwenyewe uwe na vision (maono) yako then ushauri unakuwa kama kuboresha maono hayo lakini pale unapotumia ushauri kama ndio vision yako una tatizo! Rais wetu hapendi kulaumiwa kwa kuwa kwenye serikali na taasisi zake amejaza watu kwa sababu za kirafiki, kindugu sio kwa sababu ya performance ndio maana anakuwa mgumu kuchukua maamuzi kwa kuogopa kwanza lawama pili kupoteza marafiki na kujenga maadui wa kisiasa ambao kutokana na urafiki wao wanaweza wakawa wanajua madhaifu na madhambi yake mengi sana!mtu kama magufuli alionekana kufit kila wizara kwa ufanisi mkubwa kwa nn baada ya lowasa kulazimishwa kujiuzulu asingemteua waziri mkuu??jibu sio swahiba wake!wewe ukiona rais ambaye always analalamika na kuorodhesha matatizo bila suluhisho huyo sio rais!!
 
Ukweli ni kwamba tuna ombwe la uongozi Tanzania.2015 ni mbali sana hapa tulipofika.Najua wabunge walikuwa na maana zaidi ya ile waliyoonyesha katika kikao kilichopita.MH.JK asome alama za nyakati.NA ikimpendeza aombe kuachia ngazi tu.dalili ni mbaya tena Mbuya kweli kweli.
 
Tuliwahi ambiwa kuwa duniani kuna umasikini lakini umasikini mkubwa kuliko wote ni umasikini wa mawazo, duniani kuna kutegemea lakini kutegemea kubaya kuliko kote ni kutegemea kwa mawazo, hii ndio shida tulionayo huko juu kila kitu unataka wengine watoe mawazo kwanza ili upate wa kumlaumu. Yeye aliwahi kutuambia akili za mbayuwayu changanya na zako mbona yy hachanganyi na zake? MM umesema kweli wakulaumiwa ni yeye na wala sio watendaji.
 
Sijawahi kuona raisi mdhaifu kama JK ambaye anauwezo wa kuteua mawaziri lakini hawezi kuwafuta kazi mpaka aombe ridhaa. Huu ni udhaifu mkubwa ambao unaligharimu taifa na kulifanya taifa hili lizidi kuwa maskini.

Jk anafanana amekuwa kama roboti kama vile anaendeshwa na remote
 
Mwalimu Jk Nyerere aliona mbali sana,ndo maana 1995 alimwambia Jk bado mdogo alimwona jinsi alivyokuwa!. Kwa kweli angekuwepo Nyerere Pengine kikwete angeshika madaraka ya urais kwa miaka 5 tu! Nadhani tungekuwa sasa hivi tuna Rais mwingine. Haiwezekani tuwe na serikali ya kiskaji namna hii.
 
Akili zetu bana, eti baba akila mboga kwa fujo wanasema kaipenda ila mtoto akifanya hivyo wanasema anakomba mboga.Tuwe wakweli, "mtawala" ni dhaifu na hata yeye anafahamu hilo....kama tungekuwa na uwezo wa kuweka "chunvi" kwenye "matawi" hakika mti ungekauka.
 
Back
Top Bottom